Pre GE2025 Kwa anayoyaongea Lissu kuhusu uchaguzi, vyombo vya ulinzi na usalama vina machaguo matatu tu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Vyombo vya usalama kupendelea upande fulani ushike dola ni sehemu ya usalama pia kwa manufaa ya taifa. Ipo siku vyombo vya usalama vitachagua upande wa upinzani kuongoza nchi na itakuwa hivyo.
Sawa. Lakini tulipofikia sasa kuhusu chaguzi zetu ni pabaya sana katika hazipo huru na haki, pia zinaingiliwa sana na vyombo vya dola pamoja na ccm. Kitu ambacho kinatuweka katika hatari kubwa ya machafuko.
 
Vyombo vya ulinzi na usalama havifanyi kazi kwa maamuzi Yao bali vinatumwa cha kufanya na mamlaka iliyopo madarakani
Ni vyombo vya ulinzi na usalama wa Taifa au usalama wa ccm?
 
Usisahau huko kwenyewe kumejaa makada na wanachama watiifu wa ccm hakuna chochote watafanya zaidi ya kufuata maagizo ya kulinda maslahi ya chama chao
Hayo ndiyo mabadiliko anayoyazungumzia Ndugu Lisu. Tuvibadilishe vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kutoka kuwa ulinzi na usalama wa ccm kuwa ulinzi na usalama wa Taifa.
 
Kama ni kweli, siku yakitokea machafuko Jeshi letu litakuwa limehusika kusababisha machafuko hayo.
 
Ni machawa au we ye vinadaba vya uchawa ambao wanawezacwasijueleqe au wavhague tu kutokukuelewa.
Mimi nimekuelewa na ninaunga mkono hoja hii makini; ukweli hakuna mwanaCCM anayeweza kujibu hizi hpja mujarab.
 
4. Walimu wasisimamie uchaguzi!

Hoja za kipuuzi kabisa. Kuna vyama zaidi ya kumi vilivyosajiliwa ikiwemo CCM. Vitashiriki
 
Watathubutu? Wakienda tu baada ya masaa 24 watakuwa under house arrest na hiyo Asali kupewa wanaotii amri. Wewe umezaliwa lini huwajui CCM?
Binadamu tumeumbwa kutafuta kilicho bora. Hapo si swala la umezaliwa lini. Tunachotakiwa kufanya kama Taifa ni kutafuta Katiba bora, itakayotupatia Viongozi Bora na maendeleo ya kweli kwa mtu mmoja mmoja.
 
Kwa hiyo tuendelee na katiba hii iliyopo ili tu ccm waendelee kubaki madarakani na ndugu na Jamaal zao waendelee kupata ajira serikalini na wale wasiyo na ndugu na waliyo nje ya ccm waendelee kupata tabu. Kama ndiyo hivi! Tanzania tunasafari ndefu sana ya kujikomboa.
 
CCM waelewe wanachi tumechoka kuburuzwa kibwege- bwege na chaguzi ambazo hazina maana yaani kabla ya uchaguzi kuanza basi mshindi anajulikana sasa huo kama si ubwege ni nini.

Tarumbeta / baragumu lishapigwa na Lissu. Tunakwenda kuikomboa Tanganyika yetu kuwa na chaguzi za kweli, huru na haki, asiye na mwana aeleke jiwe, mwenye watoto mapacha wawili wote awaweke mgogoni, mkulima abagae jembe begani, mfugaji aswage mifugo yake mbele, mwalimu ashike chaki mkononi, mhudumu wa bar ashike opener, mama ntilie abebe masufuria- ni shime shime.
Atakayerudi nyuma kudai mageuzi haya hatufai hata kidogo, ni msaliti lofa na si mtanganyika halisi.

Lissu kashatangulia, wazalendo wote tumfuate.
 
Endelea kuviamini Vyombo vyetu vya Usalama ndio maana Nchi yetu ni tulivu
Na ku.buja kuwa kuwapo kwa utulivu haina maana kuna amani. Amani ni tunda la haki na kwa sasa kuna utulivu tu ambao ni matokeo ya woga wa wananchi hasa baada ya kuwa na vyombo vya ulinzi na usalama vinavyofanya siasa.
 
The Last Trumpet
 
Uliouandika ni ujinga mtupu
 

"Wakati CCM tulipokubali Mfumo wa vyama vingi tulihakikisha kwamba hatushindwi."
Ali Hassan Mwinyi, aliyekuwa Rais wa Pili wa Tanzania
 
Kwa maoni yangu naona umenena vyema sana, tatizo ninaloliona kwa nchi za wajamaa ni kuchanganya, makada wa vyama na vyombo vya dola. Inafahamika kwamba wakuu wa mikoa na wilaya ni makada wa ccm ,hapo hapo unakuta ndio wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama wa mikoa/wilaya husika. na unakuta wengine wana vyeo vya kijeshi au ni mapolisi sasa hapa panatuchanganya. uwezekano wa aliye na buyu la asali akukabidhi ulambe wewe yeye akiangalia shida inaanzia hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…