Kutangaza nafasi za ajira kwa watu "Wa ndani ya NSSF" ni Ubaguzi, Rais Samia ingilia kati, unachonganishwa na wananchi!

Kutangaza nafasi za ajira kwa watu "Wa ndani ya NSSF" ni Ubaguzi, Rais Samia ingilia kati, unachonganishwa na wananchi!

Mkuu ni kwamba unakataa format ya Internal Vacant?
hii inafanyika Dunia nzima
Internal vacancy ni kwa waajiriwa tayari, (hao wanaojitolea si sehemu ya internal employees) si kwa watu wa kujitolea au interns!! Hawa NSSF in real sense siyo internal vacany bali ni kupendelea watu waliowapachika pale wajitolee kama hatua ya kwanza, na hatua ya pili ni hii kutaka kuwaajiri bila kutoa fursa kwa watanzania wote kugombea hizo nafasi!!
 
Ndugu zangu habari ya saa hizi,

Kuna kazi zimetangazwa na NSSF, sasa wamesema kabisa wanaopaswa ku'apply ni wale walio kwenye kazi za mkataba NSSF.

Sasa sisi ambao hatupo kwa nini wanatubagua? Maana hata hao waliopo kwenye kazi za Mkataba wameunganishiwa na ma'godifaza yao.

Watoto wa wakulima hatupaswi kufanya kazi NSSF?

Nimeumia sanaa
Wee jamaa vipi post ya zamani unaleta leo?? Njoo na mada mpya tujadili
 
NSSF MNAFAYA UBAGUZI, UONEVU NA UTAPELI WA HALI YA JUU KUHUSU SUALA LA AJIRA. MNAKIUKA SHERIA YA AJIRA.

Katika hali ya kusikitisha sana Mwezi huu shirila la umma la mkufuko wa hifadhi ya Jamii NSSF limetangaza ajira katika hali ya ubaguzi wa hali ya juu sana kwa kuutangazia umma wa Watanzania ya kwamba wanaopaswa kuajiriwa ni wale ambao wanafanya kazi za kujitolea kwenye ofisi zao (Special tasks).

Katika kipindi bacho kuna changamoto kubwa ya Ajira nchini NSSF wanawaingiza ndugu zao kufanya kazi kwa muda kwa kigezo kua ni ajira ya kujitolea kisha baadaye waombe kibali utumishi ili wawaajiri, huu ni ubaguzi, utapeli na uonevu wa hali ya juu sana.

TUNAOMBA NSSF, UTUMISHI, NA TAESA MJIBU MASWA YAFUATAYO:

1. Hao ambao mnadai wanajitolea kwenye ofisi zenu mlitumia utaratibu upi kuwapa hizo ajira? Mlitoa tangazo lini kwa watanzania wote wenye sifa wakapata fursa ya kuomba kuja kujitolea kwenu ili baadaye muwaombee kibali cha kuajira kutoka utumushi au sekretarieti ya ajira?

2. NNSF mmetumia sheria gani ya utumishi wa umma kuwatangazia watanzania wote kwamba wenye sifa za kuomba ajira ni wale waliojitolea kwenu?

3. Kulikua na haja gani ya kuutangazia umma wa watanzani ikiwa tayari mlikua na watu wenu mifukoni?

4. TAESA na SEKRETARIETI ya Ajira kwanini mmeruhu huu uvunjifu wa sheria ya nchi? Mna ajenda gani na NSSF ninyo?

Tunataka kulipeleka wapi hili taifa ikiwa tu kwemye taasisi za umma ambazo sasa zinakua ni miliki ya watu flani flani kutoa ajira za kibaguzi kiasi hiki?

IMG-20230924-WA0064.jpg
 
Aisee hii post mnatuma lakini mimi siwaelewi😳 mbona tangazo linasema la ndani halafu nyie mnasema
mwenzenu siwaelewi
 
Mbona huulizi majeshi wanatangaza ajira kwa kigezo uwe umepitia JKT? KWANI WOTE WANAKUWA WAMEPITIA JKT? Ni sheria gani wanatumia? Tangazo lenyewe la ndani, wewe unasema la Umma.
 
