Kuna siri gani Rais kujaza wanasheria kwenye Baraza la Mawaziri?

Tuombe radhi watu wa kanda ya ziwa,, hakuna kitu tumemaind kama kumpiga chini Dada yetu kipenzi Angelina Mabula ardhi na kumuweka huyo dogo,, tumemaind sana na mtajua tu soon kwa nini hatukupendezwa na hilo jambo
Lakini SUMUMA GANG imerudishwa kiaina "ili kubalance" kura za mwakani.
Naibu Waziri Mkuu haijaja bahati mbaya, Mchngerwa hajapelekwa pale bahati mbaya, sasa hivi maendeleo yasubiri, safu y mwakani ndio inapangwa:
Wakuu wa wilaya soon nao unatoka mkeka[DREAM TEAM ].
SUKUMA GANG wameaminishwa NAIBU WAZIRI MKUU atakuja kugombea 2030 hivyo wataunga mkono mteuaji, ikipita ndio watajua hawajui.
 
Tanzania haijawahi kukosa wasomi, na watu wenye uwezo ki fikra na mikakati, Tanzania inakosa watu wema, wazalendo wa kuwahudumia wananchi.
 
Mchengelwa japo alishawahi kuwa katibu wa Jaji kiongizi lakini kichwani hamna kitu. Alishawahi kupewa mafaili Aandae hukumu akaandika Madudu tu. Bora alivyoingia siasani tu akafie huko
Doh kumbe watu mna mnavuta tu file za watu.Imebidi nimwangalie tena nikasoma na hii comment yako nikaishia kucheka.
 
HAKUNA JIPYA WANASHERIA WANAOINGIA MIKATABA YA HOVYO
 
Wananchi Kipenzi chao ni Magufuri na sio mtu mwingine yule.
 
HAKUNA JIPYA WANASHERIA WANAOINGIA MIKATABA YA HOVYO
Ni wale wa Serikali ambao wanaingia kazini saa mbili na nusu na kutoka saa tisa mchana.
Ni wale ambao wanakuja mahakamani kwenye kesi na kumwambia hakimu sijaja na faili.
ni wale wanakuja mahakamani na kumwambia hakimu sijasoma faili naomba siku 30 tena nipitie faili kesi iendelee.
ni wale wanaopinga dhamana ya mtu yeyote, wao wamefundishwa kupinga tu.
 
Badala ya kuandoka mawakili, ungeandika wanasheria watawala Baraza la Mawaziri sababu hujui kama wote wanaruhusiwa kufanya shughuli za uwakili. Uwakili ni mpaka usajiliwe na uwe unalipa retention fees
 
Badala ya kuandoka mawakili, ungeandika wanasheria watawala Baraza la Mawaziri sababu hujui kama wote wanaruhusiwa kufanya shughuli za uwakili. Uwakili ni mpaka usajiliwe na uwe unalipa retention fees
Ni mawakili, mimi nafahamu:
Wanasheria ni hao ambao hawana roll number.
siandiki nisicho kijua.
ingia google andika "MJUE WAKILI" then andika jina la yeyote hapo, ila usikosee hata spelling kama wazaaramo badala ya kusema "MREMA " wanasema "MLEMA"
 
Ni mawakili, mimi nafahamu:
Wanasheria ni hao ambao hawana roll number.
siandiki nisicho kijua.
ingia google andika "MJUE WAKILI" then andika jina la yeyote hapo, ila usikosee hata spelling kama wazaaramo badala ya kusema "MREMA " wanasema "MLEMA"
Asante mh. Jaji. Inaonekana ulifanya research kali sana ndio ukaja na andiko.
Hongera sana pia jana mawakili na wanasheria wenzako wamepata tena uteuzi. Nafikiri almost 99% ni nyie tu. Term yenu hii mkuu. Uongozi uliopita engineers walipeta sana. Labda awamu nyingine madaktari au walimu tutapeta
 
Asante sana.
MAJALIWA KASSIM anawakilisha walimu.
JPM aliwakilisha walimu.
NYERERE aliwakilisha walimu.
Tukubali tu , walimu ndio wametufikisha tulipo, tunatambua mchango wao.
 
Asante sana.
MAJALIWA KASSIM anawakilisha walimu.
JPM aliwakilisha walimu.
NYERERE aliwakilisha walimu.
Tukubali tu , walimu ndio wametufikisha tulipo, tunatambua mchango wao.
Lakini pale kada moja inapowakilisha more than 80% ya appointments zote inafikirisha sana
 
Lakini pale kada moja inapowakilisha more than 80% ya appointments zote inafikirisha sana
Labda ndio hao hao wana uwezo.
Mwalimu gani anapigania demokrasia nchini?
Mwalimu gani ama engineer yupo kuhoji mikataba DP WORLD?
Mwalimu gani anapambana kuhakikisha watu wnapata katiba na tume huru?
Hao wanasheria wanao pambana ndio hapo hao wanaonekana kwenye teuzi!
Ukiacha Maria Sarungi ambaye hana chama na si mwanasheria wengine wanao pambana ni mawakili/wanasheria.
 
Mkuu, umesema kweli tupu. Nilitaka kuzungumzia hili, ila nashukuru umenitangulia.
 
Uko sahihi kwa sehemu.

Labda nikuweke sawa sehemu moja. Wanasheria ambao bado sio Mawakili wanaweza kuajiriwa kwenye Law Firm na hawawi researchers tu, wanaenda mbali zaidi ya hapo. Wana-draft legal documents pia, ingawa wanakuwa chini ya usimamizi wa Wakili kamili.

Aidha, pia wanaruhusiwa kuwawakilisha wateja wao kwenye mashauri ya migogoro ya kazi inayoenda CMA (Commission for Mediation and Arbitration). Ukumbuke CMA ina hadhi ya Mahakama.

Kuna Wanasheria ambao sio Mawakili wako kwenye Law Firms ambao wana uzoefu na ujuzi wa ku-draft documents kuliko hata Mawakili kamili.

Huko kwengine uko sahihi.
 
Asante kwa ufafanuzi mzuri. Lakini teuzi zikiwa zinatolewa kwa jinsi watu wanaweza kusimama na kuzungumza current issues tu na siyo vigezo vingine vya kunyamaza nahisi kuna tatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…