Kuna siri gani katika namba 9? Kwanini mtoto akae tumboni miezi 9?

Hata mi nashangaa kwanini septemba ndio 9 ,na nine pia 9
 
Unaondoka katika muktadha wa mimba kuwa ya miezi 9.

Unapokwenda ni kwenye kusema mtu ni special kwa sababu kaumbwa na Mungu atawale viumbe wengine.
Huko unanipeleka wewe kiongozi
 
Huko unanipeleka wewe kiongozi
Mkuu,

Sababu za kibaiolojia kwamba miezi 9 ndiyo muda mzuri wa mtoto wa mtu kuzaliwa na kuendelea na uhai, akizaliwa kabla anakuwa njiti, baada ya hapo uzazi utakuwa wa tabu, hazikutoshi?

Unatafuta namba za ki Freemason tulizoachiwa na aliens kutoka sayari ya Nibiru juu ya ma piramidi ya kale ya Misri kupitia wanajimu wa Kikaldayo kwa maelezo ya mtu alivyoumbwa na Anunaki kusaidia aliens kuchimba dhahabu duniani ili kumuabudu Enkidu?
 
Mkuu hebu tuzungumzie human existence na chanzo cha huyo mwanadamu. Chanzo chake ni kipi?

Wakati huo huo naomba unidadavulie kuhusu swala kwamba DNA ndizo hutumika ku pass information kutoka vhanzo fulani kwenda kingine?

Naweza kuwa sijayaweka sawa hayo maswali ila naomba twede hivyo hivyo
 
Kwanza kabisa, naomba tusitumie neno mwanadamu.

Neno mwanadamu lina mzizi (etymology) wa kutoka jina Adam. Kumaanisha kuwa watu wote wametokana na mtu wa kwanza aliyeumbwa na Mungu anayeitwa Adam aliyeishi katika bustani ya Eden.

Hizi ni hadithi za Wayahudi, huyo Adam hakuwapo, huyo Mungu hayupo.

Hivyo, jina la "mwanadamu" ni la mapokeo ya kimakosa, ni misnomer.

Mtu ni sahihi zaidi.
 
Tuendelee sasa.
 
Tuendelee vipi bila wewe kukubali kwanza?
Kukubali kwamba bin adam sio sahihi nimekubali natumia neno MTU. turudi sasa kwenye maswali niliyo kuuliza kuhusu human existence na origin yake
 
Nani kasema 9 huwa inaandikwa kwa kila namna na lugha hivo
 
Kukubali kwamba bin adam sio sahihi nimekubali natumia neno MTU. turudi sasa kwenye maswali niliyo kuuliza kuhusu human existence na origin yake
Human existence na origin yake ni suala pana sana, lenye migogoro mingi sana ambayo mingine hata wanasayansi hawajaimaliza.

Hivyo siwezi kukuahidi kwamba ni swali ambalo nitaweza kukupa jibu la kulimaliza.

Ila, ila.

Katika kutafuta jibu sahihi, kuna kitu kinaitwa "elimination method".

Ukishajua tu kuwa square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2, piga, ua, galagaza, then namba zote kuanzia 2 kwenda juu unaziondoa katika focus yako ya kutafuta square root ya 2.

Yani hata kama hujapata jibu kamili na sahihi, unaweza kuanza kuondoa majibu fulani na kusema hili si jibu kamili na sahihi, upande huu si upande wa kuangalia katika kutafuta jibu kamili na sahihi, tugeukie upande mwingine.

Na katika hiyo elimination method, mimi naweza kusema kuwa, chanzo cha maisha ya mtu si Mungu huyu mjuzi wa yote, muweza yote, mwenye upendo wote tunayemsoma katika misahafu.

Huyo Mungu naweza kusema kwa confidence kubwa sana kuwa hayupo. Hata kabla ya kujua chanzo cha maisha ni nini. Na sijawahi kusema najua chanzo cha maisha ni nini, nasema tu hakiwezi kuwa huyo Mungu kwa sababu huyo Mungu hayupo.

Mengine hata wanasayansi wakubwa duniani bado wanachunguza na wanabishana na mimi Kiranga wa JF leo kujinadi kuwa naweza kujua chanzo cha maisha ni nini, au kwamba naweza kukielezea vizuri bila kuzalisha migogoro na maswali zaidi ya majibu, nitakuwa nadanganya.
 
