Kuna kikundi kinapinga Rais Samia kuongea na upinzani

Ni kweli kabisa, wapo wahafidhina ndani ya chama tawala ambao wana sauti kubwa ndani ya chama, serikali na vyombo vya ulinzi na usalama hapa nchini. Wanatambua fika CCM ilipoteza mvuto na ushawishi wake kwa umma toka mwaka 2010.

Kwa hiyo wanatambua fika ya kwamba ili kuweza kupambana na upinzani, njia pekee iliyobakia kwao ni kwa kupitia tafu wabayoipata katika vyombo vya dola. CCM iliyokuwa na hoja za kiushindani dhidi ya upinzani ilikuwa mwisho wake ni katika nyakati za utawala wa hayati wa hayati Mkapa.
Uongo mweupe huo.....

CCM ya 2015 ilikuwa na sera ya "hapa kazi tu"....

Hayati JPM alitekeleza kivitendo malalamiko ya watanzania dhidi ya UFISADI/MAFISADI PAPA.....

Cha ajabu baadhi ya waliokuwa watuhumiwa wa ufisadi na ambao walichafuliwa sana na CHADEMA ndio haohao waliokuja KUSAFISHWA KWA DODOKI kupitia "kubadilisha gia angani alikosema mh.Mbowe".....

#SiempreCCM
#KaziIendelee
 
Nimemsikiliza Lissu kwenye mahojiano akasema ikulu inamwambia watampigia simu halafu ikifika wakati kuna njama zinafanyika kuhakikisha Mama anashidwa kuongea naye.

Tujue kuwa kuna wafaudika wakubwa hata ndani ya usalama mfano mitambo ya kudukuwa simu nani katoa budget! Watekaji nani anawalipa, pesa za kununua wapinzani nani anatoa haya ni mabilioni ambayo wanaohopa kuyakosa.

Rais Samia asikokuwa makini hawa jamaa watahakikisha kuna fujo ili waendelee na biashara zao
Lissu anaongea na samia kitu gani. Lissu kazi yake kukashifu kusema uongo na kuzua mambo. Mwanasiasa kama huyo unaongea naye nini. Maana hata kura hawana hawana kitu kisiasa wamekwisha.
 
Ni kweli kabisa, wapo wahafidhina ndani ya chama tawala ambao wana sauti kubwa ndani ya chama, serikali na vyombo vya ulinzi na usalama hapa nchini. Wanatambua fika CCM ilipoteza mvuto na ushawishi wake kwa umma toka mwaka 2010.

Kwa hiyo wanatambua fika ya kwamba ili kuweza kupambana na upinzani, njia pekee iliyobakia kwao ni kwa kupitia tafu wabayoipata katika vyombo vya dola. CCM iliyokuwa na hoja za kiushindani dhidi ya upinzani ilikuwa mwisho wake ni katika nyakati za utawala wa hayati wa hayati Mkapa.

You nailed it, ccm imeshapoteza ushawishi kwa umma, na hicho kikundi cha walaji kinachojiita system, kinajua fika mama akiongea na wapinzani kisha akalazimika kuweka uwanja sawa wa kufanya siasa, ni hatari kwa ccm, lakini kukubwa zaidi na mlo wao kupotea. Hao wanaojiita system wengi ni wenye vyeo kwenye taasisi za umma, na viongozi wastaafu wanaoendelea kulipwa mpaka wafe. Wanajua ccm ikitoka madarakani mbali ya kupoteza ulaji, hata jela wataishia kwa uhuni walioufanya.
 
Uongo mweupe huo.....

CCM ya 2015 ilikuwa na sera ya "hapa kazi tu"....

Hayati JPM alitekeleza kivitendo malalamiko ya watanzania dhidi ya UFISADI/MAFISADI PAPA.....

Cha ajabu baadhi ya waliokuwa watuhumiwa wa ufisadi na ambao walichafuliwa sana na CHADEMA ndio haohao waliokuja KUSAFISHWA KWA DODOKI kupitia "kubadilisha gia angani alikosema mh.Mbowe".....

