Kuwapa watoto majina ya kigeni Kizungu/Kiarabu ndio usasa au kutojitambua?

Waafrika tumepoteza dira , angalia mtu anaondoa ngozi yake ya asili ili aonekane Kama mzungu ! Ni uuuuungwana ?
 
Mwita hapa kutoka mara

Mtu mrefu ajabu.

Jina la kiyahudi naitwa solomon.

Hakuna mwafrika mwenye jina moja katika zama hizi za kubatizana

Tushatishwa bila ubatizo na kuzaliwa upya huendi mbinguni
 
Mkuu mbona Povu???
Mwanao umemwita Lulu nini
 
Wakoloni wamefanikiwa sana kutawala Afrika enzi za ukoloni baada ya mkutano wa berlini na sasa kiuchumi na kifikra.

Silaha moja wapo kubwa ya kumtawala mtu ni kumfanya aache asili yake na utamaduni wake audharau afuate wako. Ukimaliza hatua hiyo hatokuwa na nguvu ya kukupinga tena.

Wazungu wamefanikiwa katika hilo, leo majina ya asili, dawa asili, chakula asili, utamaduni asili unaonekana ushamba au ni uchawi...vyakuja vinatukuzwa, hakika tupo katika hasara.

Kina chief Mkwawa na Kinjikitile huko walipo wanasikitika walipigana bure tu.
 
Mimi nimeita wanangu majina ya kienyeji

Jambo la kuchekesha watu ambao ndio nilitakiwa niwacheke eti wao ndio wananicheka mimi, hapo ndio nilipojenga tabia ya kuwapangia kama wanavyonipangia

Yaani mtumwa wa kifikra ananicheka niliyejitambua, sijui weusi tukoje
 
Wanyakyusa hatunaga shobo na uzungu
 
Mwita hapa kutoka mara

Mtu mrefu ajabu.

Jina la kiyahudi naitwa solomon.

Hakuna mwafrika mwenye jina moja katika zama hizi za kubatizana

Tushatishwa bila ubatizo na kuzaliwa upya huendi mbinguni
Usifikiri matatizo yako wote tunayo

Binafsi sina jina la kibeberu na haitakaa itokee huo moto wa milele mtachomwa mnaoamini
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]amepewa jina la kikatuni
 
Wewe mfuasi wa shetani.majina yote ni ya dini kuu mbili.uislamu na ukristo.sasa uafrika wako upo wapi?wahindi wanaabudu ngombe,wachina wanaabudu jua.isitoshe kama unao watoto wape majina unayoyataka.mmoja mwite mavi,mwingine mkojo,Ngombe,Kondoo,pakan.k. Upo huru.Sasa nimeelewa kwa nini makampuni ya simu yalipandisha gharama za Internet.mijitu inaandika upuuzi tu.
 
Umeamua kuandika matusi na hukuelewa nilichoandika,nimekusamehe
 
Sahizi mtoto ukimuita majina kama masanja, mabula, misoji, minza, rhobi na mengineyo mengi unaitwa mchawi pia unaabudu mizimu. Wengine huenda mbali na kudai mizimu ya mababu huwafuata watoto, acha tusonge hivi hivi.
Kwenye mizimu inaweza kuwa na ukweli mkubwa!

Unaweza kushangaa mtoto anaandamwa na mapepo kumbe jina tu la ukoo ulilompa ndio chanzo! Maana unamfungamanisha na maagano ya kichawi ya ukoo!

Bora umuite Bahati au furaha au malaika.

Unaweza kumuita mtoto majina kama Tanzanite, au Africa, au Dhahabu, au Almasi au simba nk.
 
Hata hao wachina wana majina ya kizungu,. Kiarabu na asili (roots). Kinacho kuchanganya ni lugha na herufi, kumbuka kila jina lina maana yake jaribu kutafuta dictionary halafu tazama tafsiri za majina na maana yake bila shaka huta hangaika kuelewa ni kwanini ulipewa jina ulilo kuwa nalo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…