Kuna watu wanaweza kukaa peke yao siku nzima bila kuchoka, wanapenda wageni ila mgeni ukikaa zaidi ya saa unawaboa

Kuna watu wanaweza kukaa peke yao siku nzima bila kuchoka, wanapenda wageni ila mgeni ukikaa zaidi ya saa unawaboa

Sio kwamba mtu hapendi watu, ila anakuwa anajisikia huru na salama wasipokuwepo.
Mmoja wapo mimi hapa. Njoo home, tuongee ishu ya msingi, upate juice au kahawa, au msosi kama utakuwa ni muda wake, ondoka zako. Hivyo yaani.
Naondokaje yani?😁
 
Mimi ni mmoja kati ya hao wanaopenda kuwa peke yangu...
 
Sawa Babu
Na ndio kama hivyo tunayaepuka majungu tunaona bora tukayapike huku JF tusipojuana anyway karibu Pasaka 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
Nikaribie pasaka ili unitie majaribuni mjukuu, mwili ni dhaifu😅
 
Kipindi nipo single boy, siku kama jumamosi na jumapili mlango wa nje nilikuwa nafungua jioni ninavyotoka. Kwanza ijumaa nikila mitungi narudi na vitu vya kula siku nzima najua jumamos ni kula ngoma, movies na games.
Akija demu napenda nipige usiku, asubuhi atembee. Kwanza mi maswala unakaa na mtu kila muda anakuuliza maswali sipendi
 
Nnakoishi kila mtu na hamsini zake. Saa kumi na mbili kila mtu yupo tayar kaondoka zake home anabaki dada wa kazi tukirud jion nna nyagi langu nasaviwa na wife nae anaonja dada wa kazi anapga kidogo watoto na vijuice vyao yaan ni kimya ni kama hamna watu mpaka ilifka mwenyekiti kaja kugonga geti eti majirani wanadai ni kama hamna watu. Yaani niliwapa msomo ambao mpaka leo wakiniona wanakula kona. Mwenyekiti nilimwambia awe kila cku anakuja kwangu na daftar la kusain na nikishasaini apige kelele kuwa watu wapo. La sivo ntakuja kupga mtu la matakoni. Na mgeni kwangu kama hujafanya mawasiliano na mimi au wife utakesha getin hadi turud. Yaan nyumba yangu kwa kweli utadhan hakuish watu kila mtu ana allergy na kelele
 
Mtu yupo ndani kwake siku nzima, kama hujamzoea unaweza kuhisi kuna shida ila ukiishi hapo kwa muda mrefu unamgundua wala hana shida, haonyeshi dalili za masikitiko, ndo furaha yake,

Anapenda company lakini iwe ya muda mfupi tu, ukienda kumtembelea kaa nusu saa tembea, ukizidisha unamuona jinsi anavyoanza kuboreka,
Changamoto ya afya ya akili inahusika hapo.
Mtu wa aina hiyo asipopata tiba mapema anaweza kuwa mzigo kwa jamii.
 
Back
Top Bottom