Kuna ulazima hayo mashindano ya Quran yafanyike Mkapa Stadium? Siku ya mchezo Simba vs Orlando!?

Kuna ulazima hayo mashindano ya Quran yafanyike Mkapa Stadium? Siku ya mchezo Simba vs Orlando!?

Hayo mashindano ya quran yangepelekwa kufanyikia uwanja wa uhuru

Uwanja wa Uhuru ni Mdogo hauwezi kutosha kwa Watu wanaohudhuria.
Kumbuka kwa Mkapa wamelipia Watu wote waingie Bure ndiyomana umeona Serikali imemute hawawezi hamisha Mashindano ya Qur-an
 
Acha mashindano ya Quran yafanyike hapo, wakimamaliza muda wa maandalizi ya mechi ya Simba yatakuepo.atutaki timu yetu ya Simba iwe na mikwaruzano na dini yeyote ile.
Mkuu umeandika kwa uoga ssna unaogopa tumu yenu kupigwa al-badir
 
Ratiba yaashindano ya Qur-an yapo kwenye Kalenda ya kila Mwaka hivyo ndiyo ipo mwanzo! Hiyo ya mechi ya Simba imepangwa juzi tu baada ya Simba kushinda mechi na USGN na kufuzu hatua ya Makundi.
Sijaelewa hapa yalihamaje kutoka tarehe 10 hadi kwenda tarehe 17 April 2022..

 
Hayo mashindano yanakuwaga hapo miaka yote...Japo mimi siyafagilii mashindano yanayoendeshwa na huyu kishki...Labda ya huyu mama aisha sururu...

Kishki amekaa kisanii sanii sana...Na ndio maana Allaah kampa mtihani yamegongana na mechi...

Wakati wanapanga hayo mashindano...Caf walikuwa hawajapanga tarehe ya mechi ya simba ya robo fainali...Kwahiyo hapo kishki na uongozi wa uwanja hauna kosa...Caf ndio wameingilia ratiba ya uwanja...


Na kuna mpuuzi mmoja hapo juu...Eti waislam na wakristo wanazimiana kiki kama sijui monaizi na nani sijui...

Nikupe tu taarifa...Waislaam tunapopanga mambo yetu huwa hatuangalii wakristo wamepanga nini watasema nini...Hayatuhusu ya wakristo...Kuwa na akili ya kiutu uzima...
Aaah sheikh wangu mbona hata sio kitu cha kuficha??Kila pasaka/Xmas lazima waislam watatafuta tukio la kiki
 
Sijaelewa hapa yalihamaje kutoka tarehe 10 hadi kwenda tarehe 17 April 2022..


Hapo umeulizia Uzi wa Uknown person na sio chanzo rasmi cha Taarifa.

ZBC2 hawajawahi kukitangaza hicho kilichoandikwa kwenye huo uzi.

Taatisisi zote zinazotangaza haya mashindano hazijawahi kulizungumza hicho kilichoandikwa kwenye huo uzi.

Hivyo siwezi kujibia huo uzi.

Nitajibu utakaponiuliza kutoka chanzo Rasmi
 
Mashindano ya Qur-an ni bora zaidi ya huo upuuzi wa mpira wa simba na orlando,Uwanja ni wa taifa na unatumika kwa watanzania wote wawe waislamu au wakristo...mleta mada una chuki na uislamu na bado uislamu utazidi kupaa juu zaidi na mtabaki mnashangaa kama kule Times Square,Hoja za hovyo eti watu watatokaje uwanjani baada ya mashindano kuisha,hakuna muislam anayeweza kujaribu kujificha eti aangalie mpira bure..ilhali kaenda kwa dhati kabisa ya moyo wake kusikiliza maneno matukufu ya Mola wa ulimwengu huyo atakuwa kafiri na sio muislam..naamini baada ya shughuli kuisha watatoka wote ili kupisha wapenda mpira kuingia...uislamu ni dini ya haki hivyo hatuwezi kudhulumu haki ya mtu siku hiyo.
Ohooo,
Nilijua tu
 
Utakua hujui au kuna Kitu unafichwa:

Miongoni mwa mambo yanayofanywa viwanja vya Mpira ambayo sio mpira wa Miguu Dunia Nzima na si Tanzania tu.

1) Michezo ya Rugby
2) Sherehe za Kitaifa (Uhuru, Muungano n.k.)
3) Matamasha ya Muziki
4) Ngumi za kulipwa
5) Mashindano ya Riadha/Mbio
6) Kufanya maonesho ya Silaha za Kivita na Gwaride.
7) Mashindano mbali mbali yakiwemo hayo ya Qur-an.

SWALI KWAKO: Ni kweli hujawahi kuona popote uwanja wa Mpira kufanyiwa shuhuli yoyote isiyokuwa ya Kimpira au umeamua kuficha ukweli hata ukasema ule ni uwanja wa mpira na sio wa Dini?
Kuna sehemu kwenye bandiko langu nimesema hivyo?
Au wewe ndio unaamua kwa makusudi kupindisha?
 
Hakuna ulazima ila hayo mashindano yameanza mda mrefu hata kabla ya hizo mechi za kimataifa na hayo mashindano walishapewa kibali hata kabla simba haijulikani itacheza lini na Orlando pirates kwa hyo wanayo haki ya mashindano kufanyika taifa na uzuri hilo swala ni rahisi sana kukubalika na hata CAF wangeweza kukubali kufanyika,

tuheshimaiane jamani hizi dini tumezikuta tu hakuna aliyechagua kuwa muislamu au mkristo tumerithi tu kutoka kwa wazazi wetu hvyo tusijitoe ufahamu kiasi hicho.

Hence shown.
 
Kwanza mpira wa miguu ni haramu kwa Waislamu, vp watumie eneo lenye haramu.?
Ule sio uwanja wa mpira wa miguu tu, ule ni uwanja wa shughuli zote za kijamii, michezo na kisiasa pia ndio maana hata sherehe za uhuru zinafanyikia uwanjani
 
watu wa simba hakikishen jamaa wakiingia kwa ajili ya mashindano watumieni hao hao waombe dua kwa ajili ya mechi yenu
 
halafu lakini yanafanyika kwenye uwanja wa mpira! 😂
Usikariri, Ule sio uwanja wa mpira tu, pale kuna sehemu ya riadha pia lakini kuna sherehe za kumbukumbu za uhuru na muungano zinafanyikaga pale
 
Ule sio uwanja wa mpira wa miguu tu, ule ni uwanja wa shughuli zote za kijamii, michezo na kisiasa pia ndio maana hata sherehe za uhuru zinafanyikia uwanjani
Sherehe za uhuru wa nchi gani zishawahifanyikia hapo? Acha mihemko bro
 
Back
Top Bottom