Chekechea na Primary nimesoma english medium private
Sekondari Form 1 hadi 6 nimesoma Boarding private, Msosi Pilau kila J5 na J2, Ugali ni nadra sana.
Chuo kikuu sikupata mkopo ila si haba sikuwahi kupata changamoto za kiuchumi.
Nilipokuwa baba uchumi haukuwa vizuri ila nikaanza kuwaza watoto waje kusoma KAYUMBA ??? Kwa maisha niliyopambaniwa niyaishi kupanda magari ya njano, watoto waanze kutembe na vidumu??
Ndipo nilipoanza mapambano ya ziada kuwaandalia watoto future, yote hii ni kukwepa aibu.
Nina watoto watatu napambana mno watoto wasije pitia maisha ambayo mimi sikupitia,
Hivi hata wazazi watanichukuliaje aisee ?? Baba ulisomeshwa kwa raha watoto usomeshe kayumba ??
Shule nilizosoma zilirahishia maisha yangu ya shuleni,
- Vyoo visafi kila siku vinasafishwa
- Chakula kizuri shuleni
- Mazingira tulivu
- Usafiri shuleni hadi nyumbani
- kutumia kiingereza kwenye masomo tangu shule ya msingi
- Kila mwanafunzi ana kiti na dawati lake
- Hakuna kujazana darasani
- kujifunza computer utotoni
- Library
- masomo ya kupika, kushona, kuchora, n.k.
- Marafiki wengi hutokea familia zinazojali malezi
- n.k.
Hadi sasa napambana sana japo kipato si kikubwa.
Mtoto moja yupo form 1 ada milioni 2 na nusu kwa mwaka
Moja yupo Primary ada laki 9 day.
Huyu mwengine nae soon anaanza shule hio ya laki 9
Sina mpango wa kuongeza mtoto wa tatu labda uchumi ukae sawa
Ninajua zipo shule za bei rahisi mfano kuna shule za serikali za englsh medium, shule za sekondari za jumuia ya wazazi, n.k. kwa research yangu zimetofautiana kidogo na Kayumba.
Kwa sasa nina miaka 36 kiuchumi bado najibana sana hasa kwasababu bado najenga ili nihamie kwangu, imenibidi nitembelea IST ili kupunguza gharama za mafuta, wife ana passo, Simu yangu ina miaka mitatu sijabadili, wife nae nashukuru anajua tunayopitia nae kapunguza vizinga