Nakubaliana na wewe kabisa mkuu, pia kama utaratibu huu ni kuwajengea vijana uwezo wa kizalendo pamoja na utambuzi wa skills mbalimbali za maisha basi nashauri usiwe na mazingira ya kiubaguzi kwani sio wote wanaomaliza huenda bali wengi wao huwa ni school candidates na sio PC. Unawezaje kuona SC anafaa kujiunga na JKT halafu PC asifae ilihali wote ni vijana wa kitanzania. Pili napata tabu kujua ni utaratibu upi ulitumika kutambua kuwa wanaostahili kwenda jkt kwa mujibu wa sheria ni hawa waliomaliza six pekee? Kwa nini kama lengo ni jema serikali isiweke utaratibu unaogusa kundi kubwa la vijana na iwe ni lazima labda mtu mwenye matatizo? Naomba nimalizie kwa kusema kwamba binafsi naliona kundi linalofaa kujiunga jkt kwa mujibu wa sheria ni hawa wanaomaliza kidato cha nne na iwe hivyo kwa wote kabisa kabisa.
Sababu ni kama zifuatazo:-
1/. Utagusa kundi kubwa sana la vijana.
2/. Kutokana na mazingira ya sasa, utakuwa umeokoa vijana wengi kwa kuwafanya wakakamavu na kuwaondolea hali ya urojourojo ikumbukwe kwamba siku hizi mfumo wa maisha umebadilika vijana wengi wamezoeshwa maisha mwendokasi kwa hiyo kusubiria wamalize kidato cha sita wanakuwa wameshakubuhu.
3/. Ni kundi ambalo lina muda mrefu wa kukaa jkt bila kuwaza mambo mengine kwani huwa kuna gap kubwa kutoka kumaliza shule, matokeo kutoka, selection na kujiunga na ngazi nyingine za elimu. Na hapa utakuwa umeokoa au umenusuru watoto wengi dhidi ya mambo kurupushi ya mtaani mfano kuolewa kabla ya kufikia malengo, na mengine yenye kufanana na hayo.
4/. Kundi hili kubwa mara baada ya kumaliza mafunzo hayo, nina imani vijana wetu hawatabaki kama walivyoingia na hatimae nchi itakuwa ina vijana wengi wanaojitambua.
NB. SERIKALI ISIOGOPE GHARAMA.