Hizo story ilikuwa zamani, kwenye chaguzi tunaona kinachoendelea Wala sio Siri tena. Ccm inaigiza kufanya siasa kwa sababu kinapata upendeleo wa Dola kufanya siasa. Lakini uhayawani unaoendelea kwenye chaguzi zetu, haukipi jeuri ccm kuwa inakubalika hivyo. Na kadiri uchaguzi unavyotokea kuheshimiwa, ndio ccm inavyopoteza uwakilishi wake.
Ndio maana tunataka tume huru ya uchaguzi, ambayo itaweka uhalisia wa ccm kukubalika kwake. Na kwakuwa ccm inajua ukweli huo haiko tayari kwa tume huru ya uchaguzi, Wala katiba halisi ya wananchi. Machafuko tu ama mapinduzi ya kijeshi ndio yataionyesha ccm Iko mazingira gani hapa nchini.