Kuna kiashiria chochote cha tabia kwa mtoto anayenyonya kidole?

Ni ukweli. Inakuwa mijinga mijinga na mizembe. Amuwahi hiyo tabia aache. Huwa wanakuwa mafala
 
Mdogo wangu anakaribia 18 yrs na bado ananyonya vidole
Tulipaka upupu, shubiri sijui alovera, pilipili tulifunga hadi plaster lakini hakuacha
Aisee, poleni sana!
 
Mimi wa kwangu nilimpaka pilipili wapi zaidi anajiminya macho ikawa inamuwasha nikaacha nikavikata kiaina kwa wembe lakini wapi akalia kwa ule muda kaona damu baadae nakutana naye anyonya nikaachana nae
Alikuja kuacha mwenyewe akiwa na miaka 9, haya mdogo wake kwa sasa ana miaka 5 yumo tu kwenye kunyonya mbaya zaidi nae ni vidole gumba vyote.
Ko huyo wa kwako muache atacha tu muda ukifika.
 
Ilikuaje hadi akafikia hatua hiyo?
Hakuna anayejua! Tuliona tu akitaka kulala basi lazima akinyonye kidole ndo usingizi unamjia vizuri......hiyo akiwa mdogo sana!
 
Ahsante sana kwa alert hii
 
Ahsante
 
Oh, shukrani mkuu!
 
Mimi nilikuwa nayonya vidole viwili mpaka miaka 18 nikaacha mwenyewe mimi nilikuwa nayonya huku nafinya finya sikio la kulia, mpaka leo linakujika lenyewe mpaka watu wananishangaa😃
🤣🤣🤣
Bila kukuna hilo sikio unajisikiaje?
 
Ahsante sana!!
 
Hata mdogoangu alikuwa anatabia hiyo akiwa mdogo Hadi anafikisha miaka 7 hapo faza akaamua amuachishe kinguvu alitumia mbinu hii na ilifanya kazi.

Alimwita Kama kumkatakucha mikononi harafu akamkata jeraha dogo kwenye kidole husika baada ya hapo akamuwekea bonge la bandeji katika hicho kidole baada ya wiki alipo itoa bandeji, dogo hajawahi nyonya Tena Hadi leo ana miaka 30.
 
Ni kawaida japo kwangu mm najitahidi kumkataza toka akiwa mdogo mfano mwangu wa kiume alianza kula mikono toka akiwa na 2mnth ukimbeba anaweka mkono mdomoni anaanza kutafuta pozi la kidole gani anyonye nikajitahidi kumkataza na mama yake akafanya hivyo mpaka kakua akawa ameacha bila kupaka pilipili. Usihofu ni tabia ya kawaida ukitaka asizoee mikono mnunulie pacifier itamkeep busy muda ambao ananyonya vidole. Na haihusiani na mtoto kushiba au kutoshiba
 
Kisaikolojia hii ina implication mara nyingi watoto wanaofanyiwa ukatili, manyanyaso, kutengwa au wasioridhishwa na mwenendo wa mambo flani flani katika malezi yao (mfano kuachishwa nyonyo kablabla ya muda kutokana na ubize wa ma, mama kumuacha mwanae na hausigeli ilihali mtoto anaona watoto wenzie wanabeng na mama zao n.k)

Watoto wa ana nilizotaja hapo juu kua wakati (sio lazima) hudevelop vijitabia vya dizaini hizo kama namna ya kujifariji na mara nyingi hii huendelea hadi utu uzima kama chanzo kisipotibiwa mapema
 
Tatizo lipo. Meno yake ya mbele hasa ya juu hayatakuwa sawia. Nashindwa kuelezea vizuri ila kuna mbunge mmoja mwanamke na ni waziri nimemsahau jina, mweupe meno yake ya juu ni uthibitisho tosha kuwa utotoni alinyonya vidole. Huo ni uhakika 💯%. Uliza hata wengine watu wazima km mimi watakuambia hivihivi, ila kiafya hakuna madhara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…