Kuna viashiria vikubwa vya uvunjifu wa amani siku zijazo…

Unamaanisha sisi tuliopo Jf hatuishi huko mtaani,,ndugu acha kuingia mioyoni mwa watu,,wengi wanalalamikia mfumo unavoendeshwa sema tu hawana namna ya kufanya
Basi itakuwa wanawaogopo bakabaka
 
Punguza utoto kwenye hoja za msingi.
 
Nadhani sera 4R ikitwlezwa na serikali kwa ujumla itasaidia kuiondolea nchi maumivu asiachiqr Rais peke yake.
 
Hata wakati wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,hakuwachekea wavunjifu wa amani.Aliwaonyesha chamoto,hata wenzake aliodai nao uhuru,hakuwachekea,cha moto walikiona
Kwabahati mbaya hadithi za Nyerere kwa kizazi hiki hazina maana tena. Ni hivi, katika kitu usalama wa taifa walikosea ni kuacha chama kimoja kutawala muda mrefu hadi watu kupoteza ladha. Matokeo yake chama hicho kimegeuka pango la wezi, wakosa maadili, nk hadi chama hicho kuanza kukaa madarakani kwa njia za kishenzi kabisa. Mfano halisi ni uchaguzi wa 2020.

Hapa tulipofikia tumejikuta tuna serikali iliyopo kisheria, lakini isiyo na uhalali wa umma. Na inachofanya ni kutishia, kuua, kuhujumu kwenye sehemu za kujiingizia kipato kwa kila anayepingana na serikali hiyo haramu. Mifumo yote inaendeshwa kwa utashi wa kundi hilo la walioko madarakani bila ridhaa ya umma. Kwa sasa hakuna taasisi yoyote ya kimamlaka inafanya maamuzi kwa kufuata sheria, bali huangalia kwanza amri toka juu.

Kwahapa tulipofika, ni aidha machafuko, ama mapinduzi ya kijeshi ili tuanze upya kwenye mifumo ya utawala. katiba ya maridhiano itakuwa ni utapeli wa mchana kweupe.
 
Ningekuwa moderator ningeku BAN life kabisa hapa JF. Watu ka ninyi sijui kwa nini mlizaliwa. Muacheni Mama afanye kazi kwa ajili ya maendeleo ya watanzania. Bila CCM hakuna amani, ndiyo maana tunaendelea kushinda chaguzi zote.
Acha uchawa wewe mama

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Me mwenyewe nimechoka na ujinga wa viongozi wa CCM. Bora kibanda kiungue tuanze kukijenga upya
 
Yote haya yanakuja wakati rais ni wa kutoka Zanzibar na mwanamama wa kiislam!.

Mmesahau awamu ya tano namna watu walivyopotezwa na kuteswa mchana kweupe?.

Wengine walisulubiwa kwa kupigiliwa misumari miguuni kama Yesu alivyoteswa!.

Suala la DPW ni muendelezo wa sera za awamu ya tano zilizojenga SGR kwa jumla ya trilioni 17, tulitegemea pesa zote hizo mzigo wa kusafirishwa uwe ni mahindi na mihogo?.

Hata JPM alipofanya maamuzi magumu alisema anajua wapo watakaomchukia na wapo watakaofurahishwa na maamuzi yale. Na hiyo ndio sifa ya rais kuamini katika maamuzi unayofanya pasipo kujali kelele za kitanzania.

Mtanzania ni mlalamikaji siku zote, mtendee mema kumi na baya liwe moja tu, atajikita katika kujadili hilo baya moja bila ya kujali uwepo wa mema kumi!. Ni akili za kimaskini sana zinatusumbua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…