Lengo la dini ni kuleta uongofu kwa watu, lakini kwa Afrika Dini zimelete Upotofu! I'm so sorry to say this!
Sutajadili kwanini nasema hivi ! na wala sijadili mada yoyote kwa jicho la imani.
Ugaidi ni neno lililopoteza maana halisi, linatumika kuhalalisha 'justify' udhalimu dhidi ya Wengine
Ikiwa kuna Ugaidi, Marekani na nchi za Magharibi ndizo magaidi wakubwa!
Mzozo wa Palestina na Israel una zaidi ya karne, hivi karibuni ni miaka takribani 75.
Mzozo wa Usrael na Hamas una zaidi ya miaka 17. Leo watu wanadhani ni tukio la saa 72 zilizopita.
Mzozo ulianza baada ya HAMAS Kushinda Uchaguzi, Marekani ISRAEL na nchi za Magharibi zikakataa licha ya Mwangalizi Rais Jimmy Carter kusema HAMAS Wameshinda. Kilichofuata Israel ikaweka Gaza katika vikwazo.
Katibu mkuu UN akasema Gaza ni open air prison. Maji, Umeme na kila kitu kinafika Gaza kwa ruhusu ya Israel
Hakuna uhuru wa kutoka Gaza kwenda pengine ila kwa kibali cha Israel. Hakuna kuvua samaki bila kibali.
Tonny Blair , PM wa UK alisema hajawahi kuona eneo lenye dhiki na mateso kama Gaza
Israel wamepiga Gaza kila siku, na wanaofuatilia habari wanajua jinsi akina Mama wa Kipalestina wanavyopiga vifua kwa uchungu wa kuuliwa 'watoto wao wa miaka 0-15Years.
Israle wanasema hiyo ni '' Collateral damage'' yaani vifo visivyohusiana na vita au kwa kiswahili ' Vita haina macho''
Mwaka Jana Wapalestina 255 wamuawa na Israel! Mbona hatukuona nyuzi za kuongelea ugaidi?
Western Media hazikuonyesha! Eti leo tunasema kuna tatizo limetokea kwasababu lipo Israel!
Israel inalaani kuuawa kwa Mwanahabari! Mwaka Jana Israel ilimuua Shereen Abu Akleh wa Al Jazeera Dunia ikakaa kimya. Leo HAMAS ni magaidi kwa kuua mwanhabari, Israel iliyoua mwaka jana ni Taifa teule!
HAMAS wanaitwa magaidi kwa kurusha makombora, Israel wanapewa Bilioni 3 na Ultra modern military equipments na Marekani kuua Wapalestina! hilo hamlioni! Mumepumbazwa na neno ugaidi
Israel Imeua kiongozi wa Iran wa Nyuklia Mohsen Fakrizadeh, na kamanda wa majeshi Qasem Soleiman hilo watu hawakuona ni tatizo, leo Iran inaonekana tatizo!
Dunia yote inaona,si zaidi ya nchi 20 zimelaani tukio la juzi. Hii haina maana zingine zinakubaliana na mauaji, ina maana kwamba huwezi kulaani HAMAS kwa kuua watu wakati Israel Inaua kila siku na dunia imekaa kimya.
Israel ikiua Wapalestina , yenye na Marekani wana 'standard statement inayosema Israel has the right to defend' siyo kwamba inafanya ugaidi! HAMAS na Wapalestina nao wanasema 'they have the right to resist ''
Sikubaliana na maujai ya Raia wa aina au upande wowote, lakini msiwe 'blind folded' kwamba HAMAS wameanzisha tatizo na kwamba Israel wanaonewa! no! Fuatilieni habari kwa kina misikurupuke na headlines
JokaKuu The Boss