Mtendaji mkuu wa NSSF amevunja katiba ya nchi ibara ya 13, inayokataza ubaguzi wa aina yoyote. Kutangaza ajira kwa kuwabagua baadhi ya waombaji watanzania wenye sifa, huko ni kukiuka katiba ya nchi, AWAJIBIKE AU AWAJIBISHWE!!
Katiba nya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya:
13(4). Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au na mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya mamlaka ya nchi.
NSSF imekiuka klifungu hiki cha katiba ya nchi yetu kwa kuwabagua watanzania wengine wote wenye sifa za kuomba ajira zilizotangazwa pale NSSF, na kuwapendelea watanzania waliomo ndani ya NSSF aidha kwa kujitolea au kwa mikataba mifupi (ambao bila shaka waliingia humo kwa kupendelewa pia-uchunguzi inabidi ufanyike) ili wao pekee ndio waziombe nafasi hizo za ajira!
Inabidi Mtendaji mkuu wa NSSF ajiuzulu kwa kuvunja katiba ya nchi yetu! Hili jambo siyo dogo, na wakilipuuzia tutaenda mahakamani!! Maana haki, wajibu na maslahi ya kila mtu hulindwa na mahakama kwa mujibu wa ibara ya 13(3) ya katiba ya nchi nyetu inayosema: Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya ya watu yatalindwa na kuamuliwa na mahakama na vyombo vinginevyo vya mamlaka ya nchi vilivyowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.