Ila unaamini/ jua jkwamba kuna chanzo?
 
Ila unaamini/ jua jkwamba kuna chanzo?
Dhana yenyewe ya chanzo inatokana na udogo wa mawazo yetu tu.

Yani nakusudia in the abstract, ile dhana ya chanzo, is not necessary.
 
Wanaojifungua Watoto na miezi Tisa ni wachache sana

Watoto wanazaliwa week ya 39/40-42 ambazo ni zaidi ya miezi tisa
 
Namba,miezi, na siku hazina maana yoyote bali mwanadamu ndio America maana na kuzi name.ni kama unavyo zaa mtoto na ukaamua umuite jina x ba siyo y just utambulisho but hakuna maana yoyote hivyo hivyo kwenye numbers.
 
Dhana yenyewe ya chanzo inatokana na udogo wa mawazo yetu tu.

Yani nakusudia in the abstract, ile dhana ya chanzo, is not necessary.
Kwa hiyo mkuu dhana ya chanzo cha mtu tunaweza kuifananisha na ukubwa/upana wa universe ambao bado wataalamu hawajajua ukubwa wake upoje na mwisho wake upoje? Na kama mwisho haujajulikana maana yake hata mwanzo wake inaweza kuwa ngumu pia kujua?
 
Nakwambia hivi, habari nzima ya mwanzo na mwisho ni mauzauza tu.

Kabla hatujafika huko mbali kwenye ulimwengu ambako kuna kiza kikubwa, tuanze na dunia yetu tu hii ambayo tunaielewa vizuri zaidi.

Unaujua mwanzo au mwisho wa dunia yetu hii, kieneo?
 
mwezi wa ramadhani huwa unafunga siku 30, baada ya hapo kuna kufunga siku 6 za hiari.

30 + 6 = 36. hizo ni wiki ambazo ambazo mtoto anakaa tumboni, kila wiki ina kazi yake.

natamani sana niendelee lakini hilo zogo litakalozuka humu ndani mpaka naogopa. ombeni sana mungu awafunulie.

sipendi kubishana katika mambo kama haya. mana utabishana na mtu hana moja wala kumi na moja.
Nakuomba pm kama hutojali mie Ni mtu nayependa mno kujifunza mno uumbaji na asili ya ulimwengu. Naomba unipe madini pm Mana hapa kila mtu anajua kila kitu ndio Tanzania Kama sio afrika ilivyo yaani mwanasiasa anamkoromea daktari hajui kila kitu hawezi jua Kama vipi akacheze na mpira pia apandishe uchumi na huku wanawaza kuiba tu
 
Nilivyokuwa mdogo, nilikuwa napenda sana kusoma vitabu vya science fiction.

Nilipenda sana kusoma vitabu vya H. G Wells, Arthur C. Clarke na vya Isaac Asimov, pamoja na waandishi wengine wengi.

Sasa, kuna kitabu kimoja cha Dr. Isaac Asimov, sikikumbuki jina, Dr. Asimov alikuwa anazungumzia uhusiano uliopo kati ya Biblia na mfumo wetu wa jua, solar system.

Nikasema Dr. Asimov nipe mambo nipe mambo, haya ndiyo mambo ninayotafuta.

Basi Dr. Asimov akawa ananipeleka katika ile safari, anasema solar system ina miezi mingapi sijui, namba ya hiyo miezi ni sawa na namba ya jina la Yehova lilivyotajwa kwenye kitabu gani, namba hii ya kwenye Biblia ni sawa na hii kwenye solar system, mpaka nikafika sehemu nikawa namuamini Dr. Asimov.

Mwisho kabisa, Dr. Asimov pulled the rug from under my feet.

Akasema hakuna relationship yoyote kati ya vitabu vya Biblia na solar system, hiyo relationship yote niliyoionesha nimeitunga tu kwa kuungaunga mambo.

Alisema nia yake ilikuwa ni kuonesha kuwa mtu yeyote mjanja ukimpa datasets mbili kubwa anaweza kuonesha kuna uhusiano ambao hata haupo.

Kuanzia siku hiyo nimekuwa muangalifu sana kwenye haya mambo ya numerology.
 
Back
Top Bottom