Kuna wageni ambao hawana ustaarabu mezani saa ya chakula

Mie ndo maan siwezi kula kwa watu, yaan ni kuwekewa masharti na kuchorwa tyuuuh aaaaah
 
Mimi mara zote huwa ninakuwa na wasiwasi sana na watu ambao akli yao iko concentrated sana kwenye mambo ya chakula mezani. Ni kwa sababu utafiti wangu wa kina ulishanithibitisha pasipo shaka kabisa kuwa kawaida watu hawa huwa wana shida kubwa sana mahali fulani kichwani
 
Tatizo lenu mnapika chakula kidogo mboga kidogo akitokea tu mgeni roho mkononi sijui atachukua kiuno cha samaki? Uchoyo tu usukumani mbona haya hayapo mnakwama wapi bandugu?
 
Noted. Ila mimi sipendi kabisa kula kwa watu. Na ikitokea basi huwa napakuwa chakula kiwango kidogo kadiri nitakavyoweza. Ni bora nisishibe ugenini, nitaenda kujazia mbele ya safari (nyumbani).
Ukiwa unaenda kwa watu, fabya backup hata ya kiepe au fruits, ukifika unapakua kiasi.
 
wapakulie kabisa
 
dah'table manner inamatter sana'watu wengi nilokutana nao sehemu mbalimbali kiukwel hili suala ni changamoto especially wanaume yaani wanavitabia vinakera sana wakati wa chakula
 
Ustaarabu ni Relative Term, ukute mwenzio alichokifanya ndio ustaarabu wake!
 
Kwenye kila family kuna yule mwamba
Huwa anaambiwa .

Pakua chakula kidogo wenzio hawajala
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kabla sijapakua mboga uwa nascan bakuli kwanza kwenda chini kupata idadi kamili ya yaliyomo kama yamo

Nacross multiplication vs number of remaining candidates
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]

Apo nikipanda juu na kijiko shughuli imeisha


Remember this is a very quick assessment [emoji23]
 
mimi ni mtumia smart phone wakati nakula ila nafanya hivo kama wenyeji ni wa umri wangu vijana wenzangu na tuwe wachache
 
Mama alikuwa anasema ukialikwa mahali popote hata iwe harusi hakikisha unakula nyumbani kwako kwanza.

Usiende kwa watu na njaa yako ukiambiwa pakua unajaza sahani kama ndo pa kupakulia.

Au unafika ukumbini we unatoa mimacho kungojea muda wa kupakua.
 
Hapo kwenye smartphone inamaana mtu asijibu ujumbe wa mtu aliotumiwa

Ufipa group mna nongwa😀😀😀
 
Samaki sio mboga ni kitoweo.
Jifunzeni Kiswahili hasa kwa awamu ya tano
 
Hatufundishwi ustaarabu wa kula, na suluhisho acha kwenda kwenye nyumba za watu, nenda kwa hotel kula unachotaka, au nunua nyumbani kwako. mambo ya kuingia ingia kwenye nyumba za watu acheni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…