Kuna pepo likiingia kwenye familia hutafuna vizazi vingi

[emoji1545][emoji817] umeongea kiroho zaidi.. I wish haya masomo ya utambuzi wa kiroho yangekuwa yanafundishwa kwenye taasisi zetu za elimu
 
Broo Mshana,,naomba usitutishe walamba asali!!!
 
Hapa nimekuelewa vizuri sana mzee. Asante kwa kutuelimisha maana elimu ni pana mno. Je wale wanaonunua wanawake wanaojiuza madhara yake yapoje ukilinganisha na hawa wanao amua kudumu kwa muda mrefu na aina hii ya watu?
 
[emoji3] trust me nimeacha ulozi na kumrudia Mungu mazima.. Si unajua kiza na nuru havikai pamoja? Niliamua kuchagua nuru na niko nuruni sasa[emoji173]
Ni kweli MshanaJr: uliwahi kuwa mganga/mtoa tiba za kiasili au ni kwa sababu tu ya kujua elimu ya mambo haya?
 
Nimejufunza kitu kikubwa hapaa.Asante sana
 
Hapa nimekuelewa vizuri sana mzee. Asante kwa kutuelimisha maana elimu ni pana mno. Je wale wanaonunua wanawake wanaojiuza madhara yake yapoje ukilinganisha na hawa wanao amua kudumu kwa muda mrefu na aina hii ya watu?

Lile nalo ni pepo baya sana hasa kama una familia
Imagine mwanamke unayemnunua ana joto na vinasaba vya wanaume wangapi aliolala nao? Kwahiyo unaingizwa kwenye mnyororo bila kujua
Mbaya zaidi sio wanaojiuza wote ni kwa ajili ya umasikini na kipato wengine ni ma agent wapo kuvuna manii kwa matumizi ya kishirikina

Kudumu na huyo mwenye hizo changamoto pia ni tatizo kwakuwa kuna mambo utafanya hayaendi na yakienda ni kwa msuli mkubwa sana

Unapata kipato kizuri lakini huna cha maana ulichonacho
Una kazi nzuri lakini hali yako na familia yako havilingani na hadhi ya kazi yako
Ni rahisi kutengeneza michongo ya pesa lakini pesa ukiitia tu mkononi kuna kitu cha dharura kinahitaji pesa kinatokea na kinakuhusu asilimia 100
Una pesa, una maisha mazuri lakini ndani ya familia kila siku ni changamoto haziishi nknk
 
Hiki ndicho walichokuwa wanakifanya mababu zetu zamani.. Unaweza kukataliwa ndoa kwasababu ya background ya familia
Hili lilikuwa jepesi kwakuwa sehemu kubwa ya jamii ilikuwa inakaa pamoja. Siku hizi miingiliano mingi, kumtrace mtu historia inakuwa ngumu. Tunaoana juu Kwa juu mno. Wazazi wakikataa, tunasema tunaingiliwa.

Hatari sana.
 
[emoji3]kidogo nilijaribu kufanya kwa vitendo.. Kidogo sana lakini
Hongera pia kwa kujifunza maisha, kila mtu anapitia mambo kadhaa katika maisha. Zote ni njia ila kujua njia sahihi ni neema tu na kila jambo linayo makusudi.
 
Kuhusu DNA na mnyororo unaouongelea ni Kweli kabisa. Hiyo Iko kibinadamu.

Shetani alifanikiwa kuingiza DNA yake Kwa WANADAMU baada ya Hawa kula tunda alilokatazwa na ndo mlango shetani alitumia kutesa WANADAMU.

Wamwaminio Mungu hubadilishiwa DNA za Kuzaliwa.

Mtu anaweza Toka kwenye uzao ambao ni MASKINI Kwa kurithi, wauaji Kwa kurithi, au wenye magonjwa ya kurithi nk nk.

Bt aaminipo anabadilishiwa DNA, mababu na mizimu ikimtafuta ktk frequency zao wanamkosa.

