KUNA KAZI AU MAJUKUMU MWANAMKE AU MWANAUME AKIZIWEZA KUOA INAKUWA KIPENGELE.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
1. Chunguzi zangu zinaonyesha hivyo.
2. Wanaume kadiri anavyoshindwa majukumu Fulani anayoyaweza Mwanamke na kuyamudu majukumu ya kiume ndivyo anavyokuwa husband material. Vivyohivyo na Mwanamke.
3. Ni nadra Sana umkute Mwanaume anayeweza majukumu ya kike hapohapo akawa Husband material. Hawa ni wachache na ni ndoto za Wanawake wengi. Halikadhalika na wanawake wanaoweza Majukumu ya kiume na hapohapo akawa wife material hawa ni wachache Sana na ni ndoto ya wanaume wengi.
4. Nitakupa Mifano ili unielewe;
5. Yapo majukumu ambayo wanaume huona uvivu kuyafanya. Na wakifanya hufanya ilimradi.
5. Majukumu ya nyumbani Kama kupika, kufua, kuosha vyombo, kusafisha nyumba, kuogesha na kucheza na watoto ni majukumu magumu Sana kwa wanaume wengi.
6. Kwa upande Wangu, Sipendi sijui niseme ni mvivu kuosha vyombo tangu nikiwa mdogo. Hali iliyopelekea viboko vingi kutembea inapofikia zamu zangu.
7. Wanaume wengi kuosha vyombo ni kipengele. Na unaposhindwa kuosha vyombo automatically kupika utaona ni kipengele.
8. Sijajua ni nini ila vyombo hata viwe viwili vitatu. Hasa na masufuria inakua kipengele.
9. Wakati nasoma chuo kikuu nilipokuwa napokea boom nilikuwa nanunua stock ya kutosha ya chakula cha miezi miwili. Kipengele ikawa kupika. Ukipika Leo mziki unatokea Kesho kuosha vyombo.
10. Marafiki wakike walikuwa wakija wanaweza kukuta vyombo vya Siku hata tatu nne. Solution ikawa Mimi nanunua msosi wa kupika wapishi wapo wanakuja wanapika maisha yanaenda. Wao wanapata urahisi wa kutotoa hela yao wanatoa huduma ya mapishi na kuosha vyombo. Mimi natoa pesa ila sipiki na sioshi vyombo.
11. Wanaume wavivu wa kazi za nyumbani ni rahisi kuwapenda Wake zao na kuona umuhimu wa Mwanamke/Mke. Kwani wanajua mziki wa kazi za nyumbani.
12. Mke akisafiri wiki moja mwanaume anateseka Sana. Vyakula vya migahawani sio vizuri kivile. Vidogo, havijapikwa vile utakavyo. Kupika unasikia uvivu.
13. Kama binti au dadaangu akiniambia aolewe na mwanaume yupi, Kati ya mchapakazi wa kazi za nyumbani au Mvivu wa kazi za nyumbani. Nitamshauri aolewe na mvivu wa kazi za nyumbani. Kwa sababu;
14. Wavivu kiasili wapo Smart 🤓 tofauti na wachapakazi. Wavivu ni rahisi wewe kama binti Yangu kuonyesha tija na nafasi yako ndani ya nyumba. Unaweza hata kuwatingisha mara mojamoja ili kushinikiza Jambo Fulani.
15. Wavivu sio wanyanyasaji. Wana appreciate umuhimu wako. Na nikuambie tuu wanaume wavivu watatafuta namna ya kurahisisha kazi hapo nyumbani kwa kununua mashine kama za kufulia, majiko ya kisasa ya kupikia n.k.
16. Wavivu ni rahisi mara nyingi kununua vyakula vya hapa na pale Siku ukisema hujisikii kupika. Lakini wachapakazi kiasili ni wabahili.
17. Wachapakazi nadra Sana kukuambia pole, ku- appreciate, kukusifia. Wao muda mwingi ni kujaji chakula Leo umeongeza maji, sijui chumvi, sijui imekauka Sana. Kwa sababu wanajua na wanauwezo wa kuingia jikoni.
18. Wachapakazi sio tegemezi. Ukiondoka hata ukae mwezi mmoja. Sio ajabu asione gap. Kupika anapika mwenyewe.
Utajipigilisha simu wewe yeye wala Hana habari. Lakini Wavivu ni tegemezi.
19. Mimi kama Kakaako, na Babaako. Ndoa na mahusiano msingi wake Mkuu ni Ufanano alafu pili ni Utegemezi; lazima mwenzako kuna Jambo analokutegemea Sana. Na kama Hilo Jambo halipo basi kwenye maisha yake wewe ni irrelevant.
20. Kama kuna kazi ngumu kwa Mwanamke ni Kutafuta Pesa. Wanawake wengi hawana uwezo wa kutafuta Pesa. Na hawapendi kwani ni kazi ngumu Sana kwao.
21. Kumbuka wanawake kiasili hawapendi mambo ya kutumia Akili na nguvu nyingi. Wanapenda mambo mepesi yasiyohitaji akili na nguvu nyingi.
22. Kutafuta pesa inahitaji akili na nguvu.
23. Iko hivi. Nje ya kuajiriwa kwenye kazi za kisomi. Wanawake wengi hawana ujanja wa kuzisaka chapa. Huo uwezo wa kuuza vitumbua au kushona nguo mpaka aje awe mfanyabiashara walau wa kumiliki milioni tano. Wengi hawana huo uwezo. Wengi wanaishia kupata vilaki mbili tatu mpaka laki tano. Hao WA laki tano ndio waliofanikiwa.
24. Sasa ukimwona mwanamke mchapakazi wa kuzalisha Mali na anajiweza ni ngumu Sana kuona umuhimu wa mwanaume yaani ndoa.
25. Inashauriwa kwa kijana anapotaka kuoa kama anataka utulivu basi aoe mwanamke mvivu wa kiutafutaji. Huyo atakuwa tegemezi kwako.
26. Ni ngumu kumbabaisha mwanamke mzalishaji au mwenye kipato. Na ukiona anakunyenyekea na kukuvumilia maujinga yako basi tambua ni kwa sababu ya familia hasa watoto.
Kufikia hapo sina la ziada
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam