Kuna umuhimu wa kuripoti JKT kwa wahitimu wa Form 6?

Kuna umuhimu wa kuripoti JKT kwa wahitimu wa Form 6?

Habari zenu Wana JF,

Naomba msaada kufahamu madhara ya kuacha kuripoti wito wa kujiunga na JKT kwa wale waliomaliza A level.

Je, cheti cha kumaliza mafunzo ya JKT huwa kinahitajika kwa ambaye anataka kufanya maombi vyuo vikuu vya Serikali kama UDSM, Tanzania Institute of Accountancy na IFM, kwa mfano?

Lakini la ziada: kama mhusika hatafanya maombi ya mkopo kupitia HESLB ataathirika namna gani?

Asanteni kwa msaada.
Kama unawish kuajiriwa siku moja na serikali ya Tanzania.. nenda kimbia fasta... Ila Kama unandoto tofauti jeshini haina haja
 
Usiongee kama mwakilishi wa jumuiya, sema wewe umeona hakija kusaidia usiseme watu
Hakina mchango wowote mambo ya kutesa watoto Bure tuu, jkt waende wa kujitolea wanaotaka na wenye uhakika wa kuajiriwa jeshini, vinginevyo ni porojoo tuu havisaidii lolote
 
JKT kupoteza muda tu na kutesa vijana wetu wameshachoka na mitihani hata hawajapumzika waend tena kulima huko na kukimbiakimbia, hao wa kujitolea tu hawawaajiri wanazeekea makambini na kurejea mitaani.
Binafsi sioni faida ya kwenda huko, labda kama una ndoto na jeshi unaweza kwenda ukapata connection otherwise piga chini, chuo utaenda tu.
Kwa kizazi hiki JKT muhimu,watoto wamelegea,uzalendo hawana
 
Kila niktaka kukuacha naona unajaa kwenye 18 [emoji23][emoji23][emoji23]

Njoo wewe na huyo cocastic, nawafumua mishono yote hiyo tena situmii mundende
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] umeshindwaaa kumkaza mama zuriii, ndo uniwezeee mie??
Hebu nipishee mie mxxxxieeeew
 
Watoto wa sasa hivi ni lonyolonyo sana, nashauri mbunge litunge sheria iwe ni lazima kwenda JKT.

Kiukweli mnatusikitisha sana Toto lipo high school bado linasimamiwa na wazazi hawezi hata kujisimamia.

Kizazi hiki bila kukipitisha jeshini tunaandaa msiba mkubwa kwa Taifa.
Hakika
 
Umechafua sana watu ukaona hujachoka, umeanza kuchafua na jeshi. Kuna kitu naamini unakitafuta. Basi subiri
Wee mjinga nn, sasa Kupita JKT kwa mujibu ni ajabu? Hivi wee uko timamuuu??

Ndo maana unachapiwaa, na kusoma kwako kotee ndo akili zimeishia hapoo.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] poleeeeeh
 
Nakubaliana na wewe kabisa mkuu, pia kama utaratibu huu ni kuwajengea vijana uwezo wa kizalendo pamoja na utambuzi wa skills mbalimbali za maisha basi nashauri usiwe na mazingira ya kiubaguzi kwani sio wote wanaomaliza huenda bali wengi wao huwa ni school candidates na sio PC. Unawezaje kuona SC anafaa kujiunga na JKT halafu PC asifae ilihali wote ni vijana wa kitanzania. Pili napata tabu kujua ni utaratibu upi ulitumika kutambua kuwa wanaostahili kwenda jkt kwa mujibu wa sheria ni hawa waliomaliza six pekee? Kwa nini kama lengo ni jema serikali isiweke utaratibu unaogusa kundi kubwa la vijana na iwe ni lazima labda mtu mwenye matatizo? Naomba nimalizie kwa kusema kwamba binafsi naliona kundi linalofaa kujiunga jkt kwa mujibu wa sheria ni hawa wanaomaliza kidato cha nne na iwe hivyo kwa wote kabisa kabisa.
Sababu ni kama zifuatazo:-

1/. Utagusa kundi kubwa sana la vijana.

2/. Kutokana na mazingira ya sasa, utakuwa umeokoa vijana wengi kwa kuwafanya wakakamavu na kuwaondolea hali ya urojourojo ikumbukwe kwamba siku hizi mfumo wa maisha umebadilika vijana wengi wamezoeshwa maisha mwendokasi kwa hiyo kusubiria wamalize kidato cha sita wanakuwa wameshakubuhu.

3/. Ni kundi ambalo lina muda mrefu wa kukaa jkt bila kuwaza mambo mengine kwani huwa kuna gap kubwa kutoka kumaliza shule, matokeo kutoka, selection na kujiunga na ngazi nyingine za elimu. Na hapa utakuwa umeokoa au umenusuru watoto wengi dhidi ya mambo kurupushi ya mtaani mfano kuolewa kabla ya kufikia malengo, na mengine yenye kufanana na hayo.

4/. Kundi hili kubwa mara baada ya kumaliza mafunzo hayo, nina imani vijana wetu hawatabaki kama walivyoingia na hatimae nchi itakuwa ina vijana wengi wanaojitambua.

NB. SERIKALI ISIOGOPE GHARAMA.
Nimeipenda hii!
 
Njoo na cheti chako cha JKT na mimi na hiki kitambi changu lakini ntakuponda vbya mno.

Hakuna faida yyte kwend JKT,Usimtishe dogo
Jumbe una kitambi?[emoji38][emoji38][emoji38] mkeo inaoneana unamuonea mno na yeye anakuendekeza sana... anatakiwa akupasue kabisa
 
Ndio maana mnaitwa wajinga na wapumbavu.
Hayo yote ulitakiwa fundishwa na waliokuzaa
Sehem niliyokulia kwa bahat mbaya hatukua na shamba, na muda wangu mwingi niliutumia katika masomo nyumban ilkua ni muda likizo tu.
 
Nawashangaa sana wanaosema jkt ni kupoteza muda, je mwanafunzi akibaki nyumbani ana kitu chochote muhimu cha kufanya?? Ni familia chache tu ambazo zinawapeleka hata short course za computer watoto wao katika huo muda, Na ni wanafunzi wachache wanaojishughulisha na uzalishaji mali katika muda huo.
Asilimia kubwa wengi huwa ni wazurulaji tu mtaani na familia ikijitahid sana itampa nauli akatembelee ndugu zake.
Je huko sio kupoteza muda napo kama hafanyi shughuli za msingi??
Tatizo mnaweka matarajio makubwa kua kwenda jkt kutakupatia ajira,hapana.
Kama mwanafunzi ana jambo la msingi analofanya nyumbani ni heri aende.
 
Back
Top Bottom