Kwa dhuluma ambayo Jakaya Kikwete alimfanyia Mzee Lowassa, ataumaliza uzee wake bila amani

Tunazungumzia urafiki mungu kaingiaje hapo .kikwete hakukata jina ssbabu et hafai sasa alimpaje uwaziri mkuu ? Ni roho ya kiburi na wivu kuwa lowasa anakubalika kumzidi.
 
Lowasa alikuwa mgonjwa kila mtu alikuwa anajua
 
📝🤝👍👏
 
1. Mabaya ya Kikwete tumeyasema mengi sana. Ukibisha nitakuwekea hapa ushahidi. Mimi namsema Kikwete vibaya au vizuri kulingana na hoja. Mimi si mtu wa kusema kwa fashion au mkumbo.

Kikwete tumemsema kuanzia udhaifu wake, matumizi yake mabaya ya fedha za umma mpaka safari zake zisizo idadi. Tangu kabla hajawa rais enzi za "Kumkoma Nyani Giladi" mpaka kesho tutamsema. What are you talking about?

2. Kusema Kikwete alikuwa mtu wa Saigon ni kumtetea? Kivipi? Kusema Kikwete alikuwa mtu ambaye akipata scandal anasema "huu ni upepo, utapita tu" ni kumtetea? Kivipi? Kiongozi anayesema "huu ni upepo tu, utapita" baada ya scandal ni indifferent. Mimi kumuita kiongozi indifferent naona si sifa nzuri. Ni sifa mbaya, kwamba huyu kiongozi hajali. Anaziba masikio kwenye scandal. Sasa kumuita kiongozi hajali, anaziba masikio kwenye scandal ni mumtetea?Mbona tunaona jambo lilelile tofauti sana?

Unajenga hoja kwa mantiki au unalalamika kwa hisia tu?

Unasoma ninachoandika au unachotaka wewe niwe nimeandika?

3. Nimetoa mfano wa case moja ambayo Kikwete hakuijua ya Maxence Melo alivyoshikwa. Hii case naijua kwa sababu niliishughulikia kampeni yake ya kinataifa. Na Kikwete ndiye aliyeamuru Max aachiwe. Nikasema kutakuwa na nyingine nyingi kama hizo. Pia sikumtetea Kikwete moja kwa moja nikasema kuna cases nyingine Kikwete anapata political expediency na advantage anazifumbia macho, na kwa hizo siwezi kumtetea. Hapo napo nimemtetea Kikwete?

4. Kikwete nafahamiana naye kwa karibu? Wapi? Kivipi? Kikwete kawa rais mimi nishaondoka Tanzania. Wakati niko Tanzania Kikwete was mostly a nobody. Mpaka 95 anakuja kugombea urais tukashangaa, hata huyu naye anataka kuwa rais? Wakati kawa rais anakuja New York City mambo ya UN nilikuwa naitwa sana kwa balozi kukaa naye Kikweye, jinsi nisivyomfagilia wala kutaka kuwa karibu naye nilikataa mara zote kwenda. Nilikataa nafasi zote za kukutana na Kikwete. Sasa ningekuwa shabiki wa Kikwete u avyoni paint hivyo, ningekataa kukutana naye? Kikwete nimemjulia wapi mimi?
 
JK inawezekana ana matatizo yake, mengi tu.

Lakini, kwenye hili la Lowassa.

Mimi sielewi kwa nini JK analaumiwa kwenye hili.
Mkuu watu hawapendi watu makini, smart na calculative. Kosa walilolifanya Lowassa na Magufuli ni kutafsiri upole na ucheshi wa Kikwete for weakness, a very fatal mistake!
 
Mkuu Lowassa alijiuzulu mwenyewe kweupe bungeni akisema, namnukuu "najua shida ni uwaziri mkuu"

Kikwete anaingiaje hapo??

Alikuwa anataka uwaziri mkuu wakati alikuwa Rais?

Kukurupuka kwake na hasira zilimponza! Ukweli ni kwamba hakuna anaye mfahamu Lowassa kuliko Kikwete mwenyewe!
 
Mwinyi alijiuzulu kwa kashfa ya polisi kuua raia.
Ni hivi.

Kujiuzulu si jambo baya. Linaweza kuonesha character.

Lakini, ukijiuzulu, umekubali makosa ama kwa kitu ulichofanya wewe mwenyewe moja kwa moja, ama kwa kitu ambacho ulitakiwa kusimamia kama kiongozi lakini hukusimamia vizuri.

