Tunajua sote jinsi mchezo huu ulivyo muhimu kwa Simba na Taifa kwa ujumla, ndio wa kwanza katika historia ya Nchi yetu kutumia teknolojia ya usaidizi wa Video kwa Mwamuzi (VAR).
Zaidi ya hayo Sheria za CAF zinataka uwanja kuwa wazi angalau saa 72 kabla ya mchezo.
Pamoja na kwamba Wanasema saa 7 kamili hao washindani wa Quran watatolewa kwa usaidizi wa Polisi...
Lakini naona kabisa hapa kuna lawama zinaenda kutengenezwa sisi Waswahili tunajijua katika kutunza muda.
Lakini vipi kama mtu akaingia then akagoma kutoka ili aangalie mechi?
Lakini vipi kama hayo mashindano yakachelewa kwisha baada ya saa 7?
Ndio maana nauliza kuna ulazima haya mashindano kufanyika Lupaso?
N.B
Sina nia ya kukashifu Dini ya mtu.