Sisi Wana wa Mungu Kutoka juu, tukimpokea mtu aliyetoka kwenye vifungo vya kiukoo, Huwa tunamtenganisha na ukoo wake na tunamsajili ktk ukoo wa Wana wa Mungu.

Mtu mmoja alikuja kuomba msaada baada ya kustukia jambo Fulani baya lililokuwa linafuata familia Yao,

Walizaliwa watoto 6, Yeye alikuwa mtoto wa mwisho, waliandamwa na vifo vilivyofuatana ktk tarehe, na mwezi.

Ilikuwa Kila ilifika tarehe hiyo na Mwizi huo atafariki mmoja wa wanafamilia, aliuzika baba, mama, kaka zake wote, na alipobaki Yeye alistuka na akaja Kwa watumishi wa Mungu.

Alikatiwa connection hiyo, akabatizwa na kubadilishwa Jina. Ilipofika tarehe na mwezi husika hakufariki.



MANABII wa Kweli na UWONGO.

Mungu husema na Kila mtu, awe mwovu au mwema, tunatofaitiana tu jinsi ya kuelewa sauti hiyo sababu husema Kwa mafumbo ktk ndoto, maono au ktk Ulimwengu wa Roho.

Mtu anaweza kujisaidia Yeye mwenyewe bila kwenda Kwa manabii wa uongo kama tu atamkiri Yesu, ataacha dhambi na kuishi maisha ya usafi wa mwili na NAFSI.

Mungu hasemi na manabii pekee, anasema na watu wote, waislamu, wapagani nk nk Sema tu hawajui kusikia asemavyo.

Kama Kuna NABII wa Kweli, basi na Nabii wa UONGO yupo,

Kama Kuna mitume wa uongo, basi jua mitume wa Kweli wapo.

Hapa Tanzania Kwa mfano, Kuna madhabahu kubwa sana ya masonry inayowameza watumishi wa Mungu kuwatoa Kwa Mungu na kuwasajili huko.

Wanaanza vizuri, baada ya muda Fulani wanatekwa na kuingia huko.

Anayejiita Mzee wa.....na buldo... , Mwingiraaar,suguyuye,nk Walianza ktk Mungu bt nw ni manabii wa uongo.

Mwl Mwakasege,Mch Eliud misholi, Mch MBARIKIWA,Shehe Umar, Mchungaji Katunzi, Amiel Katekela ni baadhi ya Manabii wa KWELI wa Mungu.

So kama Bado ni mchanga kiimani Si vibaya kutafuta manabii wa Kweli wa Mungu ambao ni Wachache sana wenye kuihubiri Kweli ya Mungu.

Aamen
 

Vyombo vya habari visaidie kutoa taarifa ndugu/watu wa karibu wapatikane
 
Hii kitu unayoisema nimepata uzoefu nayo kwa sehemu. Miaka ya nyuma huko nilipata girlfriend mzuri, anaakili ya kimaisha na ya ziada. Ila hiyo ya ziada ni ya gizani. Pia nilikuja kugundua ni mtu mwenye muunganiko mkubwa sana na mapepo/majini. Sababu aliwahi kuniambia mwenyewe baadhi ya matukio ya ndoto na linalokuja kutukia physically. Tulikuwa tukivutana sana kama wote ni wanaume na Kuna wakati alikuwa na utisho. Alikuwa ni mwanamke anayetaka kuniinamisha kitu ambacho sijawahi kuota katika maisha ya mume na mke. Nikaachana naye maisha yakaendelea, lakini Kuna matukio kadhaa yalikuwa yakinitokea kwenye ndoto hata baada ya muda wa miaka zaidi ya mitano tuliyoachana! Tangu hapo naheshimu sana mambo ya uhusiano wa mwanamke na mwanaume na hata mwingiliano wa kawaida tu wa wanaume wenzangu kama marafiki. Bila shaka naeleweka vizuri na watu wenye upeo wa ziada.
 
Ndiyomaana huwa namwomba sana Mungu kuniepusha na majanga ya kuendekeza vimada kila kona ya nchi maana mengine ndiyo hayo mapepo yenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…