Wanywa komoni wanakwambia hii shule ambayo wanafunzi hawana vyoo wanajisaidia kwenye makuti huku wakiwa hatarini kudumbukia kwenye kinyesi, ni shule ya maana sana kuliko English Medium ambapo mazingira ya kujistri yanazingatiwa maana mzazi analipia huduma bora.
View attachment 3205711
Kisha wanadai hawa wanafunzi ambao hata madawati ya kukalia hawana, wana ufaulu sawa na wale wa English Medium.
Hapa kuna mayaya/mabeki tatu/wadada wa kazi za ndani wa kutosha hapa
View attachment 3205712Pia unaambiwa na hao wavivu kwamba shule kama hii ni sawa na EM na mwanafunzi wa hapa kiakili, kisaikolojia, kimaarifa anatoka sawa
View attachment 3205714
Zaidi ya hao, unaambiwa na hao wanywa kimpumu kwamba wako radhi watoto wao wasomee mazingira kama haya kuliko walipie ada EM
View attachment 3205715
Hao wazazi ni ukoo wa wale Waafrika ambao zamani babu zao walikuwa waganga na wachawi. Wamerithi akili za kichawi vizazi hadi vizazi na ndio haohao baba akiwa na biashara hataki kabisa watoto wake waziguse, hataki waendeshe gari lake wala walala vizuri kwake. Utasikia "kajenge ya kwako ulale na kuamka saa mbili; usiguse gari langu, nunua lako; sitaki kabisa mguse hiki, nawewe tafuta cha kwako".
Hawa wavivu wana ugonjwa kuamini shida na mateso ndio maisha halali, wako radhi wahonge malaya uko vilabuni ilhali watoto wao wanasoma shule ambazo wanafunzi wanajisaidia vichakani.