Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nilishasahau kuwa kuna watu mna hati miliki. Watu wengine hawaruhusiwi kuchangia kufundisha wala kutoa maoni.
Jamani wale wenzangu tusaidiane kueleweshana. waioona tamko lenye definition ya mtumishi au kiongozi wa umma naomba msaada.
hapa ni lazima tutambue kuwa watanzania wote tuna wajibu wa kuhakikisha mifumo ya kitaifa kwanza inakuwepo iliyokaa vizuri na hapo ndio tuangalie kama ni makundi je ni jambo gani ambalo lina umuhimu wa kuingia.
unaweza kuwa msanii, unaweza kuwa mlemavu, unaweza kuwa mwananmke, unaweza kuwa mzee au mwanaume tunategemea serikali kuhakikisha kuwa kila haki iliyotajwa inapatikana, ni wajibu wa bunge kusimamia hilo na kazi ya mahakama kutoa maamuzi kama kuna yeyote anadhani haki yake imekiukwa.
kama hatujaweka mfumo wa serikali uliothabiti je unadhani haki yako hiyo iliyotajwa utaipataje?
kama hatutengenezi bunge kulipa utaalamu na mifumo na nguvu ya kusimamia je unadhani nani atahakikisha unapata haki yako?
kama hatujaweka mfumo ulio huru wa mahakama je unadhani nani atatoa maamuzi ya haki kwako wewe kama haki yako itakiukwa? kumbuka hapa haki yako inapokiukwa katika jambo lolote je ni kina unaweza kuwapeleka katika mahakama na wote unaoweza kuwapeleka mahakamani unaweza kupata maamuzi yaliyo huru na je maamuzi hayo yanaweza kutekelezwa?
haswa fikiria kama unaipeleka serikali mahakamani na hapa sio katika maswala ya kudai malipo maana wengi tumekuwa tukifanya dili chafu huko na malipo tunapata lakini tuzungumzie mfano kiongozi anakuja katika eneo husika anawazuia wakulima kuuza mazao yao kwa soko lililopo na wakulima hawa wanapata hasara je wanaweza kwenda mahakamani wakulima hawa kama wameshawishika kuwa amri ya kiongozi wa serikali imekiuka katiba kwa kumyanyasa mkulima, kumuharibia soko ili wasiolima wapate mazao kwa bei nafuu au kukosa wanunuzi kabisa.
je kiongozi anaweza kutoa maamuzi akapelekwa mahakamani na mahakama zikawa huru kufanya maamuzi.
zipo haki tunazikosa sio kwa sababu hazijatajwa bali kutokana na udhaifu ulioko katika mifumo yetu ya utawala. na hapa wengi wamekuwa wakisema tatizo letu ni utekelezaji, je ni jambo gani linalosababisha tushindwe kutekeleza yale tuliyokubaliana? je unadhani kuna jambo linaweza kufanyika katika mifumo yetu ili mambo yaende vizuri?
hilo ndilo lengo la katiba mpya, kurekebisha pale tulipobaini mapungufu kwa kuweka mifumo yetu ikae sawa na utekelezaji uwezekane.
bado tunayo nafasi ya kurekebishaserikali kila kitu cha msingi ni kuangalia yaliyopendekezwa na kama huoni mapungufu au unaona mapungufu ufanye maamuzi katika kura.
kama kuna mapungufu yanayohitaji kurekebishwa basi piga kura ya hapana wakati ukiwadia ili kutoa nafasi ya marekebisho.
kama unaona kila kitu kimekaa sawa na umeridhika ndio upige kura ya ndio kwa maana kila kitu kimekaa sawa

Naona umejaribu kugusia sana suala utoaji wa haki. Kiukweli umezungumza jambo zuri sana kwamba tusichekelee suala la kuwa umetajwa ktk katiba pendekezwa naona sio kigezo cha kufurahia sana ila tuangalie imeweka misingi ipi kuhakikisha unapata haki yako bila kikwazo.
Tumeona imezungzia suala la usawa katika uongozi kati ya wanaume na wanawake. Kwa rasimu ya Warioba iliweka bayana kabisa juu ya usawa mfano katika nafasi za ubunge ilitanabaisha wazi kabisa kuwa lazima kuwe na mbunge mwanaume na mwanamke kwa kila jimbo kitu ambacho automatically usawa ulionekana lakini tukija hii haionyeshi huo usawa utapatikana kwa njia zipi. Je watalazimisha vp kwa vyama vya siasa kuwapendekeza wabunge wa jinsia hizi mbili.
Ni ngumu sana kuona ni namna gani hii katiba pendekezwa itasimamia misingi ya haki kwa pande zote yaani upande wa watendaji na wananchi.
Mi naona haki ziko vema sana katika hii Katiba Inayopendekezwa wakuu.

