Kuna watu wanaweza kukaa peke yao siku nzima bila kuchoka, wanapenda wageni ila mgeni ukikaa zaidi ya saa unawaboa

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
Mtu yupo ndani kwake siku nzima, kama hujamzoea unaweza kuhisi kuna shida ila ukiishi hapo kwa muda mrefu unamgundua wala hana shida, haonyeshi dalili za masikitiko, ndo furaha yake,

Anapenda company lakini iwe ya muda mfupi tu, ukienda kumtembelea kaa nusu saa tembea, ukizidisha unamuona jinsi anavyoanza kuboreka,
 
Tupo wengi tu nikitoka ni jioni baada ya kula ugali mrefu naenda kutafuta nyagi ya kumeng'enya msosi, baada ya hapo kidogo kampani na story ztapanda nikitoka hapo kama sina demu wa kupumzikia ni ghetto kuangalia katuni huku nacheka peke yangu
 
Hiyo ni nature ya binadamu hasa mwanaume. Usione ni tofauti, ukiona unapenda kukaa na mtu masaa 10 ujue una shida ya akili. Utakuwaje productive? Wenzetu wana mambo mengi na pia asili yao inabidi kuwa watu wa kukaa na mtu muda mrefu.

Can you imagine kukaa na watoto siku nzima? Yani mwanaume ushinde na watoto siku nzima utaweza?
Hii mambo ni nature... Ukitaka kujua hilo angalia watoto wakizaliwa mpaka wanakua.

Ukijua parten ya jinsia hutajiangaisha kukaa na watu masaa 6.

Anyway nipo hapa saa la 8 nimekaa mwenyewe nakula music and I am very okay..

Kuna muda hata kupigiwa simu naona kero.
 
Huwa sipendi mtu anae ongea ongea sana hamalizi maneno mimi ni mvivu wa kumsikiliza mtu anae ongea kwa muda mrefu huwa nachoka labda kwa sababu mimi mwenyewe sipendi kuongea ongea sana bila kuwa na sababu ya msingi ya kuongea.
 
Sipendi pia mazoea ya mtu kunifuatilia na kunitembelea tembelea katika maisha yangu binafsi kama kufahamu mahali makazi yangu yalipo kwa sababu watu wengi ni wajinga hasa Watanzania hawawezi kuheshimu uhuru binafsi wa mtu na kutunza faragha zake ndio maana naona heri maisha yangu kubaki peke yangu pia sina mazoea ya maisha ya watu wengine.

Kwa ufupi mimi ni mimi na maisha yangu tu mtu asiniletee mazoea kupitiliza yeye,wao wabaki na maisha yao kwa sababu kwangu hayana umuhimu kujua yao.
 
Watanzania wengi wanapenda sana kubwabwaja, kupiga domo na kuongea ongea pumba!!!

Ukiwa mtu wa hivyo una enjoy sana na yatakuepuka mengi sana.....ingawaje utaonekana unaringa au unajisikia lakini ni kheri ya hivyo!!!!
 
Sipendi pia mazoea ya mtu kunifuatilia na kunitembelea tembelea katika maisha yangu binafsi kama kufahamu mahali makazi yangu yalipo kwa sababu watu wengi ni wajinga hasa Watanzania hawawezi kuheshimu uhuru binafsi wa mtu na kutunza faragha zake ndio maana naona heri maisha yangu kubaki peke yangu pia sina mazoea ya maisha ya watu wengine.

Kwa ufupi mimi ni mimi na maisha yangu tu mtu asiniletee mazoea kupitiliza yeye,wao wabaki na maisha yao kwa sababu kwangu hayana umuhimu kujua yao.
Just like me . Huwa sipendi kuingilia faragha za watu the same na mimi Sitaki kuingiliwa... Kuna watu wanakosa adabu kama mbwa Koko . Kutaka kujua hadi wapi unapoweka kichwa unapolala.... Noma sana
 
Maisha yangu ya weekend hayo nipo ndani kama Sina pakwenda nitashinda ndan na usijue kama nipo au laah maana hata kupiga miziki sipend kelele kabisa mie mvivu wa kuongea nikishika simu yangu inanipa amani zote
 
Hiyo ni nature ya binadamu hasa mwanaume. Usione ni tofauti, ukiona unapenda kukaa na mtu masaa 10 ujue una shida ya akili. Utakuwaje productive? Wenzetu wana mambo mengi na pia asili yao inabidi kuwa watu wa kukaa na mtu muda mrefu.

Can you imagine kukaa na watoto siku nzima? Yani mwanaume ushinde na watoto siku nzima utaweza?
Hii mambo ni nature... Ukitaka kujua hilo angalia watoto wakizaliwa mpaka wanakua.

Ukijua parten ya jinsia hutajiangaisha kukaa na watu masaa 6.

Anyway nipo hapa saa la 8 nimekaa mwenyewe nakula music and I am very okay..

Kuna muda hata kupigiwa simu naona kero.
True
 
Back
Top Bottom