Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015


Katiba mpya ya watz ndilo jibu la ufisadi
 
Am back ladies and gentlemen.
Uwiiiiii! Sijawahi kufurahi kama leo, sijawahi kuona mkutano wenye watu wengi tokea nizaliwe kama leo.
Nimepagawaaaaaaaaa nashindwa cha kusema jamani Lowassa anapendwa sana.
Na mwaka huu ni dhahiri kua UKAWA ndio wanachukua nchi!
Ngojeni nipumzike jamani.
 

Ni kazi sana kujaribu kumbeba asiebebeka Mkuu. Pole
 
Dr. Slaa yuko principled sana na asingeweza kushiriki mazingaombwe haya. Wanasema you must stand for something or you will fall for anything. Ndiyo ni mwanasiasa lakini pia alikuwa Padri. Ni yeye aliyemtaja Lowassa kwenye ile list of shame pale Mwembeyanga. Kama padri leo hii tena asingeweza kuja kujichanganya jukwaani na mbele ya Mungu wake. Na kwa hili Slaa ataheshimiwa daima na historia itamhukumu hivyo.

Wale wabunge 30 hakuna hata mmoja aliyejiunga na CHDM. Hata sijui imekuwaje. Na Lowassa mwenyewe kwa kweli hakuongelea sera thabiti na kidogo amenishangaza kuongelea mambo ya kumtoa gerezani babu Seya mtu aliyefungwa kwa kosa la ulawiti. Utafikiri hii ndiyo sera ya UKAWA.

Anyway ngoja tuone lakini nadhani at some point reality will start settling in na hii excitement waliyonayo watu juu ya huyu mzee itaanza kupungua. His lack of charisma, energy, enthusiasm, speaking ability and understanding of the environment and context he is in is real troubling. Time will tell!
 
Kila mtu anaju watanzani wanataka nini na matatizo ya watanzania yanajulikana,sera zimeshaandikwa ,zinaitaji mtekelezaji tu.
 
1 ELIMU
2 ELIMU
3ELIMU
4 KILIMO
5 AFYA
7KILIMO CHA KISASA

8ATAWATOA MASHEKH WA UAMSHO KWA KUFATA TARATIBU ZA UTAWALA BORA
BABU SEYA
NA DAUD BALALI ATARUDISHWA NCHINI

9 RELI YA KATI ITAJENGWA UPYA



10 ATC ITAFUFULIWA

hatuwez zidiwa na vinchi VIDOGO Kama RWANDA MALAWI KENYA
 
Unadhani Rais Mstaafu Wa Awamu Ya Tatu Mkapa Alipowaita " Wapumbavu Na Malofa " Alikosea? Mkapa Ni Zaidi Ya Genius Wachache Mno Dunia Inaojivunia Kwa Sasa.

Msitake kutuaminisha ujinga. Miaka yote tumekuwa na wagombea wenye maneno mengi mazuri lakini sio wafanyaji. Kusema sana hakumaanishi ndie bora, mara zote waliobora matendo yao ndio huzungumza na sio vinywa vyao.
 
Huyu jamaa katika watu wa kudharau ni huyu,yeye anaona dili kubadilisha vyama kama mashati!!alitoka ccm akahamia cuf,baada ya muda akarejea ccm sasa hivi ametoka tena.Shame on him
 
Nakubaliana na wewe mkuu..kaongea vya maana sana. Elimu bure hadi chuo kikuu, kujenga upya reli ya kati, kufufua air tanzania...sasa sijui watu wanataka hotuba ndefu za nini
 

We kweli upo analytical, congrats Mkuu
 

Kwendraaaaaaa
 
yule Tambwe Hiza anajua sana propaganda wasoiwasi wangu asije kuwa mamluki
 
1 ELIMU
2 ELIMU
3ELIMU
4 KILIMO
5 AFYA
7KILIMO CHA KISASA

8ATAWATOA MASHEKH WA UAMSHO KWA KUFATA TARATIBU ZA UTAWALA BORA
BABU SEYA
NA DAUD BALALI ATARUDISHWA NCHINI

9 RELI YA KATI ITAJENGWA UPYA



10 ATC ITAFUFULIWA

hatuwez zidiwa na vinchi VIDOGO Kama RWANDA MALAWI KENYA
 
hayo yako, ye kasema 1.elimu, 2.elimu,3.elimu 4.atamtoa babu seya basi! Naona ana loose memory kila uchao! Vipaumbele vyake vya mama ntilie na bodaboda kavisahau tena.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…