Siyo haki tu! Ni vema utambue haki inaenda sanjari na wajibu. Hivi unaonekana mtu wa ajabu inawezekanaje wabunge wawe wa jinsia moja tuu? Cha msingi ni kwamba kila mwenye sifa wakati wa mchakato wa kuwapata wanotaka kugombea ubunge, kila mtu anayetaka kuwania nafasi hiyo kwenye jimbo husika afanye hivyo. Ndiyo maana Katiba Inayopendekezwa IMEBAINISHA katika Ibara 139.-(1) juu ya Uchaguzi wa Wabunge, Kila baada ya Bunge kumaliza muda wa maisha yake, kutakuwa na uchaguzi wa Wabunge katika majimbo ya uchaguzi kama itakavyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi utakaofanyika kwa mujibu wa sheria.
(2) Kutakuwa na uchaguzi wa mbunge katika Jimbo la Uchaguzi ikiwa kiti cha Mbunge aliyechaguliwa kuwakilisha jimbo la uchaguzi kitakuwa wazi kwa sababu nyingine yoyote isiyohusika na Bunge kumaliza muda wake.
(3) Endapo tarehe ya Bunge kumaliza muda wake imetangazwa au inafahamika, hakutakuwa na uchaguzi mdogo wa Mbunge kwa mujibu wa ibara ndogo ya (2) ndani ya kipindi cha miezi kumi na miwili kabla ya tarehe hiyo.
Swali la msingi ni je kwanini tuendelee kuwa na wabunge wakubebwa badala ya kuchaguliwa kwa kupata kura nyingi zinazomuunga mkono katika jimbo kama katiba inavyojieleza.

Hayo ulosema hayana ukweli wowote we unabashiri tu, kama una uhakika weka ushahidi hapa.Hii katiba pendekezwa inategemea kupitia sheria zitakazotungwa na bunge na kutafsiriwa na mahakama ndio ziwe msingi mkubwa wa haki si vibaya lakini tuangalie ni bunge hili hili ndilo linalovuruga sera na mipango ya serikali kwa wabunge wake walio wengi kuegemea kwenye maslahi ya chama badala ya ukweli halisi na kuwatetea wananchi.
Rais kwa mamlaka aliyopewa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika katiba ya mwaka 1977 (ya sasa) IBARA YA 66 Kifungu cha Kwanza (e) amepewa mamlaka ya kuteua Wabunge wasiozidi 10, pia Kwa mujibu wa Sheria ya Katiba Inayopendekezwa, IBARA YA 129 (2)(c) Nanukuu, "Wabunge wasiozidi 10 watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa wenye sifa za kuwa Wabunge".
nimemaliza kunukuu.
PATA UJUMBE HUO ILI UELEWE.
makundi mbalimbali yamekuwa yakipigania kutajwa katika katiba na hata wengine kudiriki kutaka mambo ambayo kimsingi si ya kuingia katika katiba.
hapa tumejisahau kuwa kinachotusumbua si kutotajwa katika katiba ndio maana hatukuridhika huko nyuma bali kutokuwepo kwa misingi ya kutoa haki pengine katika katiba ndio tatizo kubwa.
jambo la kwanza kwetu sote iwe ni kupigania misingi ya kutoa haki kwa wote ijengwe katika katiba na hapo kila mmoja katika kundi lake dogo haki yake ataipata.
Umelalamika sana siku ya kupiga kura usifanye makosa ili Katiba iweze kutoa haki via Mahakama za Tanzania. Karibu
hapa tunajadili ili tuone ni kitu gani ambacho tunakihitaji na tujiulize kama kipo na tufanye maamuzi
Ego najua umeshatumia muda wako kwa umakini sana kuisoma na kuielewa Katiba inayopendekezwa klichobaki sasa ni kufanya maamuzi, kura yako ndiyo hatima yako!jiunga na mamilioni ya wtz kuipa support ili tuendelee kulijenga taifa.

yaani ego kaongea maneno mazuri leo sana, kawa mtu wa busara mnokamwe usikubali kitu usichoridhika nacho kwa kisingizioa chochote, tujadili ili kila mmoja achague kulingana na mtizamo wake kama ameridhika au la lakini si kwa ujinga wa kutojua kilichoandikwa kinamaanisha nini.
yaani ego kaongea maneno mazuri leo sana, kawa mtu wa busara mno