Pre GE2025 Kuna vita ya chinichini inaendelea dhidi ya viongozi wa dini wanaokosoa Serikali
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Acha kujitia upofu makusudi. Hivi ingekuwa Lipumba na Maalim Seif wameenda kushiriki vikao vya siri Msikiti wa Umar AlFarouq BAKWATA Kinondoni I ungechukulia poa?
Nyie jamaa ni wote huwa mnakuwa hamna akili? Kazi ya viongozi wa Dini na wasio wenye busara ni kupatanisha. Ningefurahi sana kama Maalim na Lipumba wangepatanishwa. Iwe na Sheikh au asiye. Ana Kheri anayepatanisha. Na Upatanisho huwa so wa Public. Watu wanakalishwa kila mmoja anaongea machungu yake.
 
Padri alimuomba Mbowe amuachie Lissu. Lissu akipewa tiketi ataingia ikulu asubuhi na mapema.
 
Nyie jamaa ni wote huwa mnakuwa hamna akili? Kazi ya viongozi wa Dini na wasio wenye busara ni kupatanisha. Ningefurahi sana kama Maalim na Lipumba wangepatanishwa. Iwe na Sheikh au asiye. Ana Kheri anayepatanisha. Na Upatanisho huwa so wa Public. Watu wanakalishwa kila mmoja anaongea machungu yake.
Kama nyie tu mnaobadu sanamu!

Tunaijua NCHI hii kuwezi kutudanganya kitu! Udini ukihusu Uislam ila ukihusu ukafiri ni upatinishi!

Shenzy typ!
 
Kama nyie tu mnaobadu sanamu!

Tunaijua NCHI hii kuwezi kutudanganya kitu! Udini ukihusu Uislam ila ukihusu ukafiri ni upatinishi!

Shenzy typ!
Mnaabudu sanamu? Kwa nini? Ukiwa na akili unagundua kuwa upatanishi ni jambo jema. Wewe hupendi? Unataka wakatane mapanga? 😁
 
Ingawa video haioneshi kama Lissu kamtaja Kitima but let's assume ni yeye; hao wengine sijui kwanini Maulid Kitenge na Efm hawakua na interest ya kuwajua, kama ni Kitima, then anatembelea maagizo ya Bwana wake Yesu aliyesema, "Heri wapatanishi maana wataitwa WANA wa Mungu" Hongera sana Fr. Kitima or yeyote aliyehusika kuwakutanisha hawa watu 2.
 
Kwanini wanapotosha, kwanini hakuna anayeweka uthibitisho wa video habari hii ya madai kuwa Tundu Lissu amethibitisha Padre Dkt. Charles Kitima kushiriki vikao vya siri vya CHADEMA?

Katika video ya mahojiano na Waandishi wa Habari pale Uwanja wa Ndege hakuna mahali Lissu amemtaja Kitima lakini namna imeripotiwa ni kama viongozi wa dini hawapaswi kufanya upatanishi.

Hata hivyo ukifuatilia wote waliotoa habari hii maelezo yao ni copy and paste mwanzo mwisho kuonesha script waliyopewa ni moja.

Halafu kama kikao walichoshiriki ni kikao cha upatanisho kuna ubaya gani wao kushiriki? Maana yeyote waliyemuona na busara za kuwapatanisha ndiye aliyealikwa kwanini wahusishe na kuiponda serikali?

Lakini pia kama wanakemea uovu unaofanywa na viongozi serikalini kuna tatizo gani? Kwani kazi ya vyombo vya dini ni kusifia tu viongozi na serikali na siyo kukosoa pale wanapoona mambo hayaendi vizuri?

Hiki ndicho Lissu alizungumza

View attachment 3196312

==

View attachment 3195838
Katika tukio lililotokea jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, amethibitisha hadharani kuwa Fr. Charles Kitima, Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), alihudhuria vikao vya siri vya chama hicho vilivyofanyika katika ukumbi mdogo wa Macapuchino ulioko eneo la kanisa, Msimbazi Centre, jijini Dar es Salaam.

Mwanzoni mwa mwezi Desemba, taarifa za ndani zilisambaa zikidai kuwa Fr. Kitima, Kiongozi wa juu wa Kanisa Katoliki, alihusishwa moja kwa moja na vikao vya CHADEMA.

Taarifa hizo zilizua mijadala mitandaoni, huku baadhi ya wadau wakitilia shaka ukweli wake na wengine wakihoji nafasi ya kiongozi huyo wa kidini katika siasa za vyama.

Hata hivyo, jana Lissu amekiri waziwazi ushiriki huo, akiondoa shaka kuhusu madai hayo ambayo awali yalionekana kama uzushi.

Ukaribu wake na Fr. Kitima unatokana na ukweli kwamba wote wanatoka kijiji kimoja mkoani Singida. Ukaribu huu, kulingana na vyanzo vya karibu, umesababisha Fr. Kitima kuwa mmoja wa wapangaji wakuu wa mikakati ya kampeni za Lissu na hatua za kuipinga serikali.

Uthibitisho huu umetajwa kama "kuvuliwa nguo kwa kanisa," huku baadhi ya wadau wakidai kuwa hatua ya Lissu kufichua ushiriki wa Katibu wa TEC katika siasa za vyama imeweka wazi mgongano wa maadili unaohusiana na nafasi ya viongozi wa dini katika masuala ya kisiasa.

Kanisa Katoliki linatakiwa kutoa tamko rasmi kufuatia kauli ya Lissu, ingawa mjadala mkubwa umeibuka mitandaoni, huku waumini na wadau wa siasa wanakosoa hatua hiyo kama kinyume na maadili ya kidini.

Tukio hili linaongeza mvutano kuhusu nafasi ya viongozi wa dini katika siasa za Tanzania.View attachment 3195839
Maaskofu watatu na Mufti walimuona FAM kabla ya kuachiliwa na kufutiwa mashtaka ya uhaini
 
Cha muhimu ni hoja zenye kujenga mustakabali mwema wa taifa zaidi ya dini, kutoka kijiji ki moja, katika, kanda, chama,.....
Hoja za kujenga taifa, zenye mashiko hatutakiwi kuhoji zinatoka kwa nani.
 
Acha kujitia upofu makusudi. Hivi ingekuwa Lipumba na Maalim Seif wameenda kushiriki vikao vya siri Msikiti wa Umar AlFarouq BAKWATA Kinondoni I ungechukulia poa?
Wazoee watanzania na hasa chamudomozzzz

They twist and turn like hell

Fr. Kitima is too biased
 
Lakini pia kama wanakemea uovu unaofanywa na viongozi serikalini kuna tatizo gani? Kwani kazi ya vyombo vya dini ni kusifia tu viongozi na serikali na siyo kukosoa pale wanapoona mambo hayaendi vizuri?
Na kuna uzi humu jana unasema Waziri amesikika akimtaka mwanae alitekwa arejeshwe
 
Back
Top Bottom