Internal vacancy ni kwa waajiriwa tayari, (hao wanaojitolea si sehemu ya internal employees) si kwa watu wa kujitolea au interns!! Hawa NSSF in real sense siyo internal vacany bali ni kupendelea watu waliowapachika pale wajitolee kama hatua ya kwanza, na hatua ya pili ni hii kutaka kuwaajiri bila kutoa fursa kwa watanzania wote kugombea hizo nafasi!!Mkuu ni kwamba unakataa format ya Internal Vacant?
hii inafanyika Dunia nzima
Wee jamaa vipi post ya zamani unaleta leo?? Njoo na mada mpya tujadiliNdugu zangu habari ya saa hizi,
Kuna kazi zimetangazwa na NSSF, sasa wamesema kabisa wanaopaswa ku'apply ni wale walio kwenye kazi za mkataba NSSF.
Sasa sisi ambao hatupo kwa nini wanatubagua? Maana hata hao waliopo kwenye kazi za Mkataba wameunganishiwa na ma'godifaza yao.
Watoto wa wakulima hatupaswi kufanya kazi NSSF?
Nimeumia sanaa
Kuna wakati mwingine unaweza kuwaza kuna chuki tuNimeongezea hiyo attachment ya hizo kazi, soma kwa umakini utaelewa wasio na kazi ya mkataba NSSF hawaruhusiwiView attachment 2757218
Baadhi ya sekta zipo nje ya sheria/kanuni za Utumishi Jeshi,Police na Bunge...Mbona huulizi majeshi wanatangaza ajira kwa kigezo uwe umepitia JKT? KWANI WOTE WANAKUWA WAMEPITIA JKT? Ni sheria gani wanatumia? Tangazo lenyewe la ndani, wewe unasema la Umma.
Hii angetumiwa kigogo2014 kwenye page yake ya Instagram ingeruka haraka Sana na viongozi wengi wanaitazama, kwakweli huu ni uonevuMtendaji mkuu wa NSSF amevunja katiba ya nchi ibara ya 13, inayokataza ubaguzi wa aina yoyote. Kutangaza ajira kwa kuwabagua baadhi ya waombaji watanzania wenye sifa, huko ni kukiuka katiba ya nchi, AWAJIBIKE AU AWAJIBISHWE!!
Katiba nya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya:
13(4). Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au na mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya mamlaka ya nchi.
NSSF imekiuka klifungu hiki cha katiba ya nchi yetu kwa kuwabagua watanzania wengine wote wenye sifa za kuomba ajira zilizotangazwa pale NSSF, na kuwapendelea watanzania waliomo ndani ya NSSF aidha kwa kujitolea au kwa mikataba mifupi (ambao bila shaka waliingia humo kwa kupendelewa pia-uchunguzi inabidi ufanyike) ili wao pekee ndio waziombe nafasi hizo za ajira!
Inabidi Mtendaji mkuu wa NSSF ajiuzulu kwa kuvunja katiba ya nchi yetu! Hili jambo siyo dogo, na wakilipuuzia tutaenda mahakamani!! Maana haki, wajibu na maslahi ya kila mtu hulindwa na mahakama kwa mujibu wa ibara ya 13(3) ya katiba ya nchi nyetu inayosema: Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya ya watu yatalindwa na kuamuliwa na mahakama na vyombo vinginevyo vya mamlaka ya nchi vilivyowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.
Imeandikwq wapi kuwa ni PSRSDeal done, saiv michakato ya Ajira ni PSRS ndicho tulichokuwa tunakitaka
uzi umefika mwaka na miezi sasa, huu uzi umepitia mengi, ila tuweke imani zetu kuwa wata tangaza nafasi zingine karibuni na kila mtu ataomba.kwenye