Maneno mafupi ya Lowasa lakini ukiyatafakari unaweza kuandika hata kujaza kurasa zaidi ya 10 kwani kiuhalisia yapo kwenye ilani ya chama ya uchaguzi hivyo hapa ameongea kwa ufupi mno. wanaoongea maneno mengi ni CCM lakini vitendo vichache na ndio maana wanajikuta wakiishutumu serikali ambayo na wenyewe ni watendaji ndani ya serikali hiyohiyo
"Niwashukuru waliopita kwa kunisemea, niliahidi kampeni safi lakini wameanza lakini wakianza ndio hivyo watavyopata. Kipengele cha kwanza elimu, cha pili elimu na cha tatu elimu. Maneno haya nimeyaazima kwa waziri mkuu wa Uingereza. Cha kwanza elimu itakuwa gharama ya serikali kuanzia darasa la kwanza mpaka chuo kikuu. Eneo la pili la kilimo ili tuweze kutengeneza ajira za kutosha.
Tatu tumeweka umuhimu sana kwenye afya iwe bora kwa akina mama na watoto wadogo. Wanokwenda nje ya nchi ni watu wakubwa, eneo jingine ni mawasiliano, ni muhimu sana tuwekeze. Kwa hio jambo la kwanza nitakalofanya ni kujenga upya reli ya kati iende Kigoma na Mwanza. Tutafufua Air Tanzania, nisme mambo matatu ya mwisho.
Mashehe wa Zanzibar wako jela muda mrefu sasa, nasikia habari ya babu Seya, nimeisikia. Naelewa hisia zenu kuhusu babu Seya, Tutatumia utawala bora kuwatoa muda ukifika."