Kuna kazi au Majukumu mwanamke au Mwanaume akiziweza kuoa inakuwa kipengele

Kuna kazi au Majukumu mwanamke au Mwanaume akiziweza kuoa inakuwa kipengele

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
KUNA KAZI AU MAJUKUMU MWANAMKE AU MWANAUME AKIZIWEZA KUOA INAKUWA KIPENGELE.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

1. Chunguzi zangu zinaonyesha hivyo.

2. Wanaume kadiri anavyoshindwa majukumu Fulani anayoyaweza Mwanamke na kuyamudu majukumu ya kiume ndivyo anavyokuwa husband material. Vivyohivyo na Mwanamke.

3. Ni nadra Sana umkute Mwanaume anayeweza majukumu ya kike hapohapo akawa Husband material. Hawa ni wachache na ni ndoto za Wanawake wengi. Halikadhalika na wanawake wanaoweza Majukumu ya kiume na hapohapo akawa wife material hawa ni wachache Sana na ni ndoto ya wanaume wengi.

4. Nitakupa Mifano ili unielewe;

5. Yapo majukumu ambayo wanaume huona uvivu kuyafanya. Na wakifanya hufanya ilimradi.

5. Majukumu ya nyumbani Kama kupika, kufua, kuosha vyombo, kusafisha nyumba, kuogesha na kucheza na watoto ni majukumu magumu Sana kwa wanaume wengi.

6. Kwa upande Wangu, Sipendi sijui niseme ni mvivu kuosha vyombo tangu nikiwa mdogo. Hali iliyopelekea viboko vingi kutembea inapofikia zamu zangu.

7. Wanaume wengi kuosha vyombo ni kipengele. Na unaposhindwa kuosha vyombo automatically kupika utaona ni kipengele.

8. Sijajua ni nini ila vyombo hata viwe viwili vitatu. Hasa na masufuria inakua kipengele.

9. Wakati nasoma chuo kikuu nilipokuwa napokea boom nilikuwa nanunua stock ya kutosha ya chakula cha miezi miwili. Kipengele ikawa kupika. Ukipika Leo mziki unatokea Kesho kuosha vyombo.

10. Marafiki wakike walikuwa wakija wanaweza kukuta vyombo vya Siku hata tatu nne. Solution ikawa Mimi nanunua msosi wa kupika wapishi wapo wanakuja wanapika maisha yanaenda. Wao wanapata urahisi wa kutotoa hela yao wanatoa huduma ya mapishi na kuosha vyombo. Mimi natoa pesa ila sipiki na sioshi vyombo.

11. Wanaume wavivu wa kazi za nyumbani ni rahisi kuwapenda Wake zao na kuona umuhimu wa Mwanamke/Mke. Kwani wanajua mziki wa kazi za nyumbani.

12. Mke akisafiri wiki moja mwanaume anateseka Sana. Vyakula vya migahawani sio vizuri kivile. Vidogo, havijapikwa vile utakavyo. Kupika unasikia uvivu.

13. Kama binti au dadaangu akiniambia aolewe na mwanaume yupi, Kati ya mchapakazi wa kazi za nyumbani au Mvivu wa kazi za nyumbani. Nitamshauri aolewe na mvivu wa kazi za nyumbani. Kwa sababu;

14. Wavivu kiasili wapo Smart 🤓 tofauti na wachapakazi. Wavivu ni rahisi wewe kama binti Yangu kuonyesha tija na nafasi yako ndani ya nyumba. Unaweza hata kuwatingisha mara mojamoja ili kushinikiza Jambo Fulani.

15. Wavivu sio wanyanyasaji. Wana appreciate umuhimu wako. Na nikuambie tuu wanaume wavivu watatafuta namna ya kurahisisha kazi hapo nyumbani kwa kununua mashine kama za kufulia, majiko ya kisasa ya kupikia n.k.

16. Wavivu ni rahisi mara nyingi kununua vyakula vya hapa na pale Siku ukisema hujisikii kupika. Lakini wachapakazi kiasili ni wabahili.

