Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Rudia kusoma nilichoandika kisha rudi hapa uulize swali lako mkuu inaonekana umepitisha macho tu
Nimeomba kipande cha video cha Lissu akitamka kuwa Fr Kitima ndiye waliyekuwa naye siku tatu pale Msimbazi Centre!!

Mwenye nayo aiweke hapa,sijakwambia wewe, nimekunukuu tuu ili niweke ombi langu kwa mwenye na video hiyo.
 
Hakuna hicho kipande ndio maana na mimi nimeuliza kwanini walioripoti hii habari wanapotosha? Lissu kazungumzia biongozi watatu wa dini ila aliyetokea kikaoni ni mmoja na hakumtaja jina.
Ndio tusubiri yamkini Sisi Tu ndio hatujakiona hicho kipande
 
Moja ya kazi za Kanisa Katoliki kwenye jamii ni kutoa huduma ya Kichungaji ( Pastoral Care) kwa wafuasi wake.
Lissu na Mbowe, baada ya kutofautiana, walihitaji kupata common ground kwa ajili ya Upatanisho. Common ground hio ilihitaji mtu ambae pande zote mbili zinamuamini. Ndio sababu ya kanisa kuingia kati.
Msisahau pia, kazi nyingine ya kanisa ni kuchochea amani inayozingatia haki( To promote peace that does justice). Hio ndio sababu ya kuhusika kwa Fr.
Kama Mkatoliki na mwana CCM, ninalisifu kanisa kwa huduma hio.
 
Kwanini alifanya kwa siri na akitoka huko sirini anaikosoa Serikali Halali hadharani?
 
Kitenge ndiye amezusha habari za Dr. Kitima lakini Lissu hakumtaja Kitima.
 
Acha kujitia upofu makusudi. Hivi ingekuwa Lipumba na Maalim Seif wameenda kushiriki vikao vya siri Msikiti wa Umar AlFarouq BAKWATA Kinondoni I ungechukulia poa?
Kwani hao walikwenda kanisani? au wewe unafikiri huyo ndo kanisa
 
Acha kujitia upofu makusudi. Hivi ingekuwa Lipumba na Maalim Seif wameenda kushiriki vikao vya siri Msikiti wa Umar AlFarouq BAKWATA Kinondoni I ungechukulia poa?

..Viongozi wa Chadema ndio waliokwenda Msimbazi Center kusuluhishwa na viongozi wa Kanisa.

..Viongozi wa Dini mara nyingi wamekuwa wakitumiwa kupooza joto la kisiasa hapa nchini.

..Mfano mmojawapo ni jinsi viongozi wa Dini walivyoweza kuwashawishi Chadema wasitishe maandamano ya Ukuta wakati wa utawala wa Magufuli.
 
Acha kujitia upofu makusudi. Hivi ingekuwa Lipumba na Maalim Seif wameenda kushiriki vikao vya siri Msikiti wa Umar AlFarouq BAKWATA Kinondoni I ungechukulia poa?

..Serikali na Ccm hawampendi Fr.Kitima kwasababu ya ukosoaji wake.

..pia serikali haimpendi Shekhe Issa Ponda kwasababu ni mtetezi wa haki.

..viongozi wengi wa Kidini wanaogopa kutoa msaada na ushirikiano kwa Chadema kwasababu ya kuogopa kuandamwa na serikali.
 
Haya sio mambo binafsi! Ni mambo ya taasisi..Ndiyo maana wenyewe wamefanya Siri!

Haijakaa Sawa! Na kanisa limevuliwa nguo kwenye hili!

..viongozi wa Dini wanasuluhisha watu, na migogoro ya aina, mbalimbali.

..wanafamilia, wafanyabiashara, wanasiasa, wote wanaweza kutafuta usuluhishi kupitia viongozi wa Dini.

..Viongozi wa Chadema kusuluhishwa na viongozi wa Dini sio tatizo hata kidogo. Mwisho wa siku kinachotafutwa na maelewano, na masikilizano.

..Taasisi za Kidini kusuluhishi migogoro ya kisiasa, au ya wanasiasa, sio jambo geni duniani.

..Maadamu viongozi wa Dini hawajafunga milango yao kwa vyama vingine vya kisiasa sioni tatizo liko wapi.
 
Pengo alipowapatanisha Makonda na Gwajima haikuwa habari.

Acheni Nongwa.

Sasa hapo uko upande wa Mbowe au wa Lissu?
 
Hawa ndio watumishi wa kweli wa Mungu
 
Padre Kitima ni Kada wa Chadema na kwa sasa ni mpambe wa Lissu inajulikana siku nyingi sawa na Askofu wa sasa wa Dar kwa hiyo ni sawa tu ila waache kuwa wanatusemea waumini wote wa RC as if wote ni wafuasi wa Chadema.
 
Haya sio mambo binafsi! Ni mambo ya taasisi..Ndiyo maana wenyewe wamefanya Siri!

Haijakaa Sawa! Na kanisa limevuliwa nguo kwenye hili!
Imeandikwa katika Mathayo 5:9 'Heri wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu' . Kuwapatanisha watu wanaogombana ni kazi ya kitume kabisa hao viongozi wa kiroho walikuwa wanafuata mafundisho ya Yesu Kristo.
 
Padre Kitima ni Kada wa Chadema na kwa sasa ni mpambe wa Lissu inajulikana siku nyingi sawa na Askofu wa sasa wa Dar kwa hiyo ni sawa tu ila waache kuwa wanatusemea waumini wote wa RC as if wote ni wafuasi wa Chadema.
Chawa wa Mbowe mna hasira na kila anayekuwa upande wa Lissu
 
Wamachame wacheni chuki hizo Chadema ni chama cha kitaifa siyo mali ya Mbowe na Wamachame
 
Chawa wa Mbowe mna hasira na kila anayekuwa upande wa Lissu
Nyumbu katika ubora wake. Mimi niwe Chawa wa DJ Mbowe?? Wala siwezi kuwa mfuasi wa hiyo Saccos nyinyi endeleeni kuparurana tu huko itapendeza zaidi mking'oana meno kabisa. Watz hawawezi kuwapa nchi hii muongoze!
 
Najua wewe ni mccm na katika huu mtanange mko upande wa Sultan Mbowe lakini ndiyo hivyo Lissu ataibuka mshindi tena kwa margin kubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…