Kutawala kwa picha ya Rais Samia uwanjani ni ishara ya mafanikio katika kujenga umoja wa kitaifa na kukubalika kwake

Hizi ndo mambo alizotuachia Magufuri kujipendekeza pendekeza,Maboss wa hz timu wanajipendekeza ili mambo yao yaende,hao mashabiki unaowaona wamebeba hizo picha wanalipwa na maboss wa timu
 
Duuh!!
Unashindwa kusifu,kuabudu, kumuimbia na kumchezea Mungu wako,badala yake unamgeuza binadamu mwenzako "mungu"!!!???

Kweli umasikini wa akili na kipato ni vitu vya kutorithisha watoto wet
Mambo ya kuharibiana siku, wengi wa wanaomsifia Samia na kubeba picha ni kujipendekeza tu lakini mioyo yao ukiipasua iko tofauti, siku nyingine usituletee upuuzi wako huo yaani umsifie mtu aliyeleta hali ngumu ya maisha kwa Watanzania.
 
Hakuna mtanzania wa hivi....wewe unalipwa, kubali tu
Au wewe kwenu kilo ya mchele shilingi ngapi?
Mimi Ni mkulima mwenyewe kwa hiyo nasi wakulima tulikuwa tumechoka kupata hasara kila mwaka, Tunamshukuru Rais Samia kwa kuhakikisha kuwa wakulima tunapata soko la uhakika na kwa Bei nzuri na hivyo kutusaidia kuinuka kiuchumi.

Kilimo Ni biashara, unakaribishwa kulima maana Tanzania tuna ardhi yenye rutuba na yakustawisha mazao mbalimbali maeneo mengi
 
Hizi ndo mambo alizotuachia Magufuri kujipendekeza pendekeza,Maboss wa hz timu wanajipendekeza ili mambo yao yaende,hao mashabiki unaowaona wamebeba hizo picha wanalipwa na maboss wa timu
Siyo kila mtu analipwa Kama unavyolipwa wewe
 
Umesikia bei ya korosho lakini? Au unajiangalia wewe tu, je bei kuwa juu mwaka huu sio inasababishwa na mavuno hafifu?
 
Chawa
 
Umesikia bei ya korosho lakini? Au unajiangalia wewe tu, je bei kuwa juu mwaka huu sio inasababishwa na mavuno hafifu?
Inatokana na mazingira mazuri aliyoyaweka mh Rais kumuwezesha mkulima kuuza popote penye Bei nzuri, ndio sababu ya kauli mbiu yake ya kilimo Ni biashara
 
Hata nafsi yako inakusuta kwa hiki ulichoandika, pole sana
 
Week ya tatu maji yanatoka ya tope mjini kabisa Magomeni na kuna watu bado wako ofisini.
 
Wewe ipo siku utajikuta umechanganyikiwa,
 
Kwani hufurahi namna Taifa lilivyoungana na kuwa kitu kimoja chini ya uongozi wa mh mama Samia au unataka na kutamani kuona Taifa likiwa vipande vipande na lililogawanyika
Sawa tunamkubali na Kumpenda rais, Ila tabia hii sio nzuri hata kidogo na ni hatari sana na tunapoelekea itakuwa na matokeo hasi.

Tuache michezo iwe sehemu ya watu kujipumzisha na kufurahi na watu wasahau itikadi zao.

Kwa Tanzania haijawahi toke ila naomba rais mwenye,Tff,CUF na FIFA wakemee ili jambo ili michezo uwe sehemu salama kwa wote na kwa itikadi zote.
 
Mkulima wa lumumba huyo hakika ukiona mtu anaanza na mara ooh mimi mkulima ujue humo hamna kitu kwasababu hakuna sababu ya kuanza kujisifu mapema hivyo,laiti ungekuwa mkulima ungejiuliza hizi bei za pembejeo ni rafiki kwa mkulima?

Vipi bei ya mbegu nayo ni rafiki kwa mkulima? ila kwakuwa wewe ni kidali poo sikushangai
 
Picha kwangu nimeona kama ishara ya sisi wamoja. Watanzania.
 
Tulikuwa tunasifiana ila hatukuwa tunasifiana kijinga hivi, watu walisifiwa kwa hoja.

Labda uniambie, haya mambo ya kubeba picha za rais kwenye michezo ya mpira uliiona awamu ya nne?

Ukiona nguvu kubwa inayotumika,basi jua kuna tatizo.
 
Tuseme tu ukweli ni ushamba.
Hivi na kwa wenzetu wanafanya hivi?
Mliopo nchi nyingine mnijuze tafadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…