#SiempreCCM
#KaziIendelee
Mkuu hivi kiuhalisia, Je! Unafikiri ni nani ambaye akishinda katika nafasi ile ya kinyang'anyiro urais wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kati ya Edward Lowassa na JPM. Ilikuwa ni kupitia mbeleko la vyombo vya dola na tume ya uchaguzi isiyokuwa huru na ya haki ndipo matokeo yalipotangazwa.
 
Alisema ana taarifa za uhakika bodyguard wa magufuli kafariki ila tukamuona, lissu muongo sana
Yaani mh.Lissu ni "pathological lier".....

Nilitegemea asafishe hali ya hewa kwa kuomba msamaha kuwa ALIDANGANYA kuhusu yule ndugu....daah mpaka leo amebaki kimya.....

Mh.TL haaminiki......
 
"Pang'ang'a" za Tundu Lissu tu hizo....

Jamaa ni bingwa wa kuchezea maneno....hajali hata kama ni ya UONGO.....

#KaziIendelee
#NchiKwanza
#SiempreSSH

Na yeye ni kama Majaliwa kuwa Magufuli ni mzima na yuko ofisini anapiga kazi, hivyo tupuuze uzushi wa mitandaoni na watu wasiolitakia mema ya letu?
 
Mkuu hivi kiuhalisia, Je! Unafikiri ni nani ambaye akishinda katika nafasi ile ya kinyang'anyiro urais wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kati ya Edward Lowassa na JPM. Ilikuwa ni kupitia mbeleko la vyombo vya dola na tume ya uchaguzi isiyokuwa huru na ya haki ndipo matokeo yalipotangazwa.
Kufikiri?!!

Uhalisia ni kuwa JPM aliyekuwa anaaminika na wananchi wengi kwa uzalendo wake kuntu ,usafi wa maadili ,kukosa makandokando kulimpelekea kupata kura ZOTE ZILE...

It's a fact not fictitious......

#KaziIendelee
 
Na yeye ni kama Majaliwa kuwa Magufuli ni mzima na yuko ofisini anapiga kazi, hivyo tupuuze uzushi wa mitandaoni na watu wasiolitakia mema ya letu?
Labda unataka tu kukomalia jambo lililokuwa wazi.....

Kwani mh.Kassim Majaliwa aliitoa hiyo "statement" wiki kadhaa kabla ya mh.Rais kututangazia MSIBA.....
 
Kuna wana CCM kwenye kamati kuu yao wanataka kumharibia mama kwenye uongozi wake, awe makini sana na watu hao.

Leo mama yupo mtu kati kuhusu kesi ya ugaidi...wao wapo poa tu na wake zao.
 
You nailed it, ccm imeshapoteza ushawishi kwa umma, na hicho kikundi cha walaji kinachojiita system, kinajua fika mama akiongea na wapinzani kisha akalazimika kuweka uwanja sawa wa kufanya siasa, ni hatari kwa ccm, lakini kukubwa zaidi na mlo wao kupotea. Hao wanaojiita system wengi ni wenye vyeo kwenye taasisi za umma, na viongozi wastaafu wanaoendelea kulipwa mpaka wafe. Wanajua ccm ikitoka madarakani mbali ya kupoteza ulaji, hata jela wataishia kwa uhuni walioufanya.
Unataka kutuaminisha kuwa mh.Rais na mwenyekiti wa CCM hakijui chama vilivyo?!!

Haijui misimamo ya chama vilivyo?!!

CCM ni imani na itikadi....chama hiki cha kijamaa kamwe hakiwezi kumpitisha mwenyekiti "mwepesi" aliye "bendera fuata upepo".......

#SiempreSerikaliMbiliZaJMT
#KaziIendelee
 
Nimemsikiliza Lissu kwenye mahojiano akasema ikulu inamwambia watampigia simu halafu ikifika wakati kuna njama zinafanyika kuhakikisha Mama anashidwa kuongea naye.

Tujue kuwa kuna wafaudika wakubwa hata ndani ya usalama mfano mitambo ya kudukuwa simu nani katoa budget! Watekaji nani anawalipa, pesa za kununua wapinzani nani anatoa haya ni mabilioni ambayo wanaohopa kuyakosa.

Rais Samia asikokuwa makini hawa jamaa watahakikisha kuna fujo ili waendelee na biashara zao
Fujo gani? mmmmuu
 
Back
Top Bottom