Kuna watu wanaweza kukaa peke yao siku nzima bila kuchoka, wanapenda wageni ila mgeni ukikaa zaidi ya saa unawaboa

Kuna watu wanaweza kukaa peke yao siku nzima bila kuchoka, wanapenda wageni ila mgeni ukikaa zaidi ya saa unawaboa

Kila mtu na alivyoumbwa na mazoea pia mimi napenda kukaa mwenyewe
Ila watu wakiwepo pia sio tatizo
 
Comment ya kwanza inakupa mwelekeo wa sred nzima, aki-comment negative, basi tegemea negative comments kwa asilimia kubwa ya wadau.
Noma sana!!
Babu kwanini hamuamini kama watu watupendi kupuyanga kama hatuna issue za kufanya😂😂
Mie kheri nishinde JF kupitia kila uzi ila sio kufunga safari kwenda kwa jirani 😂
Muhimu bundle or WiFi
 
Babu kwanini hamuamini kama watu watupendi kupuyanga kama hatuna issue za kufanya😂😂
Mie kheri nishinde JF kupitia kila uzi ila sio kufunga safari kwenda kwa jirani 😂
Muhimu bundle or WiFi
Labda nyie members wa jf ndio hampendi,😅😅 ila watanzania wengi ni wongeaji sana, story njingi, uongo mwingi, hata huko mbelez wanakimbiana kwa kunafikiana na kuchomeana.
 
Jf kila mtu atajifanya yupo hivyo😅😅 oeni na oleweni kitanda sio kaburi mpaka ushinde mwenyewe na upweke na sio sifa, ni dalili za ukichaa huo😅
Siku hizi kila kitu kinasingiziwa ni matatizo ya akili kumbe vingine ni kawaida tu, duniani tuko watu zaidi ya bilioni nane hivyo hatuwezi wote kuwa na sifa zinazofanana, kila sifa ina kinyume chake na si lazima moja iwe nzuri na nyingine iwe mbaya kila mtu aishi anavyotaka
 
Siku hizi kila kitu kinasingiziwa ni matatizo ya akili kumbe vingine ni kawaida tu, duniani tuko watu zaidi ya bilioni nane hivyo wote hatuwezi kuwa na sifa zinazofanana, kila sifa ina kinyume chake na si lazima moja iwe nzuri na nyingine iwe mbaya kila mtu aishi anavyotaka
Yeah nakubaliana na wewe, hata mimi ni mkinya ila nimeona niwe tofauti tu🤣🤣
 
Comment ya kwanza inakupa mwelekeo wa sred nzima, aki-comment negative, basi tegemea negative comments kwa asilimia kubwa ya wadau.
Noma sana!!
Unataka kusemaje bwashee😃
 
Sio kwamba mtu hapendi watu, ila anakuwa anajisikia huru na salama wasipokuwepo.
Mmoja wapo mimi hapa. Njoo home, tuongee ishu ya msingi, upate juice au kahawa, au msosi kama utakuwa ni muda wake, ondoka zako. Hivyo yaani.
 
Labda nyie members wa jf ndio hampendi,😅😅 ila watanzania wengi ni wongeaji sana, story njingi, uongo mwingi, hata huko mbelez wanakimbiana kwa kunafikiana na kuchomeana.
Sawa Babu
Na ndio kama hivyo tunayaepuka majungu tunaona bora tukayapike huku JF tusipojuana anyway karibu Pasaka 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Back
Top Bottom