Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

..tatizo magamba m/kiti wenu kawafundisha mipasho, basi nyie mnadhani kila mtu amelelewa hivyo hovyooo...
lowassa amekuja kuelezea wananchi atawafanyia nn wakimchagua,vilaza wa ugambani huku wanalalamika eti ooh kaongea dkk 7, we kunguru unadhani lowassa alikua peke yake pale au muda ulikua unamsubiri yeye tu.?!
 
Acheni kuweweseka magamba kwani muda wa kampeni umeiaha? Lowassa hata asipopiga kampeni atashinda tu, anasubiri kuapishwa tu pale magogoni
 
Ikiwa hao ndiyo mawaziri wakuu waliopita! No wonder Tanzania tuna safari ndefu sana ya kwenda.

Hata wanachoongea hakieleweki.
Ikiwa in >50 years serikali ya CCM imeweza kufanya hayo tu tunahitaji karne nyiiingi sana tuweze kuwapa watoto wetu na watoto wa watoto wetu elimu itakayo wafanya waishi kama binadamu katika nchi yenye utajiri kama hii....tutahitaji karne na karne tuweze kuwapa watu wetu huduma bora za afya!
Ni ajabu unamsikia mgombea wa CCM(samia) anawahaidi watu eti wamejua shida ya wananchi wa singida ni masoko hivy o waichague ccm itawatafutia masoko ya vitunguu na alizeti...lol!
 
WAZIRI Mkuu mstaafu Frederick Sumaye ametangaza rasmi kuwa Edward Lowassa ni mgombea makini asiye doa, na anastahili kuchaguliwa ili aongoze taifa linalohitaji mabadiliko. Anaandika Jabir Idrissa … (endelea).
Amesema kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni chama kilichojifunika vyama viwili. Hakueleza kwa ufasaha tungo hiyo, labda akimaanisha chama hicho kinatumia mgongo wa dola kushikilia madaraka licha ya kukataliwa na wananchi kwenye uchaguzi mkuu.
​
Akihutubia mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya Lowassa anayegombea urais kupitia Chadema, kwa mamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) leo hii kwenye viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam, Sumaye alisema anamuunga mkono Lowassa.
“Niko pamoja na Mhe Lowassa. Niko pamoja na Ukawa… pamoja nanyi wana mabadiliko. Siku ikifika ya Oktoba 25, pigeni kura zenu kwa mhe Lowassa na tutashinda tu,” amesema.
Amemtetea Lowassa kuwa amekuwa akizushiwa kashfa zisizo zake wakati inajulikana hata ndani ya CCM kuwa alichukua uamuzi wa kiuwajibikaji ili kumhifadhi mkubwa wake.
Mkubwa wa Lowassa ni Rais Jakaya Kikwete ambaye alimtosa Lowassa alipolazimu kujiuzulu uwaziri mkuu Februari 2008, kutokana na shinikizo la Bunge lilipojadili ripoti ya uchunguzi wa mazingira ya mkataba wa kufua umeme uliopewa Richmond Development Company (RDC).
Lowassa ambaye ndiye waziri mkuu wa kwanza wa Rais Kikwete baada ya kuingia madarakani Novemba 2005, katika hotuba yake fupi bungeni alisema hakufanya kosa lolote lakini kwa kuona kuwa tatizo lililosumbua wabunge wengi ni yeye kuwa waziri mkuu, “nimemuandikia Rais kumuomba nijuzulu.”
Sumaye amesema kama Lowassa ni dhaifu basi aliyemteua kuwa waziri mkuu wakati ule, ndiye aliyekuwa dhaifu hasa. Lakini alisema Lowassa si dhaifu na ana kichwa chenye uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi.
Ametaja mlolongo wa kashfa zilizoibuka wakati wa uongozi wa Rais Kikwete, akisema hakuna hata moja ilimhusu Lowassa.
Baadhi ya kashfa hizo ni EPA (2005), Escrow (2014) kama mfano lakini akasema Lowassa alichokifanya wakati wa kashfa ya Richmond, ni kuihifadhi serikali.
Amemhfiadhi bwana mkubwa ambaye ndiye aliyebebewa mzigo katika kashfa ya Richmond.
Sumaye pia alizungumzia madai kuwa Lowassa ni mgonjwa. Alisema mtu akishapita miaka 50 anapata matatizo ya maradhi.
Lakini hata kama mgonjwa, urais unahitaji kiongozi kuwa makini tu, kazi zinafanywa na timu nzuri anayoiteua. “Kazi hii anaiweza Mhe Lowassa.,” amesema.
Sumaye akasema kwamba kama Lowassa anasemwa na viongozi wa CCM kuwa ni mgonjwa, kwani hawajui kuwa Magufuli ni mgonjwa? Anakwenda Ulaya kila mwezi kufanya nini,” alihoji.
Taarifa za ndani ya serikali zinasema kwamba Magufuli amekuwa akienda kubadilisha damu Ulaya kutokana na kuugua ugonjwa mkubwa ulio maarufu. Hatua hiyo ya kubadilisha damu kila mwezi inagharimu fedha nyingi ambazo analipiwa na serikali anayoongoza Rais Kikwete.
Elimu – serikali itagharamia elimu ya watoto mpaka chuo kikuu. Inawezekana, tunapoteza mabilioni ya pesa kwa mambo yasokuwa na maana yoyote.
Kilimo – tutatanua uzalishaji na kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji. Mazao ya chakula wakulima wakikopwa, watalipwa na riba. Hakuna kuwanyonya wakulima wetu.
Reli ya Kati – itajengwa iende mpaka Kigoma.
Tutafufua Air Tanzania (ATC), nia ni pamoja na kuimarisha sekta ya utalii.
Nidhamu ya kazi muhimu.
Masheikh wa Zanzibar na Babu Seya – naelewa hisia zenu. Tutaona namna vya kuwatoa kifungoni.
Maji vijijini, Vyuo vya Ufundi.
Naomba kura, watakaonipatia kura wanyooshe mikono… watu wanasema hivi, kura tutapata nyingi lakini zitaibiwa. Kwa hivyo,” akasimamishwa kwa shangwe ya Rais, Rais, Rais.
“Rais peke yake haitoshi. Kura, kura, ni kuhakikisha mnakwenda kupiga kura. Wameniuliza nitafutieni kura kwa watu wa Bara. Hata wakiiba wataiba nyingi lakini zitabaki nyingi za kutosha,” amesema.
Lowassa amefurahishwa na mapokezi, akisema hata wakubwa zetu, hawajapata mapokezi haya.
 
