Kunena kwa lugha ni nini? Na nini hutokea pale mtu anaponena kwa lugha?

Umeichukulia kimwili ndio maana

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hiyo ndiyo maana halisi ya kutokea dhana nzima ya kunena kwa lugha. Hao wanaojifanya kwamba wamefikia level ya juu ya ufunuo wa Kimungu ni uongo.
Mungu hana lugha ya kusema ukiongea kwa lugha hii ndiyo anakuelewa zaidi, kwake hakuna matabaka wala upendeleo wa aina yoyote labda kama unazungumzia miungu na sio Mungu.
Ndiyo maana unaweza kupeleka maombi yako kwako kwa kikerewe, kichaga, kinyakyusa na bado ukapata jawabu stahiki kutoka kwake.
Hii iliwezekana wakati ule na ilitukia hivyo kwa dhima ya kuhakikisha neno linafika mahali pote Ulimwenguni.
Ndiyo maana huwezi kusikia hayo mambo kwenye Kanisa Catholic sababu wanajua hayana tija wala uhalisia kwasasa zaidi ya kutumika kama dhana ya kutapeli wasio na uelewa wa Maandiko.
Unaongea lugha ambayo unaowahubiria hawaeielewi ili iweje?
 
Unataka kunena kwa lugha? Ni rahisi sana wewe fanya kama ifuatavyo;

1. Hakikisha unaongea.

2. Ila uongee lugha ambayo wewe mwenyewe huijui, hujui maana yake wala hujawahi isikia mahali popote pale.


Ukifanya mambo mawili hayo hapo juu👆 utakua una nena kwa lugha
 
Nafkiri kichwa cha habari hakija kamilika .... ungesema kunena kwa luga isiyo eleweka .... nini kita tokea .... ngoja ni seme ivi kwe swala lolote linalool husu imani au kufanya meditation kuna namn flani unaingia kiroho outomatic wengine hadi jasho lina watoka sas hiyo process karibu kila dini ina tafsiri yake baada ya kuwa katika hali hiyo
 
sawa ibilisi bin shetani.
 
Nikwambie kitu....kwenye kila jambo huwa kuna namna ya kulifikia kwa urahisi. Kwa mfano ukitaka kufungua nati ambayo ina kutu...njia rahisi ni kutumia kimiminika kama mafuta(hydraulic) au maji...zipo njia nyingine lakini hiyo yaweza kuwa rahisi zaidi.
Ujue sisi viumbe tuna roho(pumzi ya uhai),ila kuna viumbe wana sifa zaidi ya hiyo...wana utashi/akili/fikra/mawazo/mitazamo/hisia/nafsi.....na hao ni sisi wanadamu.
Sasa matumizi yetu ya akili(rejea concept ya ego) yamekuwa juu sana kiasi cha kuivuga roho (remember roho ni nguvu tu...sio kitu shikika/oneka. Matumizi ya akili yanapozidi ndio matatizo mengi hutokea. Yanatokea kwa sababu tunaikandamiza nguvu yetu (roho).
Sasa basi watu wakaja na mbinu ni namna gani tutaziamsha nguvu zetu za kiroho...ili tuziishi Kama ilivyo kusudiwa.
Kutamka...shaghabhala sijui shendalabooo....sio uchizi...kuna maneno ukiyatumia akili/mawazo yanakuwa kama yanapoa/yanaenda masafa ya chini sana kwa wachache akili inasimama kabisa kabisa...
Kunena kwa lugha kunaitwa mantra(nadhani ni kihindi)
Kuna maneno/neno ukiyatumia unaifikia vizuri sana ndani yako.
Mfano wa maneno hayo ni kama
Om om om
Dabaga dabaga dabaga
Yahoo yahoo yahoo
Kwa kawaida ni maneno ambayo dunia nzima inaweza ikayatamka kwa sauti inayofanana.
Naweka pozi
 
Kama ni ugonjwa (schizophrenia) kwanini uwatokee walokole tu?

Kwanini hatusikii watu wa dini zingine wakinena kwa lugha?

Au huo ugonjwa unawachagua walokole tu?
Mafundisho ya ukole ndio yanafanya uwe na schizophrenia ukiingia tu akili yako inabdailika inaanza kupata magonjwa ya akili kutokana mafundisho kwa hiyo shida kubwa ni mafundisho yao ndio yanasababisha
 
H
Hii inatokea vizuri Sana kwenye muziki kwa kuusikiliza au kuucheza. Shida ni moja tu...hatufuati kanuni tukaifikia hiyo hali. Tunacheza ili mradi,unacheza huku unakunywa,unakula,unawaza waza sana,umekodoa macho kwa wengine...ushacheza muziki ukiwa umefumba macho?😁😁😁
 
Sisi Wakatoliki hatunaga hizo swaga. Hivyo nitakuwa muongo kuwasemea hao wanenaji. Labda waje wanenaji wenyewe watusimulie hali wanayojisikia.
Katoliki hakuna ibada za kiroho wala maombi ya kiroho humo mna ibada za litrujia tu
 
Ukiwa chini (deep) kabisa ya maombi, na u msafi rohoni, mtu mwenye HAKI, ni lazima roho mtakatifu akushikie katikati ya maombi, ile nguvu ni kubwa kiasi inakufanya uanze kuongea mambo usiyoyajua, unakuwa kwenye hali ambayo huwezi kuielezea.

Sisi wakristo tumepewa nguvu hii ambayo ki ukweli inatusaidia sana kupambana na maadui zetu, its working, its free if you need it ..100% sure.
 
That is your opinion, but the Bible suggest otherise, about speaking in tongues [emoji24]
 
Hakuna cha kunena kwa lugha wala nini.Mfano mimi nikiamua kusali kwa kisukuma ,wewe kisukuma haukijui hapo utafikiri ninanena kwa Lugha.
 
That is your opinion, but the Bible suggest otherise, about speaking in tongues [emoji24]
Kwamba kuongea kugha usiyoielewa hata maana yake wala waumini wanaokusikiliza ndiyo umeongea na Mungu? Kwamba Mungu hajui kiswahili mpaka akubadilishe uongee kwa lugha yakr yeye?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…