1. Punguza kiwango Cha chakula ila usikae njaa.
2. Usiende gym Bali uwe unakimbia mara kwa mara hasa kwenye mpando angalau mara 3 kwa week asubuh na jioni.
3. Danganya mwili yaani ukiweza uwe unakula matunda, mboga za majani nyingi kabla ya chakula - yaani wakati wa kula uwe na sehem ya matunda mchanganyiko kula kwanza hayo ukimaliza ndo ule ugali,ubwavea,au chips zako. Usianze na chakula then matunda. Anza na matunda then chakula kdg.
4. Uwe na mda maalum wa kula: kutegemea kazi Yako: kama chai saa1, mchana saa6 na usiku saa12:30 au ukichelewa basi saa1 jioni. Usizidi hapo.
5.Weka ratiba ya kufunga japo mara2 kwa week,Hali ikiwa ngumu kufunga basi funga kwa kunywa maji au ukishindwa basi kula tunda na maji tu kwa siku nzima.
6. Ukiweza kulingana na afya Yako: kunywa kahawa saa 12 jioni. Kama itakuwa ni ofsni au pengine na huwezi kahawa basi tumia maji ya uvuguvugu Kila mara. Badala ya kunywa maji we jiwekee chupa ya maji moto ukae ukinywa hiyo.
7. Usitumie dawa za hospital mara mingi. Pima ila usitumie dawa tumia dawa za asili za kuchemsha ukiweza.
8.izo ni baadhi tu: kumbuka usijinyime vya kula uvipendavyo ila Kila Kitu ni kwa kiasi.
Naishia hapo kwa sasa; kwa implementation zaidi Inbox.
Asante.