Kwa heri Chadema, sitakuwa siwezi kuwa chawa wa kumsafishia njia Samia

Mkuu, yn unataka mbowe aachie madaraka afu unataka mwanaJF mwenzetu Erythrocyte akale wapi 😂
 
Yale maandano yalikua geresha tu yalitakiwa yafanyike tanga sku tu baada ya kumzika kibao sio wiki tatu toka tukio amka usingizin ndo maana watu hawakwenda
Ishu ni je, yangeanzia huko Tanga ungelishiriki? Na uliwahi kushiriki maandamano gani kabla? Au yote yalikosewa? Ahahahahaha!!!
 
..kama ni hivyo, ipi ni good deal..kucompromise na ccm na kukiacha chama km Mashinji au kucompromise na kubaki kwenye chama..
 
Kwani katiba ya CDM ina ukomo wa kugombea mpaka useme ameamua kuongeza muda?
Kimsingi hajavunja katiba wala hajang'ang'ania madaraka kikatiba.

Lakini kwanini wale tunaoamini Mbowe anapaswa kupumzika tunaogopa kwenda nae kwenye sanduku la kura?
Tumpambanie Lissu ashinde kwenye kura na sio kumlaumu Mbowe kwa kugombea.
 
Ahsantee..💪
 
Kweli mbowe kibaraka,hadi wewe leo upinzani!!
 
Somo la muhimu kwa Mbowe ni kutengeneza succession planning.

Majibu yake kuhusu ilo swali alipoulizwa hayakuridhisha.

Mikakati ya siasa haitokani na mashabiki wa mitandaoni, bali internal strategies.

Kazi ya kuendesha na kulinda chama kwa uhalisia ni ngumu kushinda kusikiliza hadithi za watu wa mitandaoni.

Na kazi ya kuendesha nchi ni ngumu zaidi kuliko fikra za mitandaoni.

Magufuli hakuwa perfect, Iła Lissu alikuwa ni shida kwa national security zama za Magufuli.

Lissu huyo-huyo ni shida kwa mustakabali wa CDM sasa, kwenye kichwa chake life revolves around his nonsense without boundaries.

Siasa ni science na ina kanuni zake, ni watu wenye uelewa wa siasa tu ndio wanaweza ona madhara ya Lissu.

Miaka mitano ya mwisho ya Mbowe ana jukumu sasa la kujenga chama kupata viongozi sahihi.
 
Ndio ukweli, mabadiliko yataletwa na vijana kama wa Sri Lanka.
 
usimuweke mdhamana mwanasiasa!

na mageuzi/mabadiliko ya kweli hayaletwi na vyama vya siasa ni wananchi tu

ova
Mabadiliko mema na ya kweli na ya salama yalitakiwa kuletwa na wanasiasa kupitia wananchi..ila mabadiliko machungu na mabaya na magumu ndiyo yanaletwa na wananchi au jeshi pasipo wanasiasa ...hivyo hoja yako ni potovu .. wanasiasa pia ni wananchi pia wanatakiwa kuinua nguvu ya wananchi kupitia siasa
 
Mbowe kwa kujua au kutokujua ndiye ametumika kuiangamiza CHADEMA. Alitakiwa asigombee amuachie mwanachama mwingine mwenye nguvu za ushawishi na mwenye uthubutu wa kukabiliana na CCM bila unafiki
 
Hili baba li DJ mbowe liondoke. Sitapigia kura tena cdm chini ya mbowe. Kutoka kuitwa mwamba Hadi tapeli la kisiasa.
 
Lissu ana kazi ngumu sana🐼

 
Hii chadema ya mbowe tena itakuwa ni chadema toothless kwa ccm sawa na cuf ya lipumba iliyo mfu ndebendebe
 
Tanzania bara hakujawahi kuwa na upinzani wa maana,

wapinzani wengi sana wameweka mslahi yao binafs ndio maana mpk leo ccm bado inatawala uko bara na kuna majimbo mengi sana ccm inashinda kihalali kabisa,

hii inatokana kuwa bado wajinga ni wengi sana kwenye iyo nchi.

Afadhali kwa upande wa znz yakija masuala yenye maslahi ya nchi unakuta ata ccm wanatofautiana mitazamamo na wanapingana wazi wazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…