Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Khaa!!! Akili fupi bana zinashindwa kutofautisha kati ya ushabiki na upigaji kura..
 
Nasema LOWASSA ndie rais anae takiwa, ukiongea saaana unasema na uongo, nimempenda bureeeee, hatutaki story tenaaaa.
 

Karibu nifah, karibu kamandaaa leoo ni furaaaahaa saana.. Tupige kuraaa tuu sasaaa
 
Sasa nimeanza kuamini lengo la mbowe kumsajili sumaye.kumbe mzee mamvi hajiwezi kabisa yeye naona abaki kutoa fedha tu.
 
tukutanr katka utekelezaji, wala haiitaji polojo na kuelezwa masaa menngi utekelezaji hakuna ..
 
Tatizo la MUDA wa kuhutubia usipotoshe

Hayo niliyoyasema yamo kwenye hotuba yake jangwani leo na ni matamshi yake ya hawari kabisa, itafute mkuu badala ya kukuza mjadara bure
 
hivi hawa magambaz ksma nzige mamluki hawa wametokea wapi...

piga ua kura kwa lowassa

mimekupenda bure mdada achana na hao nzi wa kijani na njano njoo pm tuunganishe nguvu😉😀
 

I am very dissapointed.
Heri ningejikalia nyumbani tu leo.
Makamanda wamekuwa waongo sana.
Waongo kweli kweli..
 
Kumbe nilikuwa sahihi kukaa pembeni na Dr.Slaa, sijutii uamuzi wangu.!

UKAWA wenzangu mi nafikiri mambo yalipofika sasa tunamhitaji Dr Slaa arudi jamani. Lowasa amepwaya kabisaaaaaa. Hatuchukui nchi kwa namna hii

Mahaba kwa Lowassa yanazidi, Josefina aje kufanya nini? Mtu anayeamrishwa na mkewe hatuna muda naye.
 
Napenda UKAWA hasa chadema lakini kwa uraisi kama vile watatuangusha. Naona kama wameanza vibaya sijui labda kwa kisingizio cha muda. Huenda huko mikoani watapata muda wa kuongea sana tuone waliyoyapanga
wewe unapenda wanaoongea sana!?
 
Nakubaliana na wewe mkuu..kaongea vya maana sana. Elimu bure hadi chuo kikuu, kujenga upya reli ya kati, kufufua air tanzania...sasa sijui watu wanataka hotuba ndefu za nini

Umemsahau babu seya na balali, ni vizuri umzungumzie mtu kwa ujumla wake Mkuu
 
UKAWA wamechemka sana sana, ccm bado wako vizuri sana, kama ukiwapa hawa nchi, basi hata uchumi wetu utakuwa kama wa Mugabe, na kama urais ndo hivi nilivomskiliza Lowasa, basi kila mtu anaweza.
 
Amezungumza mambo kama sita hivi, na ma3 kati ya hayo ni babu seya, balali na mashehe wa zanziba. Hayo ndo tunayoyataka kama taifa Mkuu. Think kwa kina kaka

Utakuwa una matatizo na mtindio wa Ubongo! Kataja Mambo makuu kwa ujumla wake:
1. Elimu, Elimu Elimu
2.Kilimo
3.Afya
4. Mawasiliano(Reli ya kati na ATC)
5. Utawala wa Sheria( ambapo kuhusu Masheikh amesema atashughulikia ili kuona haki inatendeka, kuhusu babu Seya aliwajibu wale walioonyesha bango kuwa nafaham na nitaahughulikia)

Mengine kasema yapo kwenye tovuti ya CHADEMA.
Mgombea mwenza kagusia Katiba Mpya.

Mimi binafsi nmependezwa na Ilani ya kisomi ambayo haina UDANGANYIFU kwa mambo ambayo ni kiini macho.
 
Tumaini Makene unatuangusha. Hadi sasa hakuna taarifa za mkutano wa leo jangwani acheni uzembe au mnasahau kazi zenu. Acheni upumbavu nendeni na kasi ilivyo. Je kuanzia hiyo kesho ya mikoani tutapata taarifa kwa wakati kweli?
Mnatukwaza sana na kutuvunja moyo
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…