Kutoka rubani wa ndege nchini Marekani hadi muokota makopo nchini Kenya

Kwahio mifano yooote umeona huo wa round ndio unafaa πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€. Acha uhuni kijana
 
Mkuu, hii story nadhani mhusika hajaeleza yote... nitafafanua. 1. Kweli mtu mwenye exposure, tena ya USA, na umefanikiwa kusoma na kumaliza urubani na kazi umefanya halafu hujui process za kupata kazi nchi nyingine? Ilikuwaje akakurupuka kurudi bila kufanya research ndogo ili ajue upatikana kazi ukoje na sifa zake. Kwa pilot mwenye ujuzi unaweza kuulizia hata ukiwa USA eg Kenya Airways na wakakupa process zote kwani ku-train pilot from ''nothing'' ni gharama. 2. Kwa nini aliondoka bila makubaliano na kukata mawasiliano na familia yake? Na baada ya kuona mambo hayaendi vizuri kwa nini hakurudi? Kwangu mimi naona huyu jamaa kuna vitu anaficha kwenye habari nzima.
 
Unaachaje kazi huna kazi nyingine,

I believe hii ni stori alioamua kushare ila kuna mengi zaidi ya hayo,

Kwa akili ya kawaida angeomba likizo ya mwaka, akaja Kenya akajisajili akakamilisha usajili then ndo atafute kazi, akipata ndo harudi USA, angekosa angerudi kuendelea na kazi yake
 
Kwahio mifano yooote umeona huo wa round ndio unafaa πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€. Acha uhuni kijana
Mimi nimezeeka Mkuu, hapa nimejaribu kutoa mfano rahisi ili vijana wa hivyo waelewe kwamba, wakiona wameanza kwenda round moja badala ya tatu, wajue wameshaanza kuufikia Umri wa Mzee Grahams hapa πŸ€—
 
Makosa ya Samweli
1. Kitokurudi nyumbani kuwaona Sponsor wake ( Kanisa) ma kumpa baraka zao za kazi mpya.
2. Kuoa mzungu nafikiri bila ridhaa ya wazazi wake

Waafica wengi walioenda Ulaya na kuoa huko wamerudi tupu - Mzungu hakupi watoto wake sahau. Sheria za huko zinamlinda sana Mke na watoto.
 
Hapana Aisee!!!

Ukioa Mzungu kubali uwe mtumwa labda ndiyo itakuwa salama yako.
Hakuna kitu kama hicho labda wale ambao huokotwa Africa na wasiojiamini, Wazungu(kwa shuhuda zangu mimi) wanajielewa na hawana longolongo. Washenzi wapo pia kama ilivyo kwa Afrika lakini huku niseme around 90% ya Waafrika wamefaidika kutokana na kuoa Wazungu.
 
