Kupotea Kwa Thamani ya Familia au Ndoa

Kupotea Kwa Thamani ya Familia au Ndoa

Kama ujao usisubutu kuoa, One Day utakuja kunikumbuka kuoa ni Shida Tena ni Bonge la mtego, cheti kabla ya mtihani ndo Ndoa.
Wengi walioa nimewasikia wakinipa huo ushauri,kuna jamaa mmoja alifika maskani akanikuta nimekaa peke yangu naperuzi JamiiForums watu walikuwa wameenda kuangalia mechi ya Simba na Yanga,akapaki gari yake kali kweli,kisha akashusha kioo cha gari akasalimia Vizuri nikamuitikia nikatega sikio kumsikiliza nikidhani kapotea au kuna mahali anahitaji nimuelekeze.

jamaa akaulizia duka la mangi nikamuelekeza akaenda kisha akarudi na soda mbili na chupa ya grants,kisha akatoa na red cup mbili nikamwambia nashukuru situmii hapo hatujuani na ndio mara ya kwanza kuonana.
Jamaa akaanza kusonya huku anatunakana,nikamuuliza vp kaka kwema,huwezi amini jamaa alianza kulia kama mtoto kisha akaniuliza kama nimeoa nikamwambia bado akasema nakushauri usiingie kwenye ndoa ndoa ni uk*** bado nikawa simuelewi jamaa akasema huwezi nielewa kaka ila ushauri wangu ndio huo,hawa wanawake ni mashetani,tulizungumza muda mrefu akaniambia kuwa kabla ya kuingia kwenye ndoa alikuwa fresh kabisa ila baada ya ndoa akaanza kuumwa presha kwa kifupi mambo yalikuwa ni mengi.
 
Mkuu tafuta wa kufanana nae umri haurudi nyuma mwanetu. Mambinti wa kutulia kwenye ndoa bado wapo
Itakuwa anasubilia toleo jingine, na hao watakuja na mambo Yao, muda huo Mzee anaoa wakuja kula pension yake
 
Mkuu tafuta wa kufanana nae umri haurudi nyuma mwanetu. Mambinti wa kutulia kwenye ndoa bado wapo
Upo sahihi,ila kiukweli sidhani wote tulikuja Duniani kwa ajili ya kutimiza mission ya ndoa.
Kwa jinsi kichwa changu kilivyo hizo purukushani za ndoa sitoweza kuziimili kwakweli niwe muwazi tu.
 
Upo sahihi,ila kiukweli sidhani wote tulikuja Duniani kwa ajili ya kutimiza mission ya ndoa.
Kwa jinsi kichwa changu kilivyo hizo purukushani za ndoa sitoweza kuziimili kwakweli niwe muwazi tu.
Una umri gani mkuu. Kuna kitu nataka nikwambie
 
Upo sahihi,ila kiukweli sidhani wote tulikuja Duniani kwa ajili ya kutimiza mission ya ndoa.
Kwa jinsi kichwa changu kilivyo hizo purukushani za ndoa sitoweza kuziimili kwakweli niwe muwazi tu.
Ukifikisha miaka 50 ndiyo utakumbuka na umri huo labda mjane au mtalaka wa mtu, lakini binti atakupelekesha hata pension yako utaiona chungu
 
Maisha ya kiusela ni maisha ya kipuuzi sana, maisha yaliyojaa uchafu mwingi kwa kijana anaejitambua sidhani kama anaweza unga mkono Kataa ndoa
Ni kweli kabisa kuna kipindi unatamani utulie nyumbani na mwenza, sasa hujaoa Wala kuolewa wanakaa wasela tu ndani heshima unaitoa wapi sasa hapo!
 
Ukifikisha miaka 50 ndiyo utakumbuka na umri huo labda mjane au mtalaka wa mtu, lakini binti atakupelekesha hata pension yako utaiona chungu
Hapana siwezi kumbuka ndoa,kwakuwa ni kitu ambacho nimeshajipangia kuwa sikihitaji kwahyo haiwezi kunisumbua.
 
Ona kama hapa ndio nimetoka kwenye mitikasi yangu ya siku nzima, mama watoto ameniandalia diko na chai ya tangawizi Kali... Kuna maisha mengine nayataka zaidi ya haya? Hapo ni kulisongesha mdogo mdogo binadam usubili kufa uwaachie wengine Dunia hii
1739995730513960614695729357094.jpg
 
Hapana siwezi kumbuka ndoa,kwakuwa ni kitu ambacho nimeshajipangia kuwa sikihitaji kwahyo haiwezi kunisumbua.
Sawa haina shida, ila Kwa maisha ya kibongo bongo ukifika umri fulani wale rika lako wote watakuwa na familia baada yakzi kila mtu anaaga kwenda kuangalia familia yake wewe sasa utaanza urafiki na vijana wadogo, angalia usije jikuta unalia mwenyewe 😅, hapo mapenzi yote Kwa mama yako siku katangulia ndiyo utajua.

Ungeenda kuwa Padre wa RC unafia huko huko, lakini huko utakosa hata wakukupa maji ya kunywa.
 
Ni kweli unayosema ila yote hayo nimesha yafikiria na nimeona ni batili,rafiki wa kweli ni pesa tu hata watoto nao utafika umri wataenda kujitafutia maisha yao kwahyo bado utabaki mwenyewe kama ulivyo kuja mwenyewe ndio utakavyo ondoka mwenyewe.
 
Back
Top Bottom