Kuoa wake wawili mpaka wanne kuna mantiki zaidi kuliko kuoa mke mmoja

Kuoa wake wawili mpaka wanne kuna mantiki zaidi kuliko kuoa mke mmoja

Nachojua nabii yacoub aliajarib na hakufanikiwa
 
Hiyo ni tamaa tu,penzi haligawanyika.
Kama ni kiongozi -popote pale- lazima kugawa mapenzi kwa wote waliopo pamoja nawe.

Hivyo Mungu anawapenda viumbe wake wote, Manabii na Mitume waliwapenda watu wao wote, Mzazi anawapenda watoto wake wote, hata wanyama madume hupenda majike wote/wengi.
 
Kuna kabila wana imani kuwa mwanamke mmoja hatoshi. Ila ni kweli ukiamgalia kwa makini kifalsafa. Kwa upande wa wakristu ni siasa tu!! Hakuna ukweli!! Nyumba ndogo kibao mtaani!!
 
Penzi haligawanyiki kuna mmoja anayependwa zaidi ya wengine!
Kwani nani alikwambia msingi wa mitala ni kugawa penzi sawa kwa wote ? Yaani huwezi kuwapenda wake zako upendo wa sawa ila lazima tuwapende wake zetu.

Kinachotakiwa kwenye mitala ni kumpa kila mke stahiki yake hasa katika huduma, upendo huchagizwa na anae pendwa. Hata wewe leo hii huwezi kuwapenda sawa watoto wako wote bali unaweza kuwahudumia kwa usawa watoto wako wote.

Kwahiyo hili tunalijua na linajulikana tangu na tangu.
 
Lazima kuna mmoja anakuwa moyoni zaidi ila kwa wengine zinakuwa tamaa za Mzee fisi
Hii si kweli sisi wanaume tunaweza tukawapenda wote na nyote mkawa moyoni ila hatuwezi kuwapenda sawa wote sababu mnatofautiana na upendo huendana na anae pendwa. Wanawake mnatofautiana sana.


Ndiyo maana tunakuwa na wivu kwa wake zetu wote.
 
Back
Top Bottom