Kuna njia nyingine ya kupunguza uzito?

Kuna njia nyingine ya kupunguza uzito?

Naomba tu kuuliza Wakuu maana huu ubonge unanikwamisha nnashindwa hata kufunga kamba za viatu.

Nitumie njia gani ili niwe Mr. Slim sio BIG.

Na halafu nachukia sana mtu kuniona mimi fala, naomba km huna njia tafuta njia upite.

Nasubiria majibu yenu hapa chini.
Funga . Usiku kula kidogo .
 
Naomba tu kuuliza Wakuu maana huu ubonge unanikwamisha nnashindwa hata kufunga kamba za viatu.

Nitumie njia gani ili niwe Mr. Slim sio BIG.

Na halafu nachukia sana mtu kuniona mimi fala, naomba km huna njia tafuta njia upite.

Nasubiria majibu yenu hapa chini.
Njia pekee ya kupunguza uzito ni kupunguza kula (Food Intake), au kula kulingana na kazi unazofanya. Kama ulikua unafukia maugali, mawali na machips bila kushughulisha mwili. Punguza na anza kula vyakula vyepesi. Pia punguza vinywaji vikali au baridi. Au jiwekee utaratibu wa kufunga mara kadhaa kwa mwezi pamoja na kufanya mazoezi.
 
mimi nilijaribu hili ila nilikosa consistency tu yaani,nlikuwa nakula mlo mara moja tu kwa siku,hiko chakula ni kama mchesho wa kuku robo,mboga mboga nyng na tango au parachichi,nlipungua kilo 6 kwa siku 10
 
Funga saumu

kulima kwa jembe la mkono.

kuachana na mwanamke umpendae na sio akupendae.


Mikopo siyokuwa na bima [kausha damu]

vitakusaidia.
 
Naomba tu kuuliza Wakuu maana huu ubonge unanikwamisha nnashindwa hata kufunga kamba za viatu.

Nitumie njia gani ili niwe Mr. Slim sio BIG.

Na halafu nachukia sana mtu kuniona mimi fala, naomba km huna njia tafuta njia upite.

Nasubiria majibu yenu hapa chini.
Ni kupunguza kufakamia misosi ovyo na kufanya mazoezi.
 
Mimi nawaona tu watu mijini wakipiga tizi Kila Leo mara mwaka umesogea lakini uzito uko pale pale, yaani unapiga tizi halafu msosi unaokula ni ule ule wa kabla ya mazoezi, badala ya kupunguza kujishindia sana lakini mtu anadhani tiba ni mazoezi tu. Vyakula vyetu hivi vinahitaji nidhamu kuvitumia, lazima ujue unakula chakula gani na tupunguze chakula gani!, tatizo ni UROHO unatusumbua.
Hapa umenena jambo mkuu kwa hio ukitaka upungue haraka unabidi ufanyeje? Kwa experience yako wewe
 
Back
Top Bottom