Kuna muda unaweza kuishiwa pesa hadi ukatamani kumkopa mdada wa kazi

Wengine hiyo misoto ndiyo tunaipitia sasa. Jana saa 1 jioni nilikuwa narejea home huku mfukoni nina 2500 tu. Hapo napiga hesabu ya nauli jero walau niingie home na buku 2.

Ile nakatiza Mlimani City service road uelekeo Lufungila kituo cha daladala nasimamishwa na dogo mdogo around miaka 10 au 11. Ananiomba hela anasema akale, hajala.

Huruma ikaniingia...nikampa yule dogo jero. Nikawaza japo nimefulia ila siwezi kumuacha huyu dogo hivi hivi. Nika sacrifice jero na kuvuruga bajeti yangu. Mungu atajua atakavyoleta riziki.

Sometimes nawaza kwa nini tupitie maisha ya shida namna hii...? Kwa nini tuna struggle to make the ends meet? Kwa nini kipato hakijitoshelezi? Hapa asubuhi kunakucha na nina jero tu, na majukumu yanayonikabili ni yanahitaji mamia ya shilingi.

Ninachomshukuru Mungu ni kuwa hata hali iwe ngumu vipi...solution ipo tu. Usikate tamaa.
 
Hii misimamo ya kikamanda sana.Yana mwisho chief.Itafikia wakati itakua ni simu moja ,tukutane benki.
 
Huwa namkopa mara nyingi tu! Kikubwa ni kuwa mwaminifu wa kulipa kwa wakati ili kulinda heshima yako
Unawezaje kumlipa kwa wakati? Yaani umkope tena Dada wa kazi halafu unamudu kumlipa kwa wakati bila kupitisha?
 
Kuna tatizo kwenye fursa
 
[emoji3][emoji3][emoji3]...
 
Daah hii mbinu inaitaji ufundi kweli ujue kuigiza


Mimi nawanangu tulikuwa tunaomba tuoshe vyombo na masufuria baada ya hapo unapewa msosi mishe imeisha
 
Ni changamoto tu wakuu,kila kitu kitakua sawa amini hivyo! Kila mmoja ana zake zinatofautiana tu ukubwa..na kupitia uzi kama huu ndio utaona si ajabu wewe una nafuu sana..tusikate tamaa.!
 
Kumbe hasira zote kwa jiwe sababu ya ufukara wako
Hakuna mtu fakara/Mnyonge anayemchukia Jiwe. Hao ndiyo walikuwa mtaji wake, ref wewe mwenyewe. Kuishiwa pesa ni jambo la kawaida unless wewe umekuja duniani jana au akili zako ndivyo hivyo tena mzee wa kujiita mnyonge
 
Hakuna mtu fakara/Mnyonge anayemchukia Jiwe. Hao ndiyo walikuwa mtaji wake, ref wewe mwenyewe. Kuishiwa pesa ni jambo la kawaida unless wewe umekuja duniani jana au akili zako ndivyo hivyo tena mzee wa kujiita mnyonge
sasa na hela zako za mbio utampendaje jiwe!!

ni upuuzi kujiita imara na unaishi chini ya $10 kwa siku.
 
Acha kutudhihaki mkuu. Km umetusua maisha ni jambo la kumshukuru Mungu.
Jiwe ameshakufa.
sasa na hela zako za mbio utampendaje jiwe!!

ni upuuzi kujiita imara na unaishi chini ya $10 kwa siku.
 
Mie nilipigika ile kisawa sawa nikamwomba x afanye backup hahaha sharti ikawa turudiane daaah nikakubali akanipa 300k

Baadae nikawa kwale kama wiki 2 nikarudisha na cha juu 400 hataki anataka turudiane

Wacha siku nipigike nimcheki akanikazia hahahaha
 
RISUG is the way now
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…