Hapa umenena jambo mkuu kwa hio ukitaka upungue haraka unabidi ufanyeje? Kwa experience yako wewe
Kwanza, punguza kula wanga sana, kula matunda na mbogamboga(siyo zile za kukarangiza zilizojaa mafuta kibao, mboga simple tu) iwe sehemu ya maisha yako, mboga na matunda ni muhimu Kwa afya na pia vitaweza kukufidia Kwa kiasi ile sehemu ya wanga uliopunguza kula.
Pili, acha kula au punguza Kwa kiasi kikubwa kula junk foods, hizi hazifai kabisaaa, dada zetu karibu wote wana vitambi sababu ya chips, kuku za kukaanga, chipsi yai and the likes.
Tatu, acha matumizi ya vinywaji baridi na vyenye sukari nyingi mfano kama hizi soda, beer nk. Kinywaji chako ni maji tu tena ya kutosha kabisa. Acha vilevi vyote kama unatumia
Nne, Acha kula nyama nyekundu Kwa wingi. Nyama ya kula ni nyeupe tena si za kukarangiza kwa kiasi kikubwa. Hapa ndipo gharama unaweza kuingia baadhi.
Tano, Fanya mazoezi ya kutoa jasho kweli kweli, kama push ups huwezi basi jifunze, kimbia sana nk.
Sita, Punguza stress Kwa kiasi kikubwa. Stress hazizuiliki lakini kwanini zizidi?, basi tafuta njia ya kupunguza stress zisiwe mzigo.
Saba, Pata usingizi wa kutosha Kila siku, huwezi kufika lengo kama unalala Kwa kubahatisha, kinachohitajika ni ubora wa usingizi wenye muda mwingi wa kujipumzisha, jiwekee ratiba.
Nane, kuwa na muendelezo, siyo baada ya miezi sita unaacha unakata tamaa na hii ndio huwafanya watu wasipungue kilo zao.
Tisa, Anza kufunga Kwa muda Fulani kama wafanyavyo waumini wa dini au punguza Milo mathalani unakula mara mbili tu Kwa siku, hii nayo husaidia sana.
Kinachotuua ni misosi tu, mazoezi watu wengi hufanya lakini Bado mfumo wao wa kula ni ule ule, huwezi pungua hata ufanyie mazoezi mbinguni.
Wanasema kuwa "Weight loss is a journey and not a race"