Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 48,055
- 116,512
At the same time uwe na kumbukumbu kuwa kipindi cha usajili wa mchezaji katika awamu ya pili ya tarehe 31 mwezi Januari ni siku 16 baada ya dirisha dogo kufungwa,Kwa kipengele (A na B) hilo linawezekana kama uongozi wa Simba ilikuwa na malengo kumtumia katika mashindano ya klabu bingwa ambavyo itamaliza hadi ishu ya kipengele D kwavile hivyo vyote inafanyika wakati wa kuingiza jina kwenye system (kabla hata ya mashindano kuanza)
Kwa kipengele C ili kujua kama haiwezekani au inawezekana tutoke kwenye nadharia twende kwenye reference ya Perfect Chikwende dhidi ya Kahata.
Katika hao wachezaji wawili, kuna mmoja hakuwa anashiriki michezo ya ligi kuu lakini michuano ya CAF alikuwa anacheza. Je iliwezekanaje?
Na ndio kipindi hicho hicho ambacho nadhani Simba waliondoa jina la Kramo ili kupata wachezaji wengine.
Kwa maana hiyo sio rahisi Kramo kuendelea kubaki kwenye system za usajili wa CAF kwa mgongo wa Simba kama mchezaji anayeweza kushiriki michuano.
Ishu ya Kahata na Chikwende kiukweli sina kumbukumbu nayo sahihi.
Ila kumbukumbu zangu nilizonazo ni kuwa Chikwende alikuja msimu wa dirisha dogo na lengo ilikuwa kuongeza nguvu kwenye michuano ya CAF na wakati huo tulikuwa na Kahata ambaye hakuwa na perfomance nzuri.
Simba ilikuwa haijafanya vizuri mahesabu yake wakati inamsajili Chikwende kwa expectations za kushiriki CAF Competitions
Chikwende alikuwa tayari kasajiliwa dirisha dogo na timu aliyotokea tayari alikuwa amesajiliwa kwenye mfumo wa CAF kama mchezaji wa hiyo timu na kufanya akose kigezo cha kushiriki CAF.
Kwa hiyo kama nimekuelewa vizuri ni kuwa swala la Chikwende kucheza ligi kuu ilitokana na zuio la CAF linalosma mchezaji hawezi kucheza timu mbili kwa msimu mmoja katika mashindano ya CAF.
Na Kahata kwa kumbukumbu zangu mbona amecheza mechi nyingi za ligi kuu?