SEKUNDE 60 TU(1)βœ…οΈ
Sekunde 60 tu. Hizo ndizo zilitosha kubadilisha mustakabali wa vita vya nyuklia, kuiaibisha moja ya mataifa yenye nguvu kubwa za kijeshi Mashariki ya Kati, na kuonyesha tena kwamba linapokuja suala la kulinda watu wake, Israel haifanyi mzaha.
Gari jeusi aina ya sedan linaendesha polepole kwenye barabara tulivu mashariki mwa Tehran.
Ndani ya usukani ameketi mwanasayansi wa nyuklia anayechukuliwa kuwa hatari zaidi duniani. Mtu ambaye ametumia miaka 30 akijenga kwa siri bomu la atomiki la Iran. Mtu ambaye jina lake lilikuwa siri kwa miongo kadhaa, ambaye sura yake haikujulikana duniani, ambaye alisafiri ndani ya Jamhuri ya Kiislamu kama kivuli akilindwa na askari 11 wa walinzi wa Mapinduzi na mfumo mzima wa usalama wa Iran.
Mke wake ameketi kiti cha mbele upande wa abiria, umbali wa sentimita 25 tu kutoka kwake.
Hajui kwamba tayari kuna silaha inayolenga moja kwa moja uso wake.
Hajui kwamba kamera iliyofichwa ndani ya lori lililoegeshwa tayari imemtambua.
Hajui kwamba umbali wa kilomita 1,600 upande mwingine wa Mashariki ya Kati, mpiga risasi anamtazama kupitia picha ya moja kwa moja ya satelaiti.
Kidole kikiwa juu ya kitufe cha kufyatua risasi kitakachorusha silaha ambayo hataisikia, kutoka nchi ambayo hataiona.
Gari linapunguza mwendo kupita kwenye speed bump, mfumo wa AI unamfungia lengo, na kutoka mbali kabisa kitufe kinabonyezwa.
Risasi 13 zinapiga gari hilo. Gari linapoteza mwelekeo na kusimama. Dereva anatoka nje akijaribu kujificha nyuma ya mlango uliokuwa wazi.
Risasi tatu zaidi zinampata, zikipasua uti wa mgongo wake. Anaanguka chini kwenye lami.
Mke wake, aliyekuwa umbali wa sentimita 25, haguswi kabisa. Hakuna hata risasi moja inayompiga.
Operesheni nzima inaisha kabla walinzi wake hawajajua hata risasi zimetoka wapi.
Kwa sababu hakuna wapiga risasi.
Hakuna kikosi cha kuvizia.
Hakuna mtu yeyote ardhini.
Kilichokuwepo ni mashine, kamera, algorithimu, na moja ya mashirika ya ujasusi yenye ujasiri mkubwa zaidi duniani, likifanya operesheni kutoka upande mwingine wa dunia.
Hivi ndivyo Mossad ilivyomuua baba wa bomu la nyuklia la Iran.
Na njia waliyoitumia haikumaliza tu maisha ya mtu mmoja.
Ilibadilisha kabisa kanuni za vita vya kisasa.
 
Anachangia nchi yake kama alivyotaka.

Hizi habari za kurudi Africa kuchangia maendeleo mimi nilizikataa.

Kwa sababu unaweza kurudi Africa ukafa kwa kukosa kazi, wakati uliweza kuisaidia sana Africa ukiwa unafanya kazi Marekani.

Huyu jamaa kuna sehemu kafanya ujinga, Wakenya wana tabia ya kuchangiana sana, kashindwa hata kuitisha Harambee asaidiwe kukamilisha vigezo vya kuwa rubani?

Kuna matatizo gani hayaongelewi hapa?

Intelligent businessman
 
Huyu jamaa alizingua. Kwani kubaki US angekuwa hajengi Kenya? Kenya inapokea misaada mingapi ya kodi za America?
 
Jamaa ali under-estimate mambo. Na labda alifanya maamuzi kwa hisia zaidi.
Lakini, nashangaa baada ya kuona mambo yanakua magumu Kenya, alishindwaje kupiga U-Turn na kurudi Marekani haraka? Inasikitisha sana.
Hizo Hela za kurudi alikuwa nazo !? Bank wamesha Kombat gari
 
Witnessj upo !? Duh kitambo sana
 
Umeongea mambo mazito sana, kiasi kwamba Umenikumbusha mambo mengi sana kuhusu maisha ,

Lakini binafsi yangu kutokana na ambayo nimewahi kuexperiance Kwa kuona kusikia na kupitia Mimi mwenyewe siwezi kuthubutu hata kidogo kumlaumu huyo Mzee

Na mara nyingi watu wengi wasicho kijua Huyo Mzee itakuwa ana sumbuliwa na issues za ancestors wao ,

Ukiwa una sumbuliwa na hayo mambo halafu ukaenda nayo against kuanguka from hero to zero ni jambo dogo sana hata uwaje , Yaani ancestors Huwa hawana masihara lazima wakufilisi na kukudhalilisha hakuna kitu utakacho weza kukifanya na ukafanikiwa, Kila unacho kifanya wanaweka barrier utajua haujui

So he's not normal,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…