Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

UKAWA wenzangu mi nafikiri mambo yalipofika sasa tunamhitaji Dr Slaa arudi jamani. Lowasa amepwaya kabisaaaaaa. Hatuchukui nchi kwa namna hii

Afadhali wewe umesema kweli, nakupenda sana sana. nakupa big 5
 
Mimi kama mwanacham wa CHADEMA nimesikitishwa sana na mwenendo wa.leo yaani mgombea uraisi anaongea dakika 11...Leo ndo ingekuw siku ya lowassa kuelez sera zake kwa mda mrefu coz nyomi ya leo ilikuw ya kutosha na watu walikuw na shauku ya kumsikia ndug Edward lowassa.nimekwatish tamaa sana na mkututano wa leo

Maneno mafupi ya Lowasa lakini ukiyatafakari unaweza kuandika hata kujaza kurasa zaidi ya 10 kwani kiuhalisia yapo kwenye ilani ya chama ya uchaguzi hivyo hapa ameongea kwa ufupi mno. wanaoongea maneno mengi ni CCM lakini vitendo vichache na ndio maana wanajikuta wakiishutumu serikali ambayo na wenyewe ni watendaji ndani ya serikali hiyohiyo

"Niwashukuru waliopita kwa kunisemea, niliahidi kampeni safi lakini wameanza lakini wakianza ndio hivyo watavyopata. Kipengele cha kwanza elimu, cha pili elimu na cha tatu elimu. Maneno haya nimeyaazima kwa waziri mkuu wa Uingereza. Cha kwanza elimu itakuwa gharama ya serikali kuanzia darasa la kwanza mpaka chuo kikuu. Eneo la pili la kilimo ili tuweze kutengeneza ajira za kutosha.

Tatu tumeweka umuhimu sana kwenye afya iwe bora kwa akina mama na watoto wadogo. Wanokwenda nje ya nchi ni watu wakubwa, eneo jingine ni mawasiliano, ni muhimu sana tuwekeze. Kwa hio jambo la kwanza nitakalofanya ni kujenga upya reli ya kati iende Kigoma na Mwanza. Tutafufua Air Tanzania, nisme mambo matatu ya mwisho.

Mashehe wa Zanzibar wako jela muda mrefu sasa, nasikia habari ya babu Seya, nimeisikia. Naelewa hisia zenu kuhusu babu Seya, Tutatumia utawala bora kuwatoa muda ukifika."
 
Kweli UKAWA wameshindwa kabisa kutumia uwingi huu wa watu kutuambia watatufanyia nini?!kweli CCM inajua kucheza na akili za watu!wanajadili kauli ya Warioba na Mkapa tu

BTW Tunashukuru kwa kutujulisha kua Lowasa ni mgonjwa

Hizi ngonjera peleka lumumba. Hata akiwa ndani ya jeneza nitampa kura yangu.
 
Yaan Lowasa anataka tumchague ili amtoe babu seya!!!! Yaan hio ndo sera ya kumpeleka ikulu. Kweli huu ni uchiziiiii.... Huyu jamaa anawaaibisha UKAWA.......

uzi wa mgombea wenu mmemwachia nani? Hata page kumi wap ila wa lowasa pg 99
 
Huyu lofa kashindwa tena kuongea. Halafu bado mnataka awe Rais?

Huo ni zaidi ya upumbavu huo ni uzumbukuku.

Mmezoea ngonjera hadi hamjui mambo ya msingi!
Yaan kwenu anayesimama na kuimba tu kama kasuku ndo mtu!
Hata awe bubu! Watz wameamua! ! ! !
 
CDM mazuzu du! sioni lolote hapa ujinga mtupu


Mnaowaleta China na madawa ya kulevya ndo wajanja?

We unataka wakuahidi ahadi ngapi??

Mimi nnachotaka huyo bwanyenye anaewabebesha madawa ya kulevya watu huko bongo na kuwaleta China atajwe na kila MTU amjue ili tueshimiane
 
Nimeshatoka Jangwani nipo home kabla sijaingia mtaani kupiga dubai.....
Nasema sitemi mate ng'oo, kuna kibaraka mmoja wa watala yuko ofisi nyeti kuliko nyeti zenyewe, na tumekaa wote jangwani huku yeye akiwa na kazi maalum na mimi kama eye witness, nakuhakikishia ccm inaondoka mwaka huy na badly hawana mgombea.

Ukiona mpaka ofisa wa ile ofisi yetu ys pale Obey anaongea kwa mdomo wake hali ni mbaya ujuwe kimewaka.
Kuna extra ordinary power ndani ya Lowasa washirikina wanaiita ngekewa hata mimi pia kuna wakati nashindwa kujuwa huyu jamaa ana nini mpaka apendwe hivi?
Halafu hizi ngekewa za uzeeni wakati life span ishapungua............................ dah! nway.
 
Watu hawana mpango na lowasa na sera zake....wanachotaka ni ccm kutoka madarakani tu
 
Nimefurahi sana kwasababu kwa kinywa chake mwenyewe leo katamka hadharani ana "tatizo" ijapokuwa ameshindwa kuliweka wazi ..Lowassa tunakushukuru kuusema ukweli, una tatizo na ndo maana hujaweza kuongea, tatizo hilo ni lipi na limeanza lini? Sumaye kajitahidi sana kuficha lakini hakujua wewe mwenyewe utakuja kupasua jipu lako, una tatizo mzee wewe ..kapumzike nyumbani uachane na maigizo

Makufuli alipoenda kunywa kikombe cha babu alikuwa ana tatizo au alienda tu kuongeza nguvu za kiume ?
 
tambwe hiza kada wa zamani wa ccm amemshangaa Dr mjinga Harison mwakyembe kwa kusema uongo kuwa Lowasa ataweza shtakiwa kwa ufisadi wa Richmond kwani anahusika mojakwamoja akiongea kwa ushahidi wa Hansard za bunge alisema mwakyembe alisema kuwa kamati yake haijamkuta Lowasa na makosa ila kwa kuwa ndie mtendaji mkuu wa serikali inamwomba ajipime mwenywwe
tambwe hiza amemshanga Dr mwakyembe kwa nini maneno aliyoaongea juzi mbeya hakuyasema kipindi kile.kama alikuwa Ana ushahidi kuwa Lowasa alihusika na ufisadi wa richmond hii inaonyesha mwakyembe anaudhalilisha u Dr wake.kwa sababu ya tumbo..kweli mwaka huu wachumia tumbo tutawjua
 
Back
Top Bottom