Kuna kiashiria chochote cha tabia kwa mtoto anayenyonya kidole?

Mfunge plasta hicho kidole anachonyonya mpaka atakaposahau na kuacha.wakati mwingine inakujaga kuwa ngumu sana kumuachisha mtoto kidole akiishazoea sana
 
Wa kwangu ananyonya mdomo wa chini tena nusu na anajaribia miaka mitano, tushakemea sana lakini wap..
 
Haina shida hata kidogo wala usihofu. Usikubali kufuata ushauri wa watu makatili eti paka pilipili au mambo mengine. Kwenye familia yetu karibu kila mtu alikuwa ananyonya kidole na wengine wamenyonya mpaka walipofikisha miaka 7 na 9. Wazazi wetu walikuwa wasomi hivyo haikuwa ni issue kwao. Pia najua watoto wengi walinyonya na vidole na wamekuwa kama watoto wengine. Tena kuna dhana kwamba wanaonyonya vidole mara nyingi huwa na akili nzuri ukubwani. La muhimu mwache anyonye kwa raha zake na akikua ataacha.
 
Hakuna shida hiyo ni tabia ambayo iko kwenye kizalia cha ukoo/familia.. In fact mtoto anayenyonya kidole sio msumbufu

Sent using Jamii Forums mobile app
Sahihi kabisa Niko nao wawili mtu na dada yake warembo haswaa mdogo miez 11 mkubwa miaka 3, 8/12 hawana tabu kabisa wamerithi kwa mama Yao
 
Mama yake alikuwa anamwacha analala ilhali ziwa liko mdomoni?
Watoto hata wawe wadogo kiasi gani, wanatakiwa wawe na kitanda Chao. Sasa kama mpaka ana miaka 2 analala na mtu mzima akiwa anachezea kiwiko au kama nilivyoanza, pengine alizoeshwa kulala ziwa likiwa mdomoni. Sasa kiashiria ni ninyi wazazi mlimvyomzoesha sio yeye.
 
Kuna mwanangu nlkuwa na university pale yuko 26 now na mindevu kabisa

Yani unaeza ingia ghetto kwake unakuta ako bize na simu huku kaweka kidole gumba mdomoni
 
Niliacha kunyonya vidole baada ya kuanza darasa la kwanza. Home ilifikia hatua hadi nilikuwa navalishwa soksi kwenye mkono πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜….

Nilikuwa napenda kunyonya vidole viwili vya kati, vya mkono wa kushoto. Na nikivinyonya, huu mkono mwingine lazima nijishike sikio au chuchu, au hata kumshika sikio sehem ya hereni aliyekuwa pembeni yangu
 
Tafiti zinasema watoto wanaopenda kunyonya vidole uwezo wao wa kufikiri ni mdogo, wakiwa wakubwa wakikumbana na msongo wa mawazo ni rahisi kusambaratika hawawezi kujipagania wenyewe.
 
🀣🀣🀣
Natamani nipate sababu hisia za kushika hayo maeneo. Kwa mfano huyu wangu lazima akushike kiwiko cha mkono wakati ananyonya hicho kidole chake kama upo karibu......lazima!!
 
Na wakianza kuota meno, Ronaldinho aingii ndani...
 
Mwanafunzi mmoja wa kidato cha sita, alikuwa ananyonya kidole. Mpaka ukubwani eti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…