Kutawala kwa picha ya Rais Samia uwanjani ni ishara ya mafanikio katika kujenga umoja wa kitaifa na kukubalika kwake

Nawachukia sana mnapowasifu viongozi Badala ya kuwaonesha Mahali wanapokosea Ili warekebishe.

Mnawapotosha viongozi wetu. Hamuwasaidii kuongoza😠😠

Unajitafutia LAANA ndugu Lucas.
 
Uchawa wako ndiyo unaashiria matumaini ya kuteuliwa.
Kwani kuongea ukweli ndio uchawa? Kwa hiyo wewe hapo unapinga pinga kila kitu ili upate faida gani?

Tusijenge Tabia ya kuwakatisha Tamaa viongozi aina ya Rais Samia waliojitoa na kujitolea kututumikia watanzania kwa uzalendo mkubwa
 
Rubbish
 
Nawachukia sana mnapowasifu viongozi Badala ya kuwaonesha Mahali wanapokosea Ili warekebishe.

Mnawapotosha viongozi wetu. Hamuwasaidii kuongoza😠😠

Unajitafutia LAANA ndugu Lucas.
Hata wewe hujazuiwa na mtu kufanya hivyo, nami naandika kulingana na ninavyoona na kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais Samia
 
Hata jina lako linazungumzia ulivyo total rubbish
 
Hata wewe hujazuiwa na mtu kufanya hivyo, nami naandika kulingana na ninavyoona na kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais Samia
Kama unampenda msaidie aboreshe na kuziba panapovuja.

Ukimpenda mtu mwambie Kweli, akifanya Vyema mwambie, akikosea mwambie arekebishe.

Yaani wewe unaona MAZURI tu???

Nani kakwambia kiongozi wetu ni Malaika hakosei???
 
Mambo ya kuharibiana siku, wengi wa wanaomsifia Samia na kubeba picha ni kujipendekeza tu lakini mioyo yao ukiipasua iko tofauti, siku nyingine usituletee upuuzi wako huo yaani umsifie mtu aliyeleta hali ngumu ya maisha kwa Watanzania.
Uwe na shukurani na kujifunza kupongeza, Hivi wewe huoni kuwa mh Rais amefanya kazi kubwa Sana katika kumsaidia mwananchi kiuchumi? Huoni alivyopambana kukabiliana na mfumuko wa Bei kwa kutoa Ruzuku ya mabillioni ya pesa za kitanzania?

Huoni kazi kubwa aliyoifanya mh Rais kusogeza huduma karibu ya mwananchi na hivyo kupunguza adha ya kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma?
 
Kama unampenda msaidie aboreshe na kuziba panapovuja.

Ukimpenda mtu mwambie Kweli, akifanya Vyema mwambie, akikosea mwambie arekebishe.

Yaani wewe unaona MAZURI tu???

Nani kakwambia kiongozi wetu ni Malaika hakosei???
Kwani wewe siyo mtanzania? Nani kakuzuia kukosoa panapovuja,
 
Week ya tatu maji yanatoka ya tope mjini kabisa Magomeni na kuna watu bado wako ofisini.

Ni aibu sana, jana niliona malalamiko ya maji kukosekana mjini wiki nzima. Kuna wat hawastahili hata kwa dakika moja kubakia katika ofisi za Umma, lakini kwa sababu hizi hizi za 'uchawa' bado wapo na hawawezi kuondolewa.

Sijui kama watu wanaona vile nionavyo mimi, tumetengeneza taifa la ajabu sana, taifa la machawa kila mtu ni chawa hadi Waziri ili aweze kuishi katika baraza ni lazima awe chawa ili kuficha UDHAIFU wake kiutendaji.

Hapa tulipofika sioni tukitoka, ilianza awamu ya JPM naona inaendelea na ajaye pia ataendelea nayo.
 
Wenzako walikua wanaweka namba za simu.

Ili vijana wa lumumba wakupigie.

#MaendeleoHayanaChama
 
Tuseme tu ukweli ni ushamba.
Hivi na kwa wenzetu wanafanya hivi?
Mliopo nchi nyingine mnijuze tafadhali
Ndio nchi nyingine wenyewe wametuzidi sisi maana wenyewe Wana Tabia na utamaduni wa kumpongeza kiongozi pale anapofanya vizuri na hata Kama Ni kukosoa wanaweza wakakosoa utekelezaji wa Sera lakini wakaunga mkono Sera husika,

lakini huku kwetu unakuta mtu kazi yake kuanzia January Hadi December nikupingaa tu kila kitu na kila Jambo, kila Sera na kila ajenda ni kupinga tuuu bila sababu Wala hoja za msingi, ndio sababu unaona hata wananchi kwa Sasa wanawapuuza wapinzani na upinzani
 
Nchi yetu hii Mungu asaidie tu
 
Kwani wewe siyo mtanzania? Nani kakuzuia kukosoa panapovuja,
Nataka kuona wewe ukiandika Thread zenye kulenga kumshauri kiongozi wetu aboreshe zaidi ktk sekta mbalimbali Ili tuongeze ufanisi.

Unachokifanya wewe ni kama vile tupo Mbinguni kwamba Kila kitu kipo sawa.

Hapo unampeleka SHIMONI kiongozi wetu.

Jifunze Kwa Nyerere alisikiza hoja mbadala zenye Nia ya kulisaidia TAIFA.

Ameeeen
 
Wenzako walikua wanaweka namba za simu.

Ili vijana wa lumumba wakupigie.

#MaendeleoHayanaChama
Tujikite katika kulijenga Taifa letu na kumuunga mkono mh Rais katika juhudi zake za kuona uchumi wa kila mtanzania unainuka
 
Sasa kubeba mipicha kila mahali inahusu nini? Kwenye mechi si tushangilie mpira siasa tuweke pembeni?
 
Kweli dunia hii wajinga wapo aisee.
 
Dawasco na Tanesco ndiyo wanaotaka kumharibia.
 
Hizo hoja mbadala ndio nataka na wewe uzilete ili Nasi tuzione na kutoa mawazo yetu lakini kwa Sasa nimeona namna mh Rais alivyojitahidi kuweka mikono yake katika kila secta ili ipate kuinuka na kuwanufaisha Watanzania wengi, ndio maana unaona hata secta binafsi mh Rais anajitahidi na kufanya kazi kubwa ya kuweka mazingira mazuri ili iweze kukua na kutoa mchango katika uchumi wetu na hata kutoa ajira kwa vijana wa kitanzania
 
Dawasco na Tanesco ndiyo wanaotaka kumharibia.
Watendaji wasiojitambua na kufanya kazi kwa mazoea naamini mh Rais atawawajibisha ili mtanzania apate huduma Bora na ya uhakika hasa ukizingatia ukweli kuwa umeme ndio kila kitu katika shughuli nyingi Sana za kiuchumi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…