Kwa hii kauli ya Wenje, Msajili Ashurutishe Vyama Vya Siasa Kuchapisha Taarifa zao za Kifedha Haraka Sana

Kwa hii kauli ya Wenje, Msajili Ashurutishe Vyama Vya Siasa Kuchapisha Taarifa zao za Kifedha Haraka Sana

Tatizo kubwa sana tena sana, kama umekuwa kiongozi wa chama kwa miaka 20 halafu bado unatoa pesa zako mfukoni, hiyo maana yake umeshindwa kuifanya taasisi kuwa na sustainability kwenye vyanzo vyake vya mapato.

Hii ni hoja nzito ya Mbowe kupumzishwa siasa na uongozi wa hiki chama
Na hapa duniani hakuna mchaga anaweza kuchezea pesa yake kijinga hivyo kama haizai. Mbowe ana biashara kubwa na CHADEMA pengine kuliko biashara NYINGINE yoyote aloyonayo.

Eti mchaga atoe 250mil hivi hivi!? Yule Mjaluo wa Shirati Kuna kitu anafanya na Mbowe
 
Issue sio mahesabu kukaguliwa, tunazungumzia busara za matumizi ya fedha nyingi walizokuwa wakipata. Kama walivuna mabilioni ya fedha na kiongozi wa chama hakuona busara kwa chama kuwa na sustainable cash flow kusaidia shughuli za chama wakati wote, hiyo ndo failure tunayoijadili.

CAG kukagua mahesabu mara nyingi ni kuhakikisha tu ikiwa taratibu za matumizi ya fedha zimefuatwa i.e. risiti za manunuzi zipo kwa usahihi etc, ila kuhusu busara ya matumizi ya fedha hilo sio jukumu la CAG. Kwahiyo kupewa hati ya ukaguzi na CAG, ni jambo lisilo na maana sana kwa muktadha wa kujadili busara na ubunifu wa viongozi kwenye matumizi ya chama.
Hawakuwa wanafanya biashara hiyo sustainable cash flow itoke wapi? Wao wanategemea ruzuku na ada za wanachama ziingie ndiyo revenues yao, kisha wanatumia kwa kufuata bajeti na wanapotumia zinaisha hiyo sustainability haiwezi kuwepo.
 
Sheria ya vyama vya siasa inataka vyama kupeleka taarifa zao za kifedha kwa msajili kila mwaka; kwakuwa vyama hivi vina maslahi kwa nchi, ningependekeza ofisi ya msajili kuzitoa taarifa hizo kwa umma wa watanzania, kuna viongozi wanastahili kufunguliwa kesi za matumizi mabaya ya fedha za umma.

Nimeshtushwa sana na hoja ya Wenje; kwa Chama cha Chadema kuchangiwa Milioni 250 na Mbowe, ambaye amekuwa mwenyekiti kwa miaka 20; hii ni hoja nzito kabisa ya kumpumzisha siasa huyu baba.

Kwa tafsiri ya kwenye biashara, Chadema haina cash flow za ku run operations zake za kila siku. Hii ni tafsiri ya taasisi iliyofilisika.

Lakini ukiwachimba sana Chadema, iliwahi kuwa na wabunge karibia 80 bungeni, maana yake hiki chama kina karibu muongo mmoja wa kujichotea pesa nyingi za ruzuku na misaada ya wafadhili nje.

Sasa hoja iliyoletwa na Wenje mezani kwamba chama kinakosa hata pesa za vikao kwa sasa, ina tafsiri ya uongozi ulioshindwa, na tukifukunyua zaidi - ikiwa msajili atatupatia taarifa za kifedha za hiki chama, yaani nahisi kabisa kuna viongozi wanatakiwa kwenye hichi chama kujibu kesi za matumizi mabaya ya madaraka.

Kama Lissu hajachanga, namuunga mkono kabisa, hata mimi nisingechangia hata senti tano, kuna haja kwanza ya kujua Chadema imefanyia nini pesa za ruzuku mabilioni ya shilingi..

Unaweza kushangwazwa eti chama kimetumia bilioni 3 kununua kofia, sasa huu si utoto kabisa huu, yaani waliacha kuwekeza hizi bilioni 3 kwenye bonds ambapo wangekuwa wanakula interest ya zaidi ya milioni 400 kila mwaka ambazo wala usingesikia kelele za kuomba michango.

Huyu mtu amechoka, apumzike kabisa.
CAG kila mwaka anavifanyia financial auditing vyama vyote vyenye usajili wa kudumu. Na kwenye ripoti ya mwisho ya CAG Chadema ilipata hati safi. Sijui unalijua hilo?
 
Back
Top Bottom