Umekubali makosa.

Sasa, ukishakubaki makosa, hilo halina maana ni lazima watu watakutupa tu.

Lakini pia halina maana watu watakupetesha tu bila kujali kuwa ulijiuzulu.

Siasa ina mambo mengi. Unaweza kuibuka kidedea hata kama a compromise candidate.

Lakini, unakuwa unewaachia watu wengine waamue fate yako, you leave so much to chance, you taint your resume.

Watu wakikufanyia hisani kukuruhusu uwe rais, ni sawa na vizuri.

Lakini, kimsingi, unakuwa umeshawapa watu sababu ya kusema "huyu alishaharibu, tusimpe nafasi, ataharibu tena".

Siasa za kipindi cha Nyerere zilikuwa tofauti sana, zilikuwa more forgiving. Chama kimoja. Uteuzi uko wa siri sana. Rais mwenyewe mnamchagua mmoja kwa kura ya Ndiyo au Siyo. Mwinyi alipewa grace hiyo.

Tanzania ike ni tofauti sana na Tanzania ya vyama vingi.

Siasa za kipindi cha Kikwete zilikuwa za ushindani zaidi. Zilikuwa za one mistake one goal, saa nyingine unatengenezewa tu goal bika mistake kama Salim Ahmed Salim. Figisu tu.

Sasa, dunia ya figisu tupu, ukishajiuzulu ndiyo umewapa watu msemo kwamba huyu hafai, alijiuzulu.

Sasa hapo Lowassa kakubali kujiuzulu, kajipiga rusasi ya mguu mwenyewe kabla ya kuanza marathon, mlitegemea na yeye aturudishe nyuma kwenye siasa za enzi ya Nyerere kweli?
 
Mkuu farsasi anavumilia kuliko punda???? 🤣 🤣 🤣
 
🤣🤣🤣🎤🔊
 
Ujasusi ni kazi ngumu wewe laani wenzio wanakula Raha maana wanaishi kwa jina la jamuhuri.... So ilaani jamuhuri🇹🇿🤐
 
Hii kazi uliyojipa ya kuwajibia wengine unaamini utaiweza kweli?!

Mimi nimemjibu Kiranga kwa kujumuisha hoja zake wakati nikijadiliana nae, sijamjibu kwa kutumia post yake moja kama ulivyo copy wewe.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
- Kinachojadiliwa hapa kumhusu Kikwete ni issue yake na Lowassa, hayo ya zamani wachana nayo. Nikitazama majibu yako kwa hii issue, ndio nimekwambia nakuona umejigeuza msemaji wake kwasababu majibu yako ni kama unatuaminisha kwamba Kikwete hakuwa mtu wa visasi, yeye anaujua na kuupenda utani wa vijiweni.

Wakati kiuhalisia nimekuwekea yaliyotokea enzi za utawala wake, ukabadilika, ukahamishia lawama kwa wasaidizi wake, nikakuuliza tena, kama hakuwa mtu mbaya kwanini hakujitokeza kuwakemea hao wasaidizi wake wakati wa awamu yake, sikuona jibu lako.

- Nashangaa hapa unaniuliza swali dogo namna hiyo!, kwamba hukujua uliposema Kikwete alikuwa mtu wa "Saigon" na "kuacha upepo upite" hukuwa unamtetea?, hukujua kama kwa kusema kwako hivyo, ulituonesha tabia za Kikwete kwamba ni mtu asiyejali maneno ya watu? mpaka pale nilipokuonesha vile maneno ya wengine yalivyomkera akawaumiza wakati wa utawala wake?!

Hata kama ulitoa mfano mmoja wa case ya Melo, lakini nami nikakujibu kwa kukupa mifano yangu inayoonesha Kikwete alikuwa tofauti, hakuwa mtu wa kupuuza maneno kama unavyotuaminisha hapa, wakati mwingine alikuwa akijibu kwa vitendo.

-Hili la wewe mara zote ulipoitwa kwa balozi ukaonane na Kikwete ulikataa, ukweli unaujua mwenyewe, lakini haufiti wala kufubaza yote niliyokuandikia hapo juu. I rest my case.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Usijali sana nani kaandika, jibu hoja tu.

Ukianza kuangalia sana nani kaandika ndiyo mwanzo wa kufanya logical fallacy ya ad hominem.

Yani ndiyo mwanzo wa kuacha kujadili hoja iliyoletwa na kumjadili mtoa hoja kwa personal attacks.