Huyu alitakiwa apewe jibu fupi tu "kalagha bhaho" bhasssss. Huu mjadala umeletwa hapa na ilielezwa tayari. Yeye Bado kakomalia kana kwamba atapata yeye.
 
The Public Service Recruitment Secretariat (PSRS) is a government organ with a status of independent Department established specifically to facilitate the recruitment process of employees to the Public Service. Public Service Recruitment Secretariat was established by the Public Service Act No. 8 0f 2002 as amended by Act No. 18 of 2007, section 29(1).

Vision​

To be a Centre of Excellence in Public Service Recruitment in the region.

Mission​

To undertake recruitment of Public servants using modern approaches by adhering to principles of equity, transparency and merits as well as providing advice to employers on employment related matters.

Functions Of Public Service Recruitment Secretariat​

The major role of PSRS is to facilitate recruitment in the Public Service. According to the Public Service Cap. 298 of 2002 as amended by Amendment Act No. 18 of 2007 section 29 (1), the functions of PSRS are:-

  • Search for various professionals with special skills and prepare database for such professionals for easier recruitment;
  • Register graduates and professionals for purposes of ease of reference of filling vacant posts;
  • Advertise vacant posts occurring in the public service;
  • Engage appropriate experts for purposes of conducting interviews
  • Advise employers on various matters related to recruitment, and
  • Do any other act or thing which may be directed by the Minister responsible for Public Service.

Core Values​

The core values of PSRS cornerstones of work performance and conduct in adaptation to changes in society, government, politics, and technology. The following were PSRS core values:-

  • Pursuit of excellence in service delivery.
  • Loyalty to Government.
  • Diligence.
  • Integrity.
  • Courtesy to all.
  • Respect for the law, and
  • Proper use of official information

Iv Hawa wabunge waliokuwa wanapigia upatu wanaojitolea kuajiriwa na taasisi kuajiri zenyewe, maana ya iyo PSRS ni nini? Na ili walilipitisha wao Leo hii iweje walivunje. Viongozi mnajisahau sana.
 
Mbona huulizi majeshi wanatangaza ajira kwa kigezo uwe umepitia JKT? KWANI WOTE WANAKUWA WAMEPITIA JKT? Ni sheria gani wanatumia? Tangazo lenyewe la ndani, wewe unasema la Umma.
Baadhi ya sekta zipo nje ya sheria/kanuni za Utumishi Jeshi,Police na Bunge...
 
Mtendaji mkuu wa NSSF amevunja katiba ya nchi ibara ya 13, inayokataza ubaguzi wa aina yoyote. Kutangaza ajira kwa kuwabagua baadhi ya waombaji watanzania wenye sifa, huko ni kukiuka katiba ya nchi, AWAJIBIKE AU AWAJIBISHWE!!

Katiba nya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya:
13(4). Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au na mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya mamlaka ya nchi.

NSSF imekiuka klifungu hiki cha katiba ya nchi yetu kwa kuwabagua watanzania wengine wote wenye sifa za kuomba ajira zilizotangazwa pale NSSF, na kuwapendelea watanzania waliomo ndani ya NSSF aidha kwa kujitolea au kwa mikataba mifupi (ambao bila shaka waliingia humo kwa kupendelewa pia-uchunguzi inabidi ufanyike) ili wao pekee ndio waziombe nafasi hizo za ajira!

Inabidi Mtendaji mkuu wa NSSF ajiuzulu kwa kuvunja katiba ya nchi yetu! Hili jambo siyo dogo, na wakilipuuzia tutaenda mahakamani!! Maana haki, wajibu na maslahi ya kila mtu hulindwa na mahakama kwa mujibu wa ibara ya 13(3) ya katiba ya nchi nyetu inayosema: Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya ya watu yatalindwa na kuamuliwa na mahakama na vyombo vinginevyo vya mamlaka ya nchi vilivyowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.
Hii angetumiwa kigogo2014 kwenye page yake ya Instagram ingeruka haraka Sana na viongozi wengi wanaitazama, kwakweli huu ni uonevu
 
Back
Top Bottom