Kuna wageni ambao hawana ustaarabu mezani saa ya chakula

Kwahio mlikuwa mnapika kuku wangapi maanake mapaja yako mawili tu. Kula mapaja mawili au manne ni kujaza choo tu kiwango kinachohitajika ni kidogo sana. Ni Sawa na mtu anaekula ugali mwingiiii anajaza Choo tu.
 
Kama vipi vi-shombo shombo vyovyote uwe una wawekea mwenyewe
 
Mwingine anaweza kujifanya mstaarabu anakula kwa adabu kumbe kwenye pochi kajibebea magimbi yake na viazi vitamu vya kuchemsha.... Mmelala ye anajigongea vitu vyake adoado.. Hiyo inaitwa usinichoshe nisikuchoshe
[emoji23][emoji23]
 
Nimepitia comments zote nimeona jinsi nilivyosumangwa 😔

Mungu atawalipa tu
 
Mimi utaratibu wangu nikienda kutembea kwa watu.mda wa kula unakuta kabla ya hapo nilipita sehem nikajipigia kitimoto na balimi mbili murua kabsa,kwa hyo wakileta chakula napakua punje 6 tu za wali,samaki ntaweka mifupa,nawambia mi sio mlaji sana.(kinachonicost tu nna tabia ya kuchomeka toothpick kichwan af nasahau kwa hyo wakiona vile wanajua uyu mwamba Kuna sehem kagonga heavyfood.


Kuna dogo alisanua et aliniona wanapouza kitimoto ilihali m mgeni kwenye huo mji.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kwani mkubwa hakatiwi hilo yai?, hapo wewe ndio unakuwa mpakuaji na unauliza hiki vipi kinatosha? Mboga nampakulia na yai nakata vipande husika, kuna wageni unaangalia wanaweza kulaza wengine na njaa
Point, Mambo ya kulazana na njaa hapana.
 
Ukitaka kumfahamu mtu kastaarabika vipi basi mwangalie wakati wa kula jinsi anavyobehave. Meza ya Chakula ni mojawapo ya kipimo kizuri sana cha tabia ya mtu.
 
Ni wapi huko nasie tuhamie maisha ya mjini hayataki masihara Ndugu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Unamchana LIVE tu sasa mbona umechukua vipande vya samaki vitatu wakati kuna wengine HAWAJAPAKUA? 😳
 
Tabia nisiyoipenda kwenye kula ni wale wanaotafuna kwa kutoa sauti na wale wanaokula huku wanajilambalamba vidole na mikono.
 
Kweli mkuu mi pia nilikua na tabia hio lkn sku moja niliadhirika kwasababu nilipakua chakula kingi Sana mpk wengine wakakosa ikabidi dada wa kazi akaange chips za fasta ili wale
Lkn mungu hataki dhambi kile chakula nimekula nusu tu kikaanza kunishinda
Kwakweli ilikua aibu kubwa Sana
Tangu siku hio nimejifunza
 
Kuna wale wanaotafuna chakula utadhani mtu anatembea kwenye matope, arggg wananikera kinyama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…