Mikopo Consultant
JF-Expert Member
- Oct 28, 2024
- 529
- 1,150
Sheria ya vyama vya siasa inataka vyama kupeleka taarifa zao za kifedha kwa msajili kila mwaka; kwakuwa vyama hivi vina maslahi kwa nchi, ningependekeza ofisi ya msajili kuzitoa taarifa hizo kwa umma wa watanzania, kuna viongozi wanastahili kufunguliwa kesi za matumizi mabaya ya fedha za umma.
Nimeshtushwa sana na hoja ya Wenje; kwa Chama cha Chadema kuchangiwa Milioni 250 na Mbowe, ambaye amekuwa mwenyekiti kwa miaka 20; hii ni hoja nzito kabisa ya kumpumzisha siasa huyu baba.
Kwa tafsiri ya kwenye biashara, Chadema haina cash flow za ku run operations zake za kila siku. Hii ni tafsiri ya taasisi iliyofilisika.
Lakini ukiwachimba sana Chadema, iliwahi kuwa na wabunge karibia 80 bungeni, maana yake hiki chama kina karibu muongo mmoja wa kujichotea pesa nyingi za ruzuku na misaada ya wafadhili nje.
Sasa hoja iliyoletwa na Wenje mezani kwamba chama kinakosa hata pesa za vikao kwa sasa, ina tafsiri ya uongozi ulioshindwa, na tukifukunyua zaidi - ikiwa msajili atatupatia taarifa za kifedha za hiki chama, yaani nahisi kabisa kuna viongozi wanatakiwa kwenye hichi chama kujibu kesi za matumizi mabaya ya madaraka.
Kama Lissu hajachanga, namuunga mkono kabisa, hata mimi nisingechangia hata senti tano, kuna haja kwanza ya kujua Chadema imefanyia nini pesa za ruzuku mabilioni ya shilingi..
Unaweza kushangwazwa eti chama kimetumia bilioni 3 kununua kofia, sasa huu si utoto kabisa huu, yaani waliacha kuwekeza hizi bilioni 3 kwenye bonds ambapo wangekuwa wanakula interest ya zaidi ya milioni 400 kila mwaka ambazo wala usingesikia kelele za kuomba michango.
Huyu mtu amechoka, apumzike kabisa.