Hoja ni kwamba umeambiwa Kikwete anazungumzwa pande zote, mabaya na mazuri yake.

Ubaya wa Watanzania wengi ni watu wa falsafa ya "all or nothing at all". No nuance.

Yani, wakimpenda mtu, wanampa mahaba yoote, hakuna kibaya watakachokiona kwake, wanamtetea kama ushabiki wa Simba na Yanga.

Na wakimchukia, wanamchukia moja kwa moja. Bila breki.

Ukiwapa watu mtihani wa kuorodhedha mazuri na mabaya ya Paul Makonda hapa, wengi wataweka mazuri tu au mabaya tu, kuweka mizani ni kitu kigumu sana kwa wengi.

Sasa tunapokuja wengine ambao tunaweza kuongea kwa nizani, siku moja Kikwete tukimtetea, siku nyingine tukimponda, kulingana na hoja, wasiompenda wengine wakiona tumemtetea wanaona huu ni ushabiki wao wa Simba na Yanga wa kila siku.

Come on man.

Some of us are more evolved than that.
 
Watu wa kaskazini wote walitaka Lowasa awe raisi haijalishi kupitia CCM au CDM.
 
Ni hivi.
Kujiuzulu si jambo baya. Linaweza kuonesha character.
Lakini, ukijiuzulu, umekubali makosa ama kwa kitu ulichofanya wewe mwenyewe moja kwa moja, ama kwa kitu ambacho ulitakiwa kusimamia kama kiongozi lakini hukusimamia vizuri.
Na pia kuna kujiuzulu ili kumnusuru Bosi na maswahiba!
Rais H.A. Mwinyi wa Zanzibar ameeleza, alimwandikia Rais Kikwete barua ya kujiuzulu uwaziri wa Ulinzi kutokana na milipuko ya Mabomu, na ilitokea mara mbili. Rais Kikwete alimkatalia kujiuzulu.

Kuhusu ENLowassa
Rais Kikwete alikuwa na uwezo wa kuita 'caucus' ya Chama chake kulijadili suala
Kikwete alikuwa na option ya kutishia kulivunja au kulivunja Bunge kama litamwandama Waziri mkuu wake
Rais Kikwete akiwa sehemu ya Bunge angeomba kwenda kulihutubia Bunge kwa kadhia hiyo.

Rais Kikwete hakufanya jitihada zozote na kumwacha ENL akikaangwa na Bunge.

Hapa simaanishi kwamba kulikuwa na makosa kumkaanga, la hasha lakini ni ukweli kwamba 'rafiki yake ' hakumsaidia. Pengine Kikwete alijua huo ndio utakuwa mwisho wa ushawishi wa ENL katika siasa za Tanzania

Lowassa alibaki na machaguo mawili, kwanza, akomae kutojiuzulu, Bunge limpigie kura ya kutokuwa na imani.
Kuondolewa kwa 'vote of no confidence' kungehitimisha ndoto na safari yake kisiasa once and for all

Pili, ajiuzulu kama sehemu ya kuwajibika na kuinusuru serikali ili apate nafasi mbele ya safari.
Hii ilikuwa '' viable option'' na tumeona ilimsaidia kurudia katika ulingo kwa mara nyingine akiwa na nguvu kubwa.

Kwanini Kikwete analaumiwa? Si kwasababu hakumpa mshirika wake Urais.

JK analaumiwa kwa mambo mawili, kwanza kumtosha ENL wakati alijua mafisadi walivyosaidia mtandao uliomweka madarakani. Kama Rais wa nchi , JK alijua mauza uza ya Richmond na walioko nyuma yake! alijua!

Pili, ENL alijijenga tena baada ya anguko la Uwaziri mkuu. Utaratibu wa chama ni majina kupitiwa na lenye kura nyingi linasonga mbele kwa mchujo zaidi. JK alijua ushawishi wa Lowassa.

Kwa kujua Lowassa hana Kikwakzo na ameshinda kwa uhalali na kwa kujua mbinu za kumzuia kwa kumuanguasha u-P,M zimeshindwa, JK akakata jina la Lowassa si kwa kushindwa bali kwa hiyana tena kinyuma na taratibu za upatikanaji wa mgombea.


Kikwete hakumdhulum Urais , alimdhulumu Lowassa kwa kuvunja taratibu zilizokuwa zinapeleka jina na Lowassa mbele. Alikata jina, Lowassa hakushindwa! hiyo ni dhuluma inayoongelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…