17. Wachapakazi nadra Sana kukuambia pole, ku- appreciate, kukusifia. Wao muda mwingi ni kujaji chakula Leo umeongeza maji, sijui chumvi, sijui imekauka Sana. Kwa sababu wanajua na wanauwezo wa kuingia jikoni.

18. Wachapakazi sio tegemezi. Ukiondoka hata ukae mwezi mmoja. Sio ajabu asione gap. Kupika anapika mwenyewe.
Utajipigilisha simu wewe yeye wala Hana habari. Lakini Wavivu ni tegemezi.

19. Mimi kama Kakaako, na Babaako. Ndoa na mahusiano msingi wake Mkuu ni Ufanano alafu pili ni Utegemezi; lazima mwenzako kuna Jambo analokutegemea Sana. Na kama Hilo Jambo halipo basi kwenye maisha yake wewe ni irrelevant.

20. Kama kuna kazi ngumu kwa Mwanamke ni Kutafuta Pesa. Wanawake wengi hawana uwezo wa kutafuta Pesa. Na hawapendi kwani ni kazi ngumu Sana kwao.

21. Kumbuka wanawake kiasili hawapendi mambo ya kutumia Akili na nguvu nyingi. Wanapenda mambo mepesi yasiyohitaji akili na nguvu nyingi.

22. Kutafuta pesa inahitaji akili na nguvu.

23. Iko hivi. Nje ya kuajiriwa kwenye kazi za kisomi. Wanawake wengi hawana ujanja wa kuzisaka chapa. Huo uwezo wa kuuza vitumbua au kushona nguo mpaka aje awe mfanyabiashara walau wa kumiliki milioni tano. Wengi hawana huo uwezo. Wengi wanaishia kupata vilaki mbili tatu mpaka laki tano. Hao WA laki tano ndio waliofanikiwa.

24. Sasa ukimwona mwanamke mchapakazi wa kuzalisha Mali na anajiweza ni ngumu Sana kuona umuhimu wa mwanaume yaani ndoa.

25. Inashauriwa kwa kijana anapotaka kuoa kama anataka utulivu basi aoe mwanamke mvivu wa kiutafutaji. Huyo atakuwa tegemezi kwako.

26. Ni ngumu kumbabaisha mwanamke mzalishaji au mwenye kipato. Na ukiona anakunyenyekea na kukuvumilia maujinga yako basi tambua ni kwa sababu ya familia hasa watoto.

Kufikia hapo sina la ziada

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ni kweli na ni irrelevant pia at some point. Tabia za binadamu ni mtambuka, ni vigumu sana kuziweka kwenye makundi kirahisi ivyo. Wapo wanawake ni wavivu na hawadumu kwenye ndoa zao, pia kuna wanaume wengi ni wavivu wa hzo kazi za nyumbani lakini ni wabahili, wanyanyasaji na hawajali wake zao.
 
Aisee kila kukicha kuna jipya 🙌

Enhee kwahiyo unasema mwanaume asiweza au asiependa au kumudu kazi unazoziita za kike ni rahisi kuitaji mwanamke na akimpata ana mheshimu🤔

Kwa hiyo huyo mwanaume tajwa hapo juu 👆
Yeye anaoa kwa sababu hiyo tu basi

Na mwanaume anaeweza kufanya kazi zote hizo yeye hana haja saana na mwanamke maana ana jiweza


Wanaume Hivi hua mnaoa kwanini?
Ni kama alivyosema Robert Heriel Mtibeli
 
Ina maana nikimwona mwanaume HAJAOA ujue anamudu majukumu ya kike? na mashoga je?
 
26. Ni ngumu kumbabaisha mwanamke mzalishaji au mwenye kipato. Na ukiona anakunyenyekea na kukuvumilia maujinga yako basi tambua ni kwa sababu ya familia hasa watoto.
Kwani lengo la kuoa mwanamke ni ili umbabaishe?

Mwanamke yoyote anatakiwa kujua nafasi ya mume wake kwake hata kama ana mali kiasi gani elimu level gani
Kwa sababu bado ana hitaji lake la kimwili ili likamilike na apate utulivu ana muhitaji huyo mwanaume

Ukiona mwanamke ni mjeuri kwa mume kisa mali kama unavyosema hapo nyuma lazima kuna kitu sio bure

Pengine mwanaume ana tabia mbaya
So mwanamke anaamua kumunyoosha

Au tu pengine mwanamke ana jeuri na mbinafisi

Lakini mbali na hapo kila mtu ana muitajia mwenzie kwa namna yoyote kwa sababu ni natural
 
roby upo sahihi
ukiolewa na mwanaume anayeyajua majukumu ya mwanamke utajuta
mara leo chumvi imezidi
nyumba leo hujaisafisha vizuri
na wanaume wa hivyo huwa hawadumu na wanawake
Sidhani kujua majukumu ya mwanamke kuna haribu ndoa
Mwanaume unaemsema hapo ni ana gubu hilo ni gubu
Kuna mwanaume hawezi chochote still ana lendenda kama hivyo
 
Binafsi yangu umuhumi wa kuoa nauona pale ambapo ukiugua,zaidi ya hapo hakuna maana yoyote ya kuoa.
Kama huna nia ya kuoa,jitahidi utafute pesa ili zije kukusaidia ukuumwa.
 
Ukiweza kila kitu, utaishia kuishi peke yako kwa sababu hakuna binadamu atakayeweza ku-fit kwenye standard zako.

Stay a bit flawed to stay married!
 
Kwani lengo la kuoa mwanamke ni ili umbabaishe?

Mwanamke yoyote anatakiwa kujua nafasi ya mume wake kwake hata kama ana mali kiasi gani elimu level gani
Kwa sababu bado ana hitaji lake la kimwili ili likamilike na apate utulivu ana muhitaji huyo mwanaume

Ukiona mwanamke ni mjeuri kwa mume kisa mali kama unavyosema hapo nyuma lazima kuna kitu sio bure

Pengine mwanaume ana tabia mbaya
So mwanamke anaamua kumunyoosha

Au tu pengine mwanamke ana jeuri na mbinafisi

Lakini mbali na hapo kila mtu ana muitajia mwenzie kwa namna yoyote kwa sababu ni natural

Sio lazima Kila MTU anamhitaji mwenzake.

Lazima mtu utengeneze kuhitajiwa/kutegemewa.

Mtu anaoa/anaolewa kwa sababu anauhitaji Fulani. Uhitaji huo usipotimizwa ndoa inakuwa haina maana


Kumbuka watoto wanaweza kupatikana bila ya ndoa
 
kuna mdogo wangu hajui chochote hata kupika maji hajui lakin mkewe anaish kama mtumwa ngumi mixa kaul mbovu
 
roby upo sahihi
ukiolewa na mwanaume anayeyajua majukumu ya mwanamke utajuta
mara leo chumvi imezidi
nyumba leo hujaisafisha vizuri
na wanaume wa hivyo huwa hawadumu na wanawake

Kuna Bro wangu anajua kupika kuliko wanawake wengi. Mke wake ameshamzoea kulalamika.
Kila akipika lazima chakula kikosolewe. Na ukiangalia kweli jamaa ni fundi

Wee ogopa mtu anarudi saa tatu usiku alafu anaingia jikoni kupika😆😆
Sisi wavivu kwa kweli hiyo haiwezekani.

Hivyo mwanamke anapata urahisi kupitia uvivu wetu. Lakini Mwanaume mchapakazi na anayejua majukumu ya home, aiseeh ninaowajua ni walalamishi mpaka unamwambia Bro hii sasa too much.
 
Sidhani kujua majukumu ya mwanamke kuna haribu ndoa
Mwanaume unaemsema hapo ni ana gubu hilo ni gubu
Kuna mwanaume hawezi chochote still ana lendenda kama hivyo

Upo sahihi kwa kiasi.
Ila MTU ambaye hakutegemei kwa lolote mahusiano yenu yapo mashakani Sana.

Hutanielewa
 
Back
Top Bottom