Magazetini asante kwa kutuletea update iliyo kwenda shule.

Tiba
 

Asituchoshe..warushe tu ile hotuba yake ya jangwani.
Ni kali sana...dah..
 
​Hasa nataka kujua mafisadi atawafanya nini?

Utayajua yote ndugu,mbona muda hupo Kampeni ndio zimeanza ukusikia leo utakuja kusikia siku nyingine,,pili Porojo tumezizoea kwa Viongozi tukiona wanakenua kenua meno kwenye majukwaa ndio tunaona watakuwa watendaji wazuri,hakuna lolote,,Rwanda ,Kenya,Ethiopia,Uganda watu awapigi dogo siku hizi,,maneno machache..Vitendo..tuu..Tuliona Kupitia YouTube,Tv.kuhusu mji mpya wa Kigamboni ,kukamilika kwake ni 2030 leo hii ni 2015 tunakimbilia 2016 hata tipa moja la mchanga alijamwagwa Kigamboni mpk sasa.sasa kama Barabara ya mabasi ya mwendo kasi ,project imechukua miaka 5 sasa sijui 6 je kujenga Mji mpya tutachukua miaka mingapi,,?? Tumechoka.Hotuba kuelezea vitu kibao utendaji hakuna..Lowasa katoa vipau mbele Elimu Elimu Elimu...Kilimo .Afya..sasa huko tuendapo ndio tunapaswa kuomba Hawa Wagombe wapatiwe Midahalo waulizwe watafanya fanya vipi,..kututatulia Hizo kero .Midahalo ni mizuri sana kwa sisi wananchi tutaweza kusikiliza zaidi kutoka kwa Wagombea wenyewe wawili,.
 
Acha uongo wewe. Pale Jangwani John Mrema alisema kuwa mkutano huo wa ufunguzi wa kampeni utarudiwa kwenye kituo cha ITV kuanzia saa tatu usiku. Wewe unakuja na ngonjera zako

Acha Ubishi, tune to ITV. Anarudia Ile Hotuba lakini akiwa Studio full AC na Kabrasha la Hotuba anasoma
 
Unapoandika thread humu uache bias ili ujumne ufike kwa walengwa na waupokee na wauchambue ili UPATE MAJIBU HALISI NA SIO YA KINAFIKI. Vipaumbele vya Taifa sema wewe ndio huvifahamu usiseme watanzania hawafahamu. Alafu Lowassa angetanguliza katiba nngemuona mjanja ila kwa uzembe wake anasema elimu wakati vituvingine kwenye elimu vingkua bora zaid kama angerekebisha katiba kwanza.

alafu mnapoiponda CCM mara zote kua inaahidi vitu vilevile kwani leo mmeongea nini kipya? au kufungua wafungwa na kufufua wafu ndio kipya?

Lowassa ni mnafiki kwa sababu watanzania siku zote wanaimba wimbo wa balali kwanini asingejitokeza aseme kama anajua balali alipo? Leo ili kuawahaada wananchi anawaambia nitalishughulikia. Tunahitaji sera na sio ahadi za mipira yenye sura yako, kufungua wafungwa na kufufa wafu.
 
Lowasa jina kubwa hakuna la maana analoongea alafu akikosa urais watalalamika kuwa wameibiwa kura.....
 

Sasa mkuu kwani UKAWA hawakujua leo wanakujakufanya nini? hawakujua kama mgombea wao anaitaji muda wa kutosha kuwaambia wananchi nini atawafanyia?
 
Lowassa hana jeuri ya kumjibu mwakyembe ataumbuka vibaya ile report ya Richmond imeacha vitu vingi kuvisema kwa ajili yake na kuiokoa serikali that time.

Hapo pa kuiokoa serikali ndio pazuri sana
Sasa Mwakyembe aseme nini alificha na kwanini alificha ili kuiokoa serikali. Lowassa hakuwa na sababu ya kumjibu kwani mara ya mwisho kama una kumbukumbu nzuri Lowasa akijibu swali kuhusu uhusika wake richmond, alikana kuhusika na akatupa mzigo kwa mkuu wa kaya. Na akasema mwenye ushahidi aende mahakamani vinginevyo afunge mdomo.

Kwa maana hiyo ni Mwakyembe ndiye anatakiwa aende mahakamani ua afunge mdomo wake. Yeye ni mwanasheria hapaswi kuongea kwenye kampeni jambo ambalo anadai ni jinai. Huo mkutano wa kampeni sio mahakama. Aende mahakamani kama naye